Gerson Msigwa atoa ufafanuzi upotoshaji wa wapinzani kuhusu takwimu za ajira

Ngaliwe

Senior Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
164
Reaction score
374
Uzushi huu hapa:
Wapinzani wamechukua na kuviunganisha vibango vinne vya mtandaoni (infographics) vinavyotengenezwa na Ayo TV vyenye taarifa ya idadi ya ajira zitakazotolewa na Serikali kwa nyakati tofauti huku vikionesha mkakanganyiko kuhusu jumla ya watu watakaoajiriwa na Serikali.

- Kibango cha kwanza kina picha ya Hayati Magufuli na maneno yanayosema: TUTATOA AJIRA MPYA MILIONI 8.

- Kibango cha pili kina picha ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na maneno yanayosema AJIRA MILIONI 12.

- Kibango cha tatu kina picha ya Rais Samia na maneno yanayosema: AJIRA MPYA ELFU 40.

- Kibango cha nne kina picha ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na maneno yanayosema AJIRA LAKI 5.

Lengo la wapinzani ni kuvunja imani waliyo nayo vijana (ambao ndio idadi kubwa) kwa Serikali yao ikiwa ni mkakati wa kujiongezea idadi ya kura ifikapo 2025.

Msigwa anena:
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa ufafanuzi kuhusu upotofu huo unaonezwa mitandaoni katika kipindi hiki ambapo Tanzania ina uhuru mkubwa wa kujieleza.

Ufafanuzi wake ni huu hapa:

- Kibango cha kwanza kinaelezea ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ambapo chama hicho kiliahidi kuzalisha ajira milioni nane katika sekta ya umma na sekta binafsi.

- Kibango cha pili kinaelezea mkakati uliopo kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2021/22-2025/26 ambapo ajira milioni 12 zitakuwa zimezalishwa.

- Kibango cha tatu kinahusu ajira 40,000 zitakazotolewa na Serikali mwaka 2021/2022 ambapo idadi hiyo itaajiriwa katika sekta ya umma.

Tuondoe Hofu:
Kwa hiyo, hakuna mkanganyiko wowote kuhusu takwimu hizo kwa sababu kiongozi anaweza kuzungumzia mambo tofauti. Mfano anaweza kusema viwanda vinne vitazalisha ajira laki 6.

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama inapenda kuona vijana wengi wanaajiriwa katika sekta mbalimbali.
 
Vijana wanaomaliza vyuo kwa mwaka mr msigwa ni zaidi ya 40,000. Sasa ukiwaambia vijana kuna ajira 40,000 hadi mwaka 2025. Unategemea watakuelewa kweli?
 
Vijana wanao maliza vyuo kwa mwaka mr msigwa ni zaidi ya 40,000. Sasa ukiwaambia vijana kuna ajira 40,000 hadi mwaka 2025. Unategemea watakuelewa kweli?
Ni serikali ya nchi gani inayoajiri vijana wote wanaomaliza vyuo? Ebu funguka tujielimishe
 
Mmmh binafsi naona wapinzani ndo wako sahihi ila msigwa amekaza fuvu tu ..all in all ajira ni tatizo kubwa Tanzania na duniani kwa ujumla
 
Mimi nawambia kwenye swala la ajira viongozi tuliopewa nafasi kwenye hizi wizara tutumie akili zetu tutengeneze ajira mpya hakika nawaambie we have to think beyond the box. Tuachane na siasa, mbona mambo ni mepesi tu.
Ninacho kijua tukipata viongozi wa wizara wenye maono wanao elewa taifa linahitaji nini swala la kutengeneza ajira ni jepesi mnoo mnooo.
 
Mimi nawambia kwenye swala la ajira viongozi tuliopewa nafasi kwenye hizi wizara tutumie akili zetu tutengeneze ajira mpya hakika nawaambie we have to think beyond the box. Tuachane na siasa, mbona mambo ni mepesi tu.
Ukosefu wa Ajira ni bomu na litalipuka mwaka 2025 kuelekea 2030
 
Kwa hiyo, hakuna mkanganyiko wowote kuhusu takwimu hizo kwa sababu kiongozi anaweza kuzungumzia mambo tofauti. Mfano anaweza kusema viwanda vinne vitazalisha ajira laki 6.
Hivi wadau mnaona haya maelezo yamekamilika...?
 
Nyumbu ni Shida.....! Habari Wanakuletea nusu ili Wakuchanganye.....!

Sioni maana ya huo ufafanuzi kifupi ajaeleweka hao wote ni viongozi wa Selikari hii hii tena zenye ilani moja unaposema unategemea kuzalisha ajira milion 8 ndani ya miaka 5 tulitarajia kuwe na wastani wa ajira mpya 1.6 million kwa mwaka so 40k ni kama hakuna kwenye 1.6 million.

Ila tunachoshukuru ni kuwa Mama anasema ukweli tofauti na hao wote angalau yeye anajitahidi sana kuwa mkweli nadhani sababu ni Muislamu maana hao wengine heheee.
 
Watu wameshaamka hakuna wa kumlisha ujinga tena. Sasa hivi uongo wa serikali ya majizi ya kura unazidi kuwekwa hadharani.
 
Uzushi huu hapa:
Wapinzani wamechukua na kuviunganisha vibango vinne vya mtandaoni (infographics) vinavyotengenezwa na Ayo TV vyenye taarifa ya idadi ya ajira zitakazotolewa na Serikali kwa nyakati tofauti huku vikionesha mkakanganyiko kuhusu jumla ya watu watakaoajiriwa na Serikali.

- Kibango cha kwanza kina picha ya Hayati Magufuli na maneno yanayosema: TUTATOA AJIRA MPYA MILIONI 8.

- Kibango cha pili kina picha ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na maneno yanayosema AJIRA MILIONI 12.

- Kibango cha tatu kina picha ya Rais Samia na maneno yanayosema: AJIRA MPYA ELFU 40.

- Kibango cha nne kina picha ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na maneno yanayosema AJIRA LAKI 5.

Lengo la wapinzani ni kuvunja imani waliyo nayo vijana (ambao ndio idadi kubwa) kwa Serikali yao ikiwa ni mkakati wa kujiongezea idadi ya kura ifikapo 2025.

Msigwa anena:
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa ufafanuzi kuhusu upotofu huo unaonezwa mitandaoni katika kipindi hiki ambapo Tanzania ina uhuru mkubwa wa kujieleza.

Ufafanuzi wake ni huu hapa:

- Kibango cha kwanza kinaelezea ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ambapo chama hicho kiliahidi kuzalisha ajira milioni nane katika sekta ya umma na sekta binafsi.

- Kibango cha pili kinaelezea mkakati uliopo kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2021/22-2025/26 ambapo ajira milioni 12 zitakuwa zimezalishwa.

- Kibango cha tatu kinahusu ajira 40,000 zitakazotolewa na Serikali mwaka 2021/2022 ambapo idadi hiyo itaajiriwa katika sekta ya umma.

Tuondoe Hofu:
Kwa hiyo, hakuna mkanganyiko wowote kuhusu takwimu hizo kwa sababu kiongozi anaweza kuzungumzia mambo tofauti. Mfano anaweza kusema viwanda vinne vitazalisha ajira laki 6.

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama inapenda kuona vijana wengi wanaajiriwa katika sekta mbalimbali.
Heri iwe nawe!
Si halali kupotosha umma mkuu. kibango cha pili kinazungumzia juu ya ajira zilizozalishwa 2016/17 mpaka 2020/21
Screenshot_20210503-001816.jpg

(source: hotuba ya WFM 2021)

Kuna wakati mzee wangu alipenda kuniambia "usiambe ukasuku" hakuna jambo baya kama kuamba ukasuku ndugu yangu. unacheza ngoma usoijua.

Labda nikuchekeshe tu kuna kibango hakipo. Hiki tukiite kibango cha kurasa ya 27 chenyewe kinadai ajira zilizotengenezwa ni usita milioni apa bila shaka kulikuwa na hesabu za kugawanya kwa mbili toka kwenye milioni kumi na mbili
20210503_003340.png
 
1619993322525.jpeg

Uzushi huu hapa:
Wapinzani wamechukua na kuviunganisha vibango vinne vya mtandaoni (infographics) vinavyotengenezwa na Ayo TV vyenye taarifa ya idadi ya ajira zitakazotolewa na Serikali kwa nyakati tofauti huku vikionesha mkakanganyiko kuhusu jumla ya watu watakaoajiriwa na Serikali.

- Kibango cha kwanza kina picha ya Hayati Magufuli na maneno yanayosema: TUTATOA AJIRA MPYA MILIONI 8.

- Kibango cha pili kina picha ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na maneno yanayosema AJIRA MILIONI 12.

- Kibango cha tatu kina picha ya Rais Samia na maneno yanayosema: AJIRA MPYA ELFU 40.

- Kibango cha nne kina picha ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na maneno yanayosema AJIRA LAKI 5.

Lengo la wapinzani ni kuvunja imani waliyo nayo vijana (ambao ndio idadi kubwa) kwa Serikali yao ikiwa ni mkakati wa kujiongezea idadi ya kura ifikapo 2025.

Msigwa anena:
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa ufafanuzi kuhusu upotofu huo unaonezwa mitandaoni katika kipindi hiki ambapo Tanzania ina uhuru mkubwa wa kujieleza.

Ufafanuzi wake ni huu hapa:

- Kibango cha kwanza kinaelezea ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ambapo chama hicho kiliahidi kuzalisha ajira milioni nane katika sekta ya umma na sekta binafsi.

- Kibango cha pili kinaelezea mkakati uliopo kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2021/22-2025/26 ambapo ajira milioni 12 zitakuwa zimezalishwa.

- Kibango cha tatu kinahusu ajira 40,000 zitakazotolewa na Serikali mwaka 2021/2022 ambapo idadi hiyo itaajiriwa katika sekta ya umma.

Tuondoe Hofu:
Kwa hiyo, hakuna mkanganyiko wowote kuhusu takwimu hizo kwa sababu kiongozi anaweza kuzungumzia mambo tofauti. Mfano anaweza kusema viwanda vinne vitazalisha ajira laki 6.

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama inapenda kuona vijana wengi wanaajiriwa katika sekta mbalimbali.
 
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama ...
Hii mnayoita serikali ya awamu ya sita bado haijakaa sawa na haileti maana, hii ni serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na rais wa 6, that's!.
 
Anafikiri bado ni msemaji wa Serikali?

Maisha yanaenda kasi sana?

Asubiri wenye Serikali wake watoe utafanuzi.
 
Unaweza fikiri tupo kwenye maigizo au comedy, lakini ndio ukweli tupo kwenye uhalisia wa jinsi Taifa linavyoendeshwa, kama kijiwe cha wavuta bangi full kudanganyana.
 
Uzushi huu hapa:
Wapinzani wamechukua na kuviunganisha vibango vinne vya mtandaoni (infographics) vinavyotengenezwa na Ayo TV vyenye taarifa ya idadi ya ajira zitakazotolewa na Serikali kwa nyakati tofauti huku vikionesha mkakanganyiko kuhusu jumla ya watu watakaoajiriwa na Serikali.

- Kibango cha kwanza kina picha ya Hayati Magufuli na maneno yanayosema: TUTATOA AJIRA MPYA MILIONI 8.

- Kibango cha pili kina picha ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na maneno yanayosema AJIRA MILIONI 12.

- Kibango cha tatu kina picha ya Rais Samia na maneno yanayosema: AJIRA MPYA ELFU 40.

- Kibango cha nne kina picha ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na maneno yanayosema AJIRA LAKI 5.

Lengo la wapinzani ni kuvunja imani waliyo nayo vijana (ambao ndio idadi kubwa) kwa Serikali yao ikiwa ni mkakati wa kujiongezea idadi ya kura ifikapo 2025.

Msigwa anena:
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa ufafanuzi kuhusu upotofu huo unaonezwa mitandaoni katika kipindi hiki ambapo Tanzania ina uhuru mkubwa wa kujieleza.

Ufafanuzi wake ni huu hapa:

- Kibango cha kwanza kinaelezea ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ambapo chama hicho kiliahidi kuzalisha ajira milioni nane katika sekta ya umma na sekta binafsi.

- Kibango cha pili kinaelezea mkakati uliopo kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2021/22-2025/26 ambapo ajira milioni 12 zitakuwa zimezalishwa.

- Kibango cha tatu kinahusu ajira 40,000 zitakazotolewa na Serikali mwaka 2021/2022 ambapo idadi hiyo itaajiriwa katika sekta ya umma.

Tuondoe Hofu:
Kwa hiyo, hakuna mkanganyiko wowote kuhusu takwimu hizo kwa sababu kiongozi anaweza kuzungumzia mambo tofauti. Mfano anaweza kusema viwanda vinne vitazalisha ajira laki 6.

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama inapenda kuona vijana wengi wanaajiriwa katika sekta mbalimbali.
Hii serikali inawaona vijana wake ni viazi sana ee
 
Back
Top Bottom