Gerson Msigwa: Puuzeni, Serikali hatuna mpango wa kununua vichwa vya treni vya Dizeli

Gerson Msigwa: Puuzeni, Serikali hatuna mpango wa kununua vichwa vya treni vya Dizeli

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amekanusha taarifa za kwamba Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapanga kununua injini zinazotumia umeme na diseli ili kuisaidia treni ya SGR umeme unapokatika safari zisikwame.

Pia, Soma: Tanzania kununua injini za disel kuendesha SGR

Akiongea usiku huu, Msigwa amesema "Zipo taarifa kwamba Shirika la Reli (TRC) linapanga kununua injini za dizeli kwa ajili ya kuendesha treni kwenye SGR naomba Watanzania tupuuze hizi taarifa hakuna mpango huo, SGR yetu inaendeshwa kwa umeme tuna treni za kisasa kabisa, changamoto ndogondogo zajitokeza lakini haina maana kwamba tumeshindwa mradi huu wa kimkakati"
View attachment 3176168
Wangenunua za kutumia solar-power tu.Ndoho shida.
 
Huyu anavyoongea tu hata kama hujui Kiswahili kama umesoma Cuba unajua hapa tumepigwa.

Washaona watanzania ni embeciles wanawageuza kama chapati tu! Sasa anamkosoa CEO wa TRC? Na kwa akiki yake anaamini ataaminika tu
 
Je kuna mwenye video M.Kadogosa alivyokuwa anaongea tupate burudani kidogo huku tukiwa tunapuuza taarifa?
 
Back
Top Bottom