eucalyptos
JF-Expert Member
- Jan 23, 2010
- 391
- 139
Ndugu wanajamvi,
Kutokana na maongezi ambayo tumekuwa nayo juu ya gesi yetu ya asili, ninachikua fursa hii kutoa mawazo yangu juu ya uthamani na kazi za gesi hii vitakavyoleta maendeleo ya haraka.
Maoni yangu:-
1. Gesi hii inatakiwa itumike kwaajili ya kuzalishia umeme.
Hii itaokoa gharama za ununuzi wa mafuta yanayotumika kuzalishia umeme.
2. Tunatakiwa kutumia gesi kwa kuendesha magari kama wanavyofanya India. Huko india magari makubwa kwa madogo hata bajaji zinatumia gesi. Hii itaondoa gharama za uagizaji wa Petrol, Diezel na mafuta ya taa toka nje ambayo kwa mwaka 2010 zilikuwa zaidi ya shilingi TRILIONI TATU (3Tr)-Source Tanzania Oil - imports - Economy.
Matumizi ya gesi katika kuendesha magari hayachafui mazingira (hewa).
Katika matumizi ya taifa ya pesa za kigeni za ununuzi wa mafuta ndio unaoshikilia namba moja katika matumizi yote. Iwapo pesa hizi zitaokolewa zitawekwa kwenye matumizi ya maendeleo ya taifa. Pesa hizi ni nyingi sana, hatuhitaji kuuza nje ya nchi (export) gesi iliyosindikwa ili kupata pesa za maendeleo.
Tukumbuke kwamba nchi nyingi za Africa zinazouza mafuta nje, mapato yake hayajaweza kuleta maendeleo katika nchi hizo.
Kwahiyo mapendekezo yangu ni kuwa viwanda vinavyotaka kusindika gesi na kuuza nje, visimamishwe kwanza mpaka mahitaji ya ndani yametosheleza.
3. Gesi inatakiwa itumike kwa matumizi ya majumbani ili kuondoa gharama za kuagiza gesi(LPG) inaayotumika kwa sasa na kunusuru mazingira (kupunguza matumizi ya kuni na mkaa) pia kuokoa afya za wananchi.
Nawasilisha.