Gerson Msigwa: Filamu ya Royal Tour hazikutumika fedha za Watanzania

Ngoja nijiinamiye kwa tafakari ya kina.Nitarudi
 
CAG atakagua hayo matumizi yake? Au sio za serikali? Nani aliratibu upokeaji wake? Ziliingilia kwenye akaunti ipi?
 
B
Swali langu lipo kwenye kichwa cha habari cha uzi wako Bakharesa, Mo Dewj, Dangote walichangia tshs. ngapi?? Kama matajiri ndio watu wanaoendesha serikali tujulisheni, kama Rais Samia alishinikizwa kuongoza twambieni, Ikiwezekana tuachane na hiki kinachoitwa royal tour tufocus kwenye economic development ya nchi yetu
 
Tumepigwa na kitu kizito sana chenye ncha kali kichwani...
Nadhani kwa kujua alivochemka kamuita Mwamba Mbowe amuweke sawa. Hoja zipi


waende nazo kwenye vikao vyao. Na taarifa zipo watoe kwa jamii. SSH anamuogopa Mbowe kuliko kawaida.
Katiba ilikuwa moto ikapoozwa kinamna. Sasa ROYO TUA imekuwa moto zaidi. Tunarudi pale pale kwenye Katiba.


Unganisha dots... theorise... analyse... conclude!
 
Royal tour ni filamu ya kutangaza vivutio mbali mbali vya kitalii vilivyomo inchini. Filamu ni biashara, sioni ubaya kama watanzania wenye uwezo wameweza kuchangia hii filamu. Je filamu hii ni kitu kizuri kwa nchi yetu - wengi wanafikiri itaongeza watalii wa ndani na nje. Sheria za ulipaji kodi zipo kwahiyo sioni tatizo kama hawa matajiri ambao pia ni raia wema wameamua kufanya kitu kizuri kwa nchi. Watanzania lazima tubadilike nchi nyingi zilizoendelea ni kawaida wafanya biashara au matajiri kuchangia kwenye jambo jema. Kama angesubiri pesa hiyo itoke kwenye mfuko wa serikali peke yake unadhani hiyo filamu ingekuwa imefanyika? Kila jambo lina pande mbili - chanya na hasi. Kwanini tunapenda kutazama pande hasi peke yake. Utalii Tanzania umedorora sana kutokana na UVIKO-19 ulikuwa unahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka, utalii ni asilimia 25 ya pato la taifa. Tuipe muda hii filamu ili tuone kama italeta mafanikio yanayotarajiwa. Hao matajiri wamewekeza kwenye filamu hiyo- lazima kuna faida ambayo itapatikana. Wananchi wengi wa Tz wamezoea na mara nyingi wanasubiri Serikali ifanye kila kitu- hata kuchimba mifereji ya kuongoza maji ya mvua kando ya nyumba zao.
 
Unasumbuliwa na umasikini. Tafuta pesa utakuja futa huu ujinga
 
Sukuma gang at work
 
Bila shaka kutakuwa na msamaha wa kodi wa muda mrefu, kwa hao matajiri waliojitolea kuchangia hii project ya mama yetu kipenzi.

Miaka 50-100 itapendeza, maana sasa hakuna namna.
Sukuma gang mnachekesha sana
 
Mawazo ya kimaskin na chuki zidi ya tajiri utazan umaskin wake wauleta tajiri
Taifa linarochukia utajiri na kuona umaskini fulsa
 
Tuwalaumu matajiri waliochangia Kwa maslahi
Tunawafahamu?Kataja Taasisi lundo na zingine za umma.Yale yale ya gawio la serikali kutoka kwa taasisi zisizopata faida bali zinaishi kwa ruzuku na mitaji hasi.
 
Kauli ya ajabu kabisa ati alikinga bakuli pesa ya Royal tour kachangiwa na wafanyabiashara ni aibu sana hii. Hata angejipa muda wa kufikiria namna ya kudanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…