Gerson Msigwa: Filamu ya Royal Tour hazikutumika fedha za Watanzania

Mlipo ambiwa andikeni katiba mpya, jengeni taasisi imara mlishupaza shingo mkijua boss wenu ataishi milele. Haya ni matokeo ya nchi kukosa taasisi imara zinazoweza kusimamia maslahi ya nchi na ukosefu wa katiba inayoweza kumuajibisha kiongozi yeyote anapo kwenda kinyume na miongozo iliyopo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Royal Tour ni jambo jema kabisa kwa maslahi mapana ya Taifa.
Bali matajiri walichangia almost karibu wote ni watu hatari sana na wanaotarajia malipo na tumeona tayari wamenza kujipenyeza ktk maeneo nyeti kwa maslahi binafsi
 
Mkuu endekea, mwaga yote naamini unawafahamu waliochangia na lazima wameanza kupata ahueni ya kodi.
 
Kwamba familia yetu IMEHONGWA!! Nan wa kusaidia kuibua HOJA hii bungeni, tupige kura ya maoni?
 
Hizo ni Kodi za wananchi. Hakuna cha mchango wala nini.

Matajiri karibu wote walikufa na Corona na wengine kufilisika.
Wapi Mafuruki, Gulam, HansPope n.k
Na wengine walifilisiwa na wengine kutekwa na Mwendazake
 
Kwa msomi wa uhasibu au kozi yeyote pale IFM wanaielewa hii maadili.ukicremisha kile kipengele kinasema zawadi isizidi nominal value.nominal valua ndio wanafunzi huwa hatuielewi.
Lakini 7bil ni nominal value kwa level yake.
Kwa level yangu ni Tshs 50,000.
 
Hata wakilipa kodi wewe itakusaidia nini? Pesa ngapi zinapotea mikononi mwa hao wakusanya kodi?

Acheni wivu
Halafu maendeleo yatakuwa kwa kutumia mitishamba ya ukoo wako? Waliozoe kuishi kwa kuroga ni shida sana
 
Umeandika vyema ila kumbuka wapo watu wanaona mwakani. So le us see. Ila nazidi kukumbusha hakuna tajiri anafanya jambo la hasara. Nilaxima tuirudishe in direct. Yes
 
Ndiyo maana masikini wanabaki kuwa masikini, fikra za kimasikini hazitukomboi
 
Kuna orodha nimeiona mahali kwa CHAWA mmoja ikidaiwa ndiyo ya wachangiaji.

Pamoja na Rais mwenyewe kusema kachangiwa na taasis pamoja na watu binafsi ile list imetaja taasis tu tena bila kiasi walichotoa.

Kuna ubabaishaji mwingi mno kwenye hili.
 
Nadhani ipo haja ya kuyaweka haya mambo bayana.

1. Waliochangia tuwatambue ni kina nani
2. Wamechangia kiasi gani kila mmoja
3. Utaratibu wa kuchangia ulikuwaje? Walifuatwa na kuombwa? Nani aliwafuata? Kwa utaratibu upi? Kwa nini wao? n.k.

Kama hakuna makandokando hakuna sababu ya kufichaficha mambo haya. Hii ni nchi yetu wote!
 
Kama tunakatiba inayompa rais afanye atakalo sasa mnalalamika nini.

Kipindi cha mzee Magu ilikuwa hivi hivi anagawa hovyo hela.

Anaamua analoona linafaa hata kama ni kinyume na sheria za nchi ama ustaarabu wetu.

Tuache kulaumu mtu,tupambane tuwe na katiba ifaayo dhidi ya yeyote yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…