DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mahojiano ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alipozungumza na Kituo cha UTV, leo Jumatatu Oktoba 13, 2025.
Kuhusu Polepole nini kauli ya Serikali
Jeshi la Polisi limeshatangaza kutaka aende akatoe maelezo juu ya kauli alizokuwa akichapisha, zilikuwa kauli nzito, hakufanya hivyo, baadaye ikatolewa taarifa kuwa amepotea, amechukuliwa.
Kusema ametekewa inatakiwa ithibitishwe kwa kuwa lazima kuwe na ushahidi, Jeshi la Polisi limesema linafuatilia kuhusu hoja hiyo, linafanya uchunguzi.
Yapo matukio mengine ambayo yalitangazwa fulani kapotea baadaye ikagundulika kuwa hajapotea bali amejihifadhi sehemu, ni vema Watanzania wakasikiliza vyombo vyetu vya Usalama, ni vizuri kujiridisha.
Serikali haijui alipo Polepole, Polisi imeshatangaza kuwa inafuatilia. Jeshi la Polisi ni chombo cha Serikali siyo lazima niseme mimi.
Mtu akipotea ni jukumu la Polisi kufuatilia na kufanya uchunguzi.
Kwa nini Serikali haijaonesha kulinda raia wake kwa kumlinda Polepole?
Tukisikia fulani hayupo ni kazi ya Polisi kulinda na kuhakikisha usalama wa kila raia.
Taarifa za kutoweka kwa watu hazikuanza leo lakini kipindi hiki cha uchaguzi imekuwa gumzo.
Kutekwa ni kuchukuliwa kwa makusudi na inatakiwa kuthibitishwa, ni tofauti na kuondoka mwenyewe sehemu. Anayekuwa na taarifa anatakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika, ndio maana Jeshi la Polisi limetangaza kufanya uchunguzi na yeyote mwenye taarifa awasilishe zisadie uchunguzi.
Mtu akipotea anatafutwa, akipatikana umma utajulishwa amepatikana, kama hatapatikana Vyombo vya Usalama vitaendelea kufanya uchunguzi.