McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Serikali imeboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi katika maeneo ya vijijini na mijini
Amesema kuwa bajeti ya Wizara ya Maji imeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 680 kwa mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.12 kwa mwaka huu. Ongezeko hili linaonyesha dhamira ya dhati ya serikali katika kuhakikisha huduma ya maji inaimarika nchi nzima.
Msigwa ameongeza kuwa, fedha hizo zinaelekezwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ili kuwapatia wananchi huduma bora. Matokeo ya uwekezaji huo yameanza kuonekana, ambapo upatikanaji wa maji umefikia asilimia 85.5 kwa maeneo ya vijijini na asilimia 95.2 kwa maeneo ya mijini