ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Msemaji wa Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia fedha za ndani licha ya kuibuka kwa matamko kadhaa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo wa Tanzania ya kusitisha misaada ya kifedha kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Msigwa ameyasema hayo leo Novemba 23, 2025 wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu mikakati ya serikali katika utekelezaji wa miradi kwa fedha za ndani, ambapo amesema serikali itaendelea kufanya mazungunzo na wadau hao ili kueleweshana baadhi ya mambo ambayo huwenda hawajayasikia kutoka upande wa serikali kuhusu tuhuma hizo.