Gerson Msigwa kaondoka Ikulu nafasi ipo wazi, Pascal Mayalla ana nafasi ya kulamba uteuzi

Gerson Msigwa kaondoka Ikulu nafasi ipo wazi, Pascal Mayalla ana nafasi ya kulamba uteuzi

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

Msemaji/Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Mheshimiwa Gerson Msigwa hatimae kaondoka Ikulu.

Mheshimiwa Msigwa kapelekwa Idara ya Maelezo kama Mkurugenzi na Msemaji Mkuu wa Serekali. Sijui kama ndio kupanda cheo huko au kushuka,muhimu kaondoka Ikulu.

Mwanajamvi mwenzetu Pascal Mayalla ana sifa zote za kuongoza Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.Ifahamike ndugu yetu kwa muda mrefu amekuwa ni mtu wa bahati mbaya kila nafasi ikijitokeza anasahaulika sijui kalogwa na nani,hata msukuma mwenzake hakumuona.

Wanajamvi wote wasiokuwa na husda na roho ya korosho tumweke katika maombi mwetu hasa kipindi hiki cha Pasaka akumbukwe katika uteuzi wa nafasi ambayo ipo wazi.

Iwapo Mayalla au njaa atateuliwa hakutakuwa na malalamiko ya ukabila wala udini.

Ngongo safarini Chake Chake,Pemba.
 
Mayalla maana yake Njaa.Jina tu limkoseshe mtu kazi !.Tuangalie utendaji,weledi na ujuzi nadhani Mayalla anakidhi vigezo vyote tumwombe.

Mwanakondoo ameshinda tumfuate.
Hafai hata kidogo
 
Kwani yeye Pascal amesema anahitaji kuteuliwa? kama kasema hivo basi tumuombee ila kama sio acha kujipendekeza
 
Hii nafasi atailamba Maria Tsehai,Wamuweke yule Mwanaharakati ili achangamshe Ikulu kidogo.Maana kulikuwa kumepoa sana
 
Back
Top Bottom