Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali tayari imeshanunua treni 10 za mchongoko ambapo treni 8 zimeshawasili na kati ya hizo 8, treni moja siku ya Jumamosi Januari 25, 2025 inakamilisha majaribio yake kutoka Morogoro kuelekea Dodoma ili ianze kutoa huduma rasmi
Msigwa ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akizungumza na wanahabari kabla ya kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na wanahabari hao ambapo Januari 25, 2025 atakuwa na mkutano wa kuelezea miradi mbalimbali ya kimkakati ya serikali.
Msigwa amesema kuwa hapo awali watu wengi waliongelea vibaya mradi huo wa Treni za SGR, kuwa Serikali imenunua treni zilizopitwa na wakati ambazo sio ‘mchongoko’ hata hivyo wao pia ni mashahidi wa treni zilizopo hivi sasa.