Gerson Msigwa: Puuzeni, Serikali hatuna mpango wa kununua vichwa vya treni vya Dizeli

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amekanusha taarifa za kwamba Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapanga kununua injini zinazotumia umeme na diseli ili kuisaidia treni ya SGR umeme unapokatika safari zisikwame.

Pia, Soma: Tanzania kununua injini za disel kuendesha SGR

Akiongea usiku huu, Msigwa amesema "Zipo taarifa kwamba Shirika la Reli (TRC) linapanga kununua injini za dizeli kwa ajili ya kuendesha treni kwenye SGR naomba Watanzania tupuuze hizi taarifa hakuna mpango huo, SGR yetu inaendeshwa kwa umeme tuna treni za kisasa kabisa, changamoto ndogondogo zajitokeza lakini haina maana kwamba tumeshindwa mradi huu wa kimkakati"
Your browser is not able to display this video.
 
Msigwa wadanganye Wajinga
 
Miradi mkubwa na mzuri wa kimkakati unakatika kati kati ya safari.....Mbona sound zimekuwa tele kama pishi la mchele?
 
#VIDEO “Zipo taarifa kwamba Shirika la Reli (TRC) linapanga kununua injini za dizeli kwa ajili ya kuendesha treni kwenye SGR, naomba Watanzania tupuuze hizi taarifa hakuna mpango huo, SGR yetu inaendeshwa kwa umeme tuna treni za kisasa kabisa, changamoto ndogondogo zajitokeza lakini haina maana kwamba tumeshindwa mradi huu wa kimkakati” —Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali.
 
Keupe kekundu! Ndo mana wamemrudisha huyu jamaa kwa hii kazi
 
Kadogosa (CEO wa reli) alisema kuwa wana mpango wa kutumia injini za mafuta ya dizeli kama sehemu ya kukabiliana na risk ya umeme kukatika.

So hii si habari iliyotoka out of nowhere tu.
Anakanusha Ili kufanya watu wajinga Kwa sababu jambo Hilo limekabiliana na Upinzani wa Umma na mshangao.

Ila Kwa mujibu wa kadogosa wameagiza
 
Nunueni tyu mkiona navyo avifai tafuteni na betri mvifungie tyu.
 
 
Basi Masanja Kadogosa afukuzwe kazi kama anatoa taarifa ambazo hazijulikani hata na serikali.
 
Huyu kwa moyo wa dhati kabisa; kama ningekuwa na uwezo (sina), ningeunyofoa Ukatibu mkuu na kumrudishia Ukurugenzi wake na kisha kumfanya msemaji mkuu.
Anyway namuombea kheri hiyo.
 
Kwani iyo taarifa alitoa nani hadi apuuzwe,kwamba haijatoka serikalini au
 
Majaliwa....JPM yupo poa kabisa kabisa....
DP WORLD.....Hatujasaini mkataba...
Ndege kushikiliwa nje....Zipo matenenezo....
Utekaji.....Mwenye ushahidi alete.....

Nk nk nk nk nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…