GE2025 Gerson Msigwa: Goli la Mama liko Pale Pale – Goli 1 Vilabu shiriki kupewa 5M, Robo 10M, Nusu fainali 20M

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa Amezitakia kheri klabu za Tanzania Simba, Yanga pamoja na Singida Black Stars ambazo hii leo zinashiriki katika mashindano ya kimataifa barani Afrika ngazi ya klabu bingwa na shirikisho.

Msigwa akiwasilisha Salamu za heri kwa niaba ya serikali amesema kuwa goli la mama liko pale pale na Rais Ameamua kuwa zawadi hiyo ya Goli la mama ianze kutolewa katika hatua za awali kabisa ambapo kila goli la ushindi ni shilingi milioni tano hivyo kila klabu itakayoshinda itapokea kadiri ya magoli itakayoshinda ambapo hatua ya robi fainali Goli la mama litakuwa milioni 10 na hatua ya nusu fainali goli la mama litakuwa milioni 20 na fainali itaandaliwa zawadi maalum huku ushindi wa matuta utahesabiwa kama goli moja.

“Ninatambuwa kuwa Yanga leo itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Wiliete nchini Angola, mechi zinazofuata ni Simba watakaocheza dhidi ya Gaborone ya Botswana, Azam watakuwa nchini sudan wakicheza dhidi ya El-Merriekh na Singida black stars watakuwa nchini rwanda wakicheza na Rayon Sports tunawatakia kila la kheri na goli la mama liko pale pele tena kwanzia hatua hizi za awali” amesema Gerson Msigwa.

Soma zaidi hapa
 
Duuuh..!! Jamaa wanaendeleza kufuja kodi za watanzania hili kujipendekeza kwa wanainchi baada ya kuona hawakubaliki... wakati huo huku kibondo kwenye zahanati ya kata hakuna gloves na pakiti moja ni 6,000/= tu.

Kweli hawa watu wanastahili kuondoka hata kwa nguvu.
 
Naona kodi za wananchi zinaendelea kutumika vizuri haswa!. Nimejaribu kupiga hesabu kama timu ikipata ushindi wa goli 5 mechi moja ni milioni 25 kama akifanikiwa kufika hiyo nusu si mipesa itatoka ya kutosha
====================

“Ninatambuwa kuwa Yanga leo itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Wiliete nchini Angola, mechi zinazofuata ni Simba watakaocheza dhidi ya Gaborone ya Botswana, Azam watakuwa nchini sudan wakicheza dhidi ya El-Merriekh na Singida black stars watakuwa nchini rwanda wakicheza na Rayon Sports tunawatakia kila la kheri na goli la mama liko pale pele tena kwanzia hatua hizi za awali” amesema Gerson Msigwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa Amezitakia kheri klabu za Tanzania Simba, Yanga pamoja na Singida Black Stars ambazo hii leo zinashiriki katika mashindano ya kimataifa barani Afrika ngazi ya klabu bingwa na shirikisho.

Msigwa akiwasilisha Salamu za heri kwa niaba ya serikali amesema kuwa goli la mama liko pale pale na Rais Ameamua kuwa zawadi hiyo ya Goli la mama ianze kutolewa katika hatua za awali kabisa ambapo kila goli la ushindi ni shilingi milioni tano hivyo kila klabu itakayoshinda itapokea kadiri ya magoli itakayoshinda ambapo hatua ya robi fainali Goli la mama litakuwa milioni 10 na hatua ya nusu fainali goli la mama litakuwa milioni 20 na fainali itaandaliwa zawadi maalum huku ushindi wa matuta utahesabiwa kama goli moja.

“Ninatambuwa kuwa Yanga leo itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Wiliete nchini Angola, mechi zinazofuata ni Simba watakaocheza dhidi ya Gaborone ya Botswana, Azam watakuwa nchini sudan wakicheza dhidi ya El-Merriekh na Singida black stars watakuwa nchini rwanda wakicheza na Rayon Sports tunawatakia kila la kheri na goli la mama liko pale pele tena kwanzia hatua hizi za awali” amesema Gerson Msigwa.

Soma zaidi hapa
Madawati hakuna shule ya msingi turiani ,mvomero Morogoro.
 
GOLI LA MAMA KUANZA HATUA YA AWALI
“Goli moja katika mechi ya ushindi itakuwa shilingi milioni tano”
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Rais Samia atatoa kitita cha shilingi milioni tano kwa kila goli litakalofungwa kwenye mechi ya ushindi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kwa klabu za Tanzania.

Msigwa amesema katika hatua ya robo fainali, goli la mama ni shilingi milioni 10 na kwenye hatua ya nusu fainali goli la mama ni shilingi 20.

Katibu Mkuu huyo amesema kwenye mchezo wa fainali wataandaa zawadi kubwa zaidi.

Yanga wapo Luanda nchini Angola kucheza dhidi Wiliete Sports Clube
Simba ipo Francistown Botswana kucheza dhidi ya Gaborone Unite
Azam FC ipo Juba Sudan Kusini kucheza Al Merriekh Bentiu
Singida BS wapo Kigali Rwanda kucheza dhidi ya Rayon Sports

(Imeandikwa na @allymufti_tz)
 
Duuuh..!! Jamaa wanaendeleza kufuja kodi za watanzania hili kujipendekeza kwa wanainchi baada ya kuona hawakubaliki... wakati huo huku kibondo kwenye zahanati ya kata hakuna gloves na pakiti moja ni 6,000/= tu.

Kweli hawa watu wanastahili kuondoka hata kwa nguvu.
Hilo hawana habari nalo mdau, wao na familia zao hawatibiwi huko!
Hawana shida ya maji, umeme, chakula, usafiri, kusomesha watoto, wao ni raha, kusaza, ku enjoy!
Sasa unakaa foleni jua kali kuwarudisha madarakani?!
Tujitambuwe WADANGANYIKA!
 
Yanga tumshejihakikishia 15m, sasa kazi ni kwa wadogo zetu wanaotufuatia. SIMA, AZAM, SINGIDA
 
SIMBU kwenye Marathon huko Tokyo Katuletea Medali ya Dhahabu( kaweka historia) ambayo haikuwahi kuwepo.

Sekunde za mwisho kajitosa kabisa kwa uwezo wote hadi kupata nafasi hiyo kwa kiwango ambacho imeingia kwenye rekodi za dunia( naamini haitakaa itokee kufunjwa hii kushinda marathon kwa ufinyu wa muda wa 0.03sekunde)

Ila nimeona kapewa tuu hongera peke yake( hi ni dharau ki ukweli)

Kwa alichokifanya ni kikubwa nilitamani hata angepewa hata zaidi ya 200m kuzidi ile atakayo pata kwenye kushika natasi ya kweli
 
Hilo hawana habari nalo mdau, wao na familia zao hawatibiwi huko!
Hawana shida ya maji, umeme, chakula, usafiri, kusomesha watoto, wao ni raha, kusaza, ku enjoy!
Sasa unakaa foleni jua kali kuwarudisha madarakani?!
Tujitambuwe WADANGANYIKA!
Mishaara yao unakuta ina range 900k mpaka 7m ila wanasomesha watoto wao shule za ada 40m, wanamiliki magari ya kutembelea yenye thamani ya 120m+ bado wakiugua wanaenda kutibiwa Agakhan... na wakizidiwa sana wanaenda India tena kwa gharama za serikali

Aisee kwa style hii kamwe hawawezi kuwakumbuka wanyonge... wanyonge watawakumbuka kwenye kampeni.

Ila hawa jamaa tukiwaacha mwaka huu ndio wataendelea kutudharau sana na watakuwa wanaiba na kuteka watu adharani bila kificho.
 
Back
Top Bottom