GE2025 Gerson Msigwa: Serikali haijui alipo Humphrey Polepole, ndio maana Polisi inafanya uchunguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ndugu zangu Watanzania,

Hilo ni swali lililoulizwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Gerson Msigwa.

Kwa Hiyo wewe kama una Majibu ya Swali hilo unaweza kujibu hapa Jukwaani ili kulisaidia Jeshi letu la Polisi na vyombo vingine vya kiuchunguzi juu ya jambo hilo.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Captain Tesha, unamsikia huyu mtu
 
Hivi Serikali ikifikia inajibu maswali namna hii kweli ni chi hiyoooo? Tumeliwa.
Yaani sasa hivi CCM ni Genge la wahuni.
Yaani FBI wajibu kwa Democrats kama hivi sijui itakuwaje. This is about National Security
Kaka ndio ujue kwamba hili taifa tayari limeshakuwa banana republic, yaan taifa la ovyo lenye viongozi wa ovyo ambao wamevimbiwa nguvu ya madaraka kiasi kwamba wanaweza kumfanya chochote mtu yoyote bila kuhofia chochote.

Yaani hawajui hata kuudanganya uma, wanatoa majibu mepesi kwa suala zito namna hii, ovyo sana hawa.

Ngoja tu wazidi kuichafua image ya tanzagiza kwenye ulimwengu wa kimataifa, tuone hiyo misaada wanayoitegemea kufanya ufisadi wao kama wataipata tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…