Gerson Msigwa tumia taaluma yako kukwepa kuonekana unafanya kazi za Jaffar Haniu

Gerson Msigwa tumia taaluma yako kukwepa kuonekana unafanya kazi za Jaffar Haniu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais( Ikulu) ni nafasi mbili tofauti zenye majukumu tofauti.

Lakini kwa uteuzi wa Gerson Msigwa na Jaffari Haniu itakuwa vigumu sana kutenganisha majukumu haya na kuleta picha kwamba Gerson anamfunika Jaffari au anaingilia kazi zake.

Kwanini nimeona hivi; majukumu haya kwa sasa nivigumu kuyatenganisha na social media. Kila barua au maelekezo lazima yapite kwenye mitandao ndipo yawafikie walengwa.

Jaffar Haniu bado jina lake ni geni mitandaoni, Gerson Msigwa Ni mpana sana mitandaoni. Lakini pia utawala huu siyo utawala wakujimwambafai kwamba kila alipo kiongozi wa Nchi basi Mkurugenzi lazima asimame aseme na hata akiwa anasema bado mwangwi hautakuwa mkubwa Kama awali.

Kwa mazingira haya na ili kutenganisha majukumu haya kwenye mitandao ambayo ni chanzo kikuu Cha habari nimshauri mdogo wangu asiwe mwingi sana kuhabarisha ya ikulu. Amwache Jafari afanye kazi hiyo na kuzifanya account za Jaffari kuwa source ya taarifa za Ikulu.

Page za Msigwa zikiendelea kuwa source ya taarifa za Ikulu italeta picha Kama Hawa wawili ni wamoja na kwamba mmoja anaweza kufanya yote mawili.

Ntatoa mfano; ukiangalia utenguzi na uteuzi wa Jana utaona page ya Msigwa na Jaffari zilipost same barua ila mmoja aliweka nakshi na waliozoea page ya Msigwa awakukimbilia kwa Jaffari Tena.

Ni mambo madogomadogo ila tukiyasema yanaleta mtengano wa kimajukumu, na tusiposema sisi huku mitandaoni may be wanaohusika awataweza kulisemea.

Niwatakie kazi njema wadogo zangu
 
Source ya habari mi upuuzi mtupu.

Malisa ni mlamba viatu wa Mbowe
 
Page za Msigwa zikiendelea kuwa source ya taarifa za Ikulu italeta picha Kama Hawa wawili ni wamoja na kwamba mmoja anaweza kufanya yote mawili
Hata mimi nashindwa kuwatofautisha naona kama ni wabia
 
Ila pale ikulu palimpendeza sana mwamba wa Songea! Nahisi hata yeye anavutiwa na nafasi yake ya awali kuliko hii ya sasa! Ningekuwa nina mamlaka msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais angekuwa mtu mmoja!
 
Haniu apambane kujijenga asitegemee msigwa kumsaidia.

Nafasi hizo mbili kuna sehemu nyingi zinafanana majukumu.

Mwambieni basi Mama yenu amfukuze kabisa kazi Msigwa atawasikiliza
 
Source ya habari mi upuuzi mtupu.

Malisa ni mlamba viatu wa Mbowe
Uzinzi na umalaya ni kipaji kama ilivo kucheza mpira au basket ball na inaonekana mapema kama vipaji vingine tu toka udogoni ndio maana mkiambiwa mchague wa kuzaa naye mnakuwa na jazba na hasira,serikali hawezi kuingilia vipaji vya watu its in human nature.

WHERE THERE IS A WHEEL, THERE IS A WAY!!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais( Ikulu) ni nafasi mbili tofauti zenye majukumu tofauti..
Majukumu yapo tofauti sana tena kubwa tu, tatizo wengi walizoea wakati wa Magufuli alikuwa anamtumia msemaji wa ikulu kama ndio msemaji wa serikali kiujumla.

Kiufupi Mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ndio msemaji wa Ikulu na hutoa taarifa za ofisi ya rais na mambo ya ikulu pekee. Ila Mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano ya Serikali yeye anaongelea Mambo ya wizara zote pamoja na utendaji wa serikali kiujumla.

Kimsingi wote ni wakurugenzi tu sema mmoja yupo ikulu na mwingine yupo chini ya wizara ya habari lakini kivyeo wapo sawa but kimaslahi inaweza kuonekana kama huyu wa Ikulu ni boss zaidi Ila majukumu yao tofauti.
 
Sijui hata umesoma uzi, muda wote unamuwaza Mbowe tu.
Mkuu hao ni wa kuonea huruma tu, kwani washbrain ya mwendazake aliyowapiga itachukua miaka mingi sana , kuisha, ili ndio akili zao zianze kujirudi?!!"Ndio maana unashangaa jitu linaongea hata halieleweki,
 
Ila pale ikulu palimpendeza sana mwamba wa Songea! Nahisi hata yeye anavutiwa na nafasi yake ya awali kuliko hii ya sasa! Ningekuwa nina mamlaka msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais angekuwa mtu mmoja!

Wewe kama sio Msigwa mwenyewe utakuwa ndugu yake Msigwa!! Msigwa aliishaambiwa humu JF Kuwa it was just a matter of time before someone else was appointed to that position!! Alionekana kupenda title zote mbili though.!
 
Kiukweli naona hii nafasi n kama moja hivi. Yaan sion ulazima wa kuwa na watu wawili tofauti.
Ila pale ikulu palimpendeza sana mwamba wa Songea! Nahisi hata yeye anavutiwa na nafasi yake ya awali kuliko hii ya sasa! Ningekuwa nina mamlaka msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais angekuwa mtu mmoja!
 
Back
Top Bottom