Pre GE2025 Gerson Msigwa: Hali ya upatikanaji wa umeme nchini imeimarika na kufikia 78.4%

Pre GE2025 Gerson Msigwa: Hali ya upatikanaji wa umeme nchini imeimarika na kufikia 78.4%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeifanya Tanzania kuwa kinara barani Afrika katika uzalishaji na usambazaji wa umeme.

Akizungumza na wanahabari katika Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) mkoani Pwani siku ya Jumapili Februari 16, 2025, Msigwa amesema kuwa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati uliofanyika Januari 27-28, 2025 jijini Dar es Salaam, ni uthibitisho wa mafanikio ya Tanzania katika sekta hiyo.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwa mujibu wa Msigwa, hali ya upatikanaji wa umeme nchini imeimarika na kufikia 78.4%, huku serikali ikipanga kuhakikisha asilimia 100 ya Watanzania wanapata huduma hiyo ifikapo mwaka 2030.

Aidha amesema kuwa idadi ya wateja waliounganishwa na umeme imefikia milioni 5.2, huku serikali ikitarajia kufikisha umeme kwa wateja milioni 13.5 ndani ya miaka mitano ijayo.

Amebainisha kuwa Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) umeanza kuzalisha umeme, hatua ambayo imesaidia kuimarisha huduma za umeme nchini. Kwa sasa, mitambo iliyounganishwa kwenye Gridi ya Taifa ina uwezo wa kuzalisha MW 3,796.71, huku kiwango cha juu cha matumizi kilichorekodiwa hadi sasa kikiwa ni MW 1,900.62 mnamo Februari 14, 2025; ongezeko la MW 124.22 kutoka MW 1,776.4 za Novemba 2024.

Msigwa amebainisha kuwa ifikapo mwisho wa mwaka 2025, uwezo wa kuzalisha umeme utaongezeka hadi MW 4,081.71, kutokana na kukamilika kwa mashine ya mwisho ya JNHPP na ongezeko la MW 50 kutoka mradi wa umeme wa jua wa Kishapu.

Aidha, Tanzania inalenga kufikisha MW 7,992.5 ifikapo mwaka 2030, hatua ambayo itaifanya nchi kuwa na nishati ya kutosha kwa matumizi ya viwanda, biashara na wananchi kwa ujumla.

Serikali inaendelea kuwekeza katika miradi mipya ya umeme ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma hiyo kwa uhakika na kwa gharama nafuu.
Screenshot 2025-02-16 204631.png
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeifanya Tanzania kuwa kinara barani Afrika katika uzalishaji na usambazaji wa umeme.
Huku ni kujitoa akili. Afrika Kusini inazalisha umeme wa kuweza kugawa nchi zote za Africa ikiwa wao hawatautumia
 
Huku ni kujitoa akili. Afrika Kusini inazalisha umeme wa kuweza kugawa nchi zote za Africa ikiwa wao hawatautumia
Nimesoma yote sijaona sehemu aliosema Tanzania inaongoza kwa uzalishaji umeme Africa.
 
Back
Top Bottom