Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Suzy, angalau tarehe ya bandiko hili Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!
Humo nilisema
Chuma alibadili sheria na kuleta sheria mpya ya madini, sasa kila kinachochimbwa kwenye ardhi ya Tanzania, 16% ya net profit ni mali ya Watanzania kupitia free carried shares.
Hivyo sasa gesi ni yetu!.
P
 
Wooote mlio changia hapa ni Mamburula tupu!!!...kwa sababu hata Gas ikiachwa hapo miaka Million mbili hakuna mwenye akili za kuchimba hiyo Gas!! Mlikuwa wapi kabla ya wao kuja kuchimba???

Ok! mnaweza kuchimba mna vifaa!! haya mtaifanyia nini baada ya kuipata? mfano mkonge mlichukua mbona mashamba yameoza mnalishia mifugo tu bila aibu? mpaka sasa!.. Mara milk! iko wapi?

MUTEX,Mwatex. kiwanda cha nyuzi Tabora kunako limwa pamba kwenu huko viko wapi!......tena ulikosomea babaako akiwa afisa usalama

Anzia hukooo kwenu kanda ya ziwa! ulikokulia na kuyaona tangu ukiwa kinda mali za Umma zikiporwa mchana kweupeee usipafumbie macho! kwakuwa ni ndg zako kuna mapungufu meeengi...unarukia huku heee!

OK! km haitoshi jimbo lako weye paskal ulilowahi gombea lina kiwanda cha nyama za kopo leo ni mfu leo! hiyo gas ingetumika hukoo! lkn huna akili za kuvifufua umekalia uchochezi tuu!

kalamu ikitumika vibaya ni sumu kali sana itakayo kukula weye na wanao wooote! halafu ina tabia kwamba hatari yake inaanzaga na weye uliyeshika kiberiti!...kama Stan katabaro!! unamjua alipo?

Niliwahi kusema watanzaia sasa tumeamua ni mkuki gani utuchome! mkanishangilia sana! Paskali ulikuwa mmoja wao! acha undumila kuwili!....nimechukia sana!
 
Mkuu uko sas hiii wakt mwingine paskali ananikera anavyojifanya mwerevu kumbe Ni mweupe mnoo tu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tuache unafiki Magufuli muda mwingine akiwatukana wastaafu wenu wala msilalamike na huwezi kusikia wakijibu kitu maana wanajua madudu waliyomwachia mwenzao
Yule alikuwa Mgonjwa wa akili!!!...….Rais kichaa kuwahi tokea ulimwenguni kichaa chake kilimtuma asisalimie Marais wenzake!!……..hata kusafiri tu aliogopa kuanguka na ndege! kiinge hajui yaaani......

Akaanza kukamata panya hovyo!!mfano kukamata kale kakijana kakihindi na mibunduki lukuki kalikosa nini?? kumpiga Tundu lisu Risasi zooote zile Rais ana akili kweli??...yule tundu lisu nikumuita tu unamwambia acha hizo!
 
Mkuu Meneja Wa Makampuni,
asante sana kwa uzi huu elimishi
Ubarikiwe sana,
Karibu na pande hizi!.
P
 
Duh...!. Huu jameni sio uchochezi huu?.
Contents za mkataba bado hatujaambiwa!, wewe umeanza kulalamika tunaibiwa!. Mbona Waziri January Makamba hili ameliweka vizuri kabisa hapa , japo mkataba bado haijawekwa wazi, baadhi ya vionjo vya mkataba huo tumeisha anza kumegewa.
1. Mkataba huu utatumia sheria yetu mpya ya madini, hivyo Watanzania tutamiliki 16% shares ambazo zitamilimilikiwa na serikali kwa niaba ya Watanzania.
2. 10% ya gesi yote ya LNG, itatumika nchini!, this is huge amount of gas ni nyingi kuliko vigesi gesi vyote vinavyotumika nchini put together!.

Mwaka 2012, nilifunga safari hadi Bungeni Dodoma, nikamtafuta JJ. Mnyika na Zitto, nikawapa hii dossier iliyomo humu Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe! himo nilisema
That was then, he did nothing!, they did nothing!.
Baada ya Watanzania kulia sana kuhusu kuibiwa rasilimali zetu kwa kufanywa shamba la bibi, hatimaye Mungu akasikia kilio chetu, hapa kati akatupatia mtu sahihi, akapindua meza, akabadili sheria yetu ya madini, gesi asili ikaingizwa kwenye madini chini ya extractive industry, sasa kwa mujibu wa sheria yetu, kitu chochote kinachochimbwa kutoka ardhi ya Tanzania, 16% stake ni mali ya Watanzania, and to be honest, this is a lot!. Maadam JJ.Mnyika, haujui mkataba una nini, then asubiri aone mkataba una nini na sio kuufanya huu uchochezi anaenda kuufanya mikoa ya Kusini!.

P
 
Nimekumbuka kipindi hicho ukiitwa PASCO hakika ulikuwa unaleta vitu nyeti kwa maslahi mapana ya Taifa, ila ulivyogeuka na kuitwa Pascal Mayalla mada zako za hivi zimepotea au zimekuwa adimu.

Wale wasiojua kusoma na kuandika tena wanaishi vijijini hakika wanafurahia maisha, taarifa kama hizi hawazijui wala hawafuatilii vitu vya kuimiza vichwa vinavyogusa maisha ya wengi. Wao wakilishwa propaganda wanajua mambo yako hivyo.
 
Cha kushangaza wewe mayala mwandishi wa makala hii ambae unaexposure na haya maswala Kila siku upo bize kuipigia debe ccm humu. I don't get it. Sikuelewi kabisa we mzee.
Mkuu crankshaft , huwa tunasaidia saidia kushauri...
P
 
Hivi Pascal Mayalla hizi hoja huwa unafikisha kwa wahusika au zinaishia hapa, je kwa sasa sekta ya gesi unaionaje?
 
Hivi Pascal Mayalla hizi hoja huwa unafikisha kwa wahusika au zinaishia hapa,
Mkuu Dimeta, D Metakelfin , naamini uliisoma hii para ya mwisho
je kwa sasa sekta ya gesi unaionaje?
Yule kiongozi kichaa alikuja kuingia, ni JPM, tukapitisha sera ya gesi, tukapitisha sheria ya rasilimali za taifa, tukapitisha sheria mpya ya madini, sasa Tanzania inamiliki 16% free carried shares kwenye migodi yote!.

Wakati sheria hiyo inapitishwa niliuliza kitu Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?
Hapo niliuliza maswali manne
  1. Zita Act Retroactively?​

  2. Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?​

  3. Can we Stand?​

  4. Do we have the Guts?​

1. Mambo hayo yote manne yametokea
La kwanza mpaka sasa ni mgodi mmoja tuu umekubali kutekeleza sheria hii mpya, mgodi wa Barrick, migodi mingine yote wamegoma ama wana sua sua!. Ile mikataba yote tuliovunja, tumeshitakiwa nje ya nchi, tumeshindwa kesi zote!, tumelipishwa mabilioni!.
Wakati sheria hiyo mpya ipo, Tanzania tukaingia mkataba wa IGA ya DPW ni illegal contracts kwa mujibu wa sheria zetu!, baada ya kusaini IGA, wakataka kuibadili sheria ndipo tusaini HGA, lakini kilichofanyika ni Ile IGA batili ilitupwa uvunguni, tukasaini HGA safi, kimya kimya kwa siri!.
2. Hatukuvunja mikataba yote bali sheria mpya iko ignored! Sheria ya zamani ambayo haipo, imeisha futwa ndio inaendelea kutumika!.
3. Tumeshondwa ku stand, tunashitakiwa kila siku, tunashindwa kesi tunalipishwa mamilioni, tunalipa kwa siri!.
4. We don't have the guts!. Kilichomkuta Patrice Lumumba, Blood diamonds, Saddam Hussein, Muammar Quadafi, ndicho kilichomkuta JPM!. Nilitoa angalizo kabla US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali? tukashindwa kum protect... akaliwa kichwa!.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…