Kutoa ufafanuzi wa jambo ambalo ni jukumu la serikali inayoendeshwa kwa kodi za wananchi sio kwasababu hao wananchi kuna jambo wanaweza kumfanya rais.ila unatakiwa tu ujue kua wananchi ndio waajiri wa huyo rais na wakiamua kumkwamisha wanaweza.
UFAFANUZI.
Tsh. Bil. 4 za Sherehe za Uhuru zilizotumika kujenga barabara ya Morroco-Mwenge (2016) zilifanya upanuzi wa barabara za njia 2 zilizopo katikati ya barabara na Tsh. Bil. 71.8 za msaada wa Japan zimetumika kujenga barabara za njia 4 zilizozinduliwa na Mhe. Rais Samia.