Gesi ilivyoung’arisha Mkoa wa Mtwara

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
"MTWARA ya sasa ni tofauti na ile ya miaka ya 2011 na kurudi nyuma, kwani ilikuwa ikidharauriwa na haikuwa ikifikika kwa urahisi kutokana na miundombinu mibovu hususan barabara."Ilikuwa si ajabu mtu kulala njiani kwa muda wa siku tatu hadi wiki nzima ndipo ufike Mtwara lakini kwa sasa unahesabu saa tano na nusu hadi sita unakuwa tayari umefika.

"Halafu ukifika Mtwara unajisikia fahari kuwa nimefika kwani kumekuwa kunavutia na kunapendeza ukilinganisha na hapo zamani.
"Sasa kuna maghorofa mengi, hoteli nzuri, lami kwenye barabara za ndani ya manispaa na hali ya kibiashara kwa sasa ni nzuri kiasi kwamba unaweza ukafanya biashara yoyote bila wasiwasi wa kutopata wateja.

Hayo si maneno yangu bali ni ya mwenyeji wangu Mohamed Namkopa, ayezungumza nami baada ya kuwasili katika mkoa huo ambao wenyeji wake wanajinasibu kuwa umepiga hatua kiuchumi na kimaendeleo kutokana na kugundulika kwa gesi asilia, mafuta na uwekezaji wa viwanda vya saruji unaofanywa na mwekezaji maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote.

Nami bila kusita naanza kwa kutaka kufahamu historia ya mkoa huo kwa undani hususan thamani ya ardhi kabla na baada ya ujio wa neema hiyo.Ikiwa ni takribani miaka mitatu imeshapita kutoka gesi ilipogunduliwa kwa mara ya kwanza mkoani Mtwara, hali imebadilika kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba ardhi imegeuka na kuwa lulu kwa kila anayeihitaji.Hali hiyo inatokana na wamiliki wa ardhi ambao wengi wao ni wenyeji wa mkoa huo kubaini kuwa kuna uhitaji mkubwa wa ardhi kutoka kwa watu wanaotoka nje ya mkoa ambao wanataka waitumie kwa uwekezaji.


Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini jambo hilo la kupanda kwa thamani ya ardhi ambayo kabla ya kugundulika kwa gesi ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi kidogo cha fedha ukilinganisha na baada ya ugunduzi huo.mKatika maeneo ya Kijiji cha Hiyari kilichopo takriban kilomita 20 kutoka katikati ya Manispaa ya Mtwara kilipo kiwanda cha saruji cha Dangote, ardhi kwa sasa inauzwa sh. milioni 2.5 kwa heka ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo ukubwa huo ulikuwa ikiuzwa kwa bei ya sh. 100,000 hadi 200,000.


"Kabla ya kampuni hii ya Dangote kuanza ujenzi wa kiwanda chao hapa Hiyari, ardhi ilikuwa ikiuzwa kwa bei ya chini sana ambayo ilikuwa ni sh.50,000 hadi 100,000 au ukibahatika inafika 150,000 kwa heka moja."Sasa inauzwa zaidi ya sh. milioni 2. hadi 3. Wananchi wameona kuwa ardhi kwa sasa ni ‘dili' kubwa sana na ndiyo maana wameipandisha bei," anasema Namkopa ambae baadaye nilikuja kubaini kuwa ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Hiyari.

Aidha, mwenyekiti huyo aliendelea kueleza kuwa ni vigumu sana kupata ardhi kwenye kijiji hicho kwani mara baada ya wajanja kuona ujenzi wa kiwanda hicho walikimbilia kijijini hapo kununua ardhi kabla ya wakazi wa Hiyari kushtuka lakini baada ya wao kufahamu umuhimu wa ardhi nao walianza kugoma kuwauzia kwa bei ya chini."Nakwambia ndugu yangu hapo wajanja walinunua ardhi kwa bei ya chini kabla ya wanakijiji kushtuka lakini baada ya kufahamu basi hali ikawa ni tofauti.

Wanataka wauze kwa bei wanayoitaka na ndiyo sababu ya kupanda hadi kufikia bei niliyoitaja hapo mwanzo, na kila siku inazidi kupanda thamani na usishangae ikapanda mpaka kufikia sh. milioni 10 au 20,"anasema. Hali ni tofauti kwenye vijiji vilivyopo kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi hususan vile vya Mgao, Namgogori na Kisiwa ambavyo ndivyo mwekezaji Alhaji Aliko Dangote anatarajia kujenga bandari ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa ukanda huo wa kusini kwani ardhi imekuwa ikiuzwa kati ya sh. milioni 8 mpaka 20 kwa ekari moja.

"Kuna Watanzania wenye asili ya Asia walikuja huku na kununua ardhi kubwa sana. Waliuziwa hekari moja kwa sh. milioni moja hadi mbili lakini kwa sasa bei hiyo imekufa na tumeizika zamani sana."Kwa sasa tunauza kati ya sh. milioni 8 hadi 20, inategemea na mtakavyoelewana na kitu unachotaka kuwekeza,"anasema mwanakijiji mmoja wa Mgao ambaye hakutaka kubainisha jina lake.

Gazeti hili lilipata shauku ya kufahamu undani wa kauli aliyoizungumza mkazi huyo wa Mgao hivyo liliamua kumtafuta Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abdurahman Shah na ambaye bila kusita anasema hali ndivyo ilivyo."Ulichoelezwa ndugu yangu ndicho hicho hicho. Kabla ya Alhaji Dangote kubainisha adhma yake ya kujenga bandari kijijini hapa, kuna wahindi (Watanzania wenye asili ya kiasia) waliuziwa ardhi kwa bei ya chini sana lakini kwa sasa bila milioni 8 hadi 20 hupati kitu,"anasema Shah.

Vivyo hivyo mwenyekiti huyo anabainisha kuwa kuna mkazi mmoja ambaye alimpatia Alhaji Dangote eneo la hekari mbili kwenye mwambao wa pwani ya kijiji hicho alifanikiwa kukiuza kipande kingine cha ardhi hekari nne kwa sh. milioni 60.
Katika kuthibitisha kuwa hali ya sasa ni tofauti na ilivyokuwa zamani, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mahamoud Kambona ambaye kabla ya kuwa DC wa wilaya hiyo, alikuwa ni Ofisa Tarafa wa Kata ya Mayanga, Wilaya ya Mtwara Vijijini anasema miaka ya 2010 hadi 2012 mwanzoni thamani ya ardhi ilikuwa ni ndogo ukilingana na sasa.

"Kabla ya kuja kwa mwekezaji huyu (Alhaji Dangote) thamani ya ardhi ilikuwa ndogo kupindukia, kipande cha hekari moja kilikuwa kinauzwa kuanzia sh.50,000 hadi 150,000, bado wanunuzi hawakuwepo.Ulikuwa ukiwa na shida ya kuuza ardhi inakupasa utafute mnunuzi hata kwa wiki mbili ama tatu lakini kwa sasa ukisema unauza ardhi dakika hiyo hiyo mnunuzi anafika,"anasema DC Kambona.

Aidha, DC huyo anaendelea kubainisha kuwa hali ya kiuchumi kwa mkoa huo ilikuwa mbaya na hususan vijiji vya Mgao, Namgogori, Kisiwa na Hiyari vilivyopo kwenye Wilaya ya Mtwara Vijijini ndiyo ilikuwa mbaya zaidi kutokana na wakazi wake kutokuwa na shughuli zozote za kuwaingizia kipato zaidi ya kilimo cha korosho ambacho nacho ni cha kusuasua na cha msimu.

"Hapo Hiyari hadi Mgao hapakuwa na shughuli zozote za kibiashara zaidi ya korosho tu. Wakazi wake walikuwa na maisha duni kwa kuwa uchumi wa mkoa ulivyokuwa mdogo lakini mara baada ya miradi ya Dangote kuwasili basi hali imebadilika na kuwa kama ulivyoiona. Biashara zipo hadi zile za fedha kupitia mitandao, uchumi umekua kwa kiasi kikubwa.

"Makazi mazuri pamoja na hoteli nzuri za hadhi ya juu zimejengwa mkoa mzima na hata kwenye vijiji hivyo kuna hoteli nzuri zinajengwa. Ni jambo la faraja kuona uchumi wa mkoa unapaa kwa kasi ya ajabu na si ajabu kuuona ukiwa kwenye safu ya mikoa yenye uchumi mkubwa nchini kutokana na kasi ya uwekezaji mkoani hapa,"anasema DC Kambona.Hali ya kupanda kwa thamani ya ardhi haipo kwenye Wilaya ya Mtwara Vijijini pekee bali hata kwenye Manispaa ya Mtwara Mikindani kwani hali ni hiyo hiyo. Bei ya viwanja iko juu tofauti na kabla ya ugunduzi wa gesi asilia mkoani humo.

Akida Zidikheri, mmiliki wa hoteli na nyumba za kulala wageni za Akida Appartments, anasema kabla ya ugunduzi wa gesi, bei za viwanja kwenye manispaa hiyo hazikuwa kubwa tofauti na ilivyo sasa.Mwandishi wa habari Mohamed Mwaya mkazi wa mkoa huo, akizungumzia jambo hilo anabainisha bila kusita kuwa hali ya maendeleo ni kubwa tofauti na zamani kabla ya ugunduzi huo na pia hata hadhi ya mkoa imepanda kwa kiasi kikubwa.

"Kipato cha mwananchi wa kawaida kwa sasa kimekua kwani hata bila ya kusubiri tafiti ziseme, unaweza ukaona kwa macho tu kwani wakazi wa mkoa huu sasa wanafanya biashara kwa wingi na zinatoka kwa kiasi cha kuridhisha. "Kwa upande wa maendeleo, miundombinu imeimarika na sehemu nyingi za mkoa kwa sasa zinafikika kwa urahisi zaidi tofauti na zamani. "Huduma za kijamii kama vile zile za afya, elimu, maji, benki na nishati zinapatikana kwa urahisi na kwa ukaribu zaidi kiasi kwamba unaweza ukafanya shughuli zako bila wasiwasi na hata ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa sasa unafanyika kwa urahisi kupitia maduka ya kubadilishia fedha na benki,"anasema Mwaya.

chanzo jambo leo
 
shikamoo GAS and kudos to watu wa kusini for their positive stance they showed in 2012-2013.shikirieni hapo hapo.:glasses-nerdy:
 
misaka mitano ijayo patakuwa hapashikiki,labda kama rais ajae ataharibu
 
Gesi ni msingi wa maendeleo ya nchi yetu,tuiunge mkono juhudi hizi za serikali zakutuletea maendeleo kwa kutumia rasilimali gesi
 
Sikuwahi kufikiri kuwa kuna siku mkoa dhalili utakuwa top ten ya kila kitu katika nchi hii. Kijografia, mtwara ni mkoa wa tatu kwa udogo wa eneo, ikiizidi Dar es Salaam na Kilimanjaro, lakini ni miongoni mwa densely populated katika ile tuiitayo Population density( uwiano wa watu na eneo mraba) hapa ikizidiwa saaaana na Dar es Salaam kwa sababu ambazo ziko obvious.

Kwa sasa kuna hotel za kufa mtu, achilia mbali lodges! Sema tu muanzisha uzi kachukua kutoka gazetini. Kama Sinzinga na THE BIG SHOW,wangetusaidia picha current kabisa za sasa hasa miundombinu mbalimbali watu wangekubali.

Ukienda kule Msimbati kuna nyumba za kisasa za wafanyakaz wa Kiwanda cha gesi, lakini eneo la Msijute( 18km kutoka Manispaa) kilikuwa ni kijiji tu, leo ujio wa Dangote ni mji kabisa unaojitegemea.

Tungepata picha za BNN Hotel, Msemo Hotel, NAF Beach Hotel, NAF View Hotel, Maisha Club, Makonde Royal Club, Copa Cabbana na maeneo kadhaa ya mjini pamoja na Hotel amabazo nmezisahau ingejustify maelezo yq uzi huu.

Kuna wakati ilitajwa kuwa kiwanja kilishawahi kuuzwa kwa Tsh 2bn/- eneo la Shangani West.

Kiuhalisia, mkoa unakua kwa kasi sana. Hapo zamani redio ilikuwa moja tu yaani RTD/TBC na Redio One wakati wa usiku kupitia AM! Kwa sasa kuna redio tatu za Mjini Mtwara( Pride FM, Info Radio, Safari Radio, PC FM hii ilioparate lakini ikafunga matangazo yake, lakini Radio Jamii - Community Radio ilianzishwa lakini haikurusha matangazo) na redio za miji mingine ni RFA, Clouds, Radio One,Magic FM, Capital Radio, TBC FM/ Taifa,Radio Maria, Uhuru FM na Radio Heri.
Pale Wilayani Newala wana kituo chao cha Redio na pia pale Masasi wana kituo chao cha TV! Mambo haya niliyoyasema siyo mageni kwa Watanzania, ila yamewekwa hapo kuonyesha mabadiliko ya huvi punde. Mengi ya vitu nilivyovitaja hapo ni kuanzia mwaka 2012 hadi sasa, yaan ndani ya miaka3 tu.

Hivyo ni kweli Mtwara kama mkoa uko poa sana kwa sasa, na kwa Manispaa ndo usiseme, mji uko poa sana na wageni ni wengi, kumbuka Dar imejengwa na Watanzania wote, basi naamini Mtwara itajengwa na Watanzania wote lakini wenyeji watatumia fursa ipasavyo, hongera Mtwara, viva Mtwara!
 
Hoja yako imekaa vizuri but ilitakiwa iende sehemu ya Uchumi na Biashara kuileta kwenye jukwaa la Katiba unaipunguzia nguvu, nakushauri uipeleke kule hapa achia Katiba!
 


Hoja yako imekaa vizuri but ilitakiwa iende sehemu ya Uchumi na Biashara kuileta kwenye jukwaa la Katiba unaipunguzia nguvu, nakushauri uipeleke kule hapa achia Katiba!
 
Maendeleo unayoyaona Mtwara ni maendeleo ya kawaida sanaa ambaya hayakuhitaji gesi tu ndio yafanyike, mimi binafsi kwa mtazamo wangu sijaona cha ajabu sana kama watu wanavyoongeza chumvi! Kwa kuanza na hizo hotel yaani hamna kitu kabisa sababu hata hiyo Naf Beach Hotel ni level za kariakoo tuu labda tusubiri hiyo itakayojengwa na jamaa wa Sea Cliff maana nasikia wamenunua eneo kule beach. Nyingi zilizojazana ni Lodges yaani nyumba za wageni za kawaida sana kwa mtu yeyote mwenye exposure ya maendeleo.
Tunapoangalia maendeleo usitazame kwenye burudani na starehe tu, angalia mambo ya mzingi kama shule na afya pia. Mfano Mtwara mbali ya yote uliyoyasifu mpaka sasa hakuna hospitali ya maana yenye uwezo wa kutoa vipimo vya kisasa! Hospitali inayotegemewa ni ya Mission ambayo iko zaidi ya Km 100 nje ya mji! Miundo mbinu kama barabara bado si ya kuridhisha mingi iliyopo ni ya kubabaisha kwana hata kampuni zilijenga ni kampuni uchwara za 10%!
Binafsi sitegemei mabadiliko makubwaa kama inavyowekwa chumvi na wanasiasa wetu sababu hata huko Geita, Mwadui, Bulyanhulu dhahabu imeanza kuchimbwa lini? Na angalia maendeleo yaliyopo kama kuna uwiano wowote na rasilimali zinazotoka maeneo hayo.
Mwisho napenda kusema tuwe makini sana tunapozungumzia haya mambo kwani yanahitaji uchambuzi wa hali ya juu sana tusiyatazame kwa juu juu.
 

Ndugu kazi ndo msingi wa maendeleo kama wewe ni mvivu tu hutaki kufanya kazi unakalia siasa hayo maendeleo utayasikia kwenye bomba tu utapigwa gap mpaka uzimie!jishughulishe na ufanye kazi kwa bidii u will see ua own development afu kumbuka Roma haikujengwa kwa siku moja we kalia kulala tu!
 
Weka picha


Haina haja ya picha kama umepita shule japo kidogo utakua unajua impact ya gas katika maendeleo ya nchi na eneo husika inakochimbwa sio kila kitu lazima uletewe picha ndo kanuni ya maeneo yenye miradi mikubwa ya uchimbaji lazima yapate mabadiliko!
 

mimi nakubaliana ma wewe moja kwa moja kwamba maendeleo yanayosemwa na watu ni tofauti sana na hali halisi, mi niilikuwa mtwara juzi lkn bado sijaona mabadiko kivile watu wanasifia, labda kwa upande wa usafiri uko bomba kwa sasa unachagua basi la kupanda na yote ni mazuri lkn ukizunguka baadhi ya mitaa iliyokuwa imechangamka miaka ya nyuma sasa ivi imedumaa sana nenda mitaa kama chikongola, majengo,mdenga, magomeni, tandika, na mingine mingi bado nyumba za kizamani sana barabara nyingi za mitaani haziptiki na gari, pale stand kubwa sasa ivi hakuna huduma ya tax kama zamani zimejaa toyo na bajaji,
kwa hiyo ndugu zangu wa mtwara bado mkoa unahitaji madiliko huo bado kbsaa kwa kuupa sifa ila tujitume kufanya kazi kwa bidii ndio msingi wa mabadiko na maendeleo
 
Mji wa mtwara huo
 

Attachments

  • 1430490277236.jpg
    110.8 KB · Views: 321
Hoja yako imekaa vizuri but ilitakiwa iende sehemu ya Uchumi na Biashara kuileta kwenye jukwaa la Katiba unaipunguzia nguvu, nakushauri uipeleke kule hapa achia Katiba!
Yani humu ndani kuna watu utaon ajinsi walivyokawa darasani ni watu wa kwenda kinyume kweny A anaandika C badala ya kuweka hii mada kwenye uchumi na siasa ye kaja kuipachika huku kwenye katiba
 
Weka hoja bhana hayo hayanna maana humu ndani kama picha kawaonyeshee huko kwenu

Bro ka kwenu wenyewe mmeshindwa kuweka Picha ,sisi wa huku tutaipata wapi ya Mtwara ? Na ndio maana nimewawekea hiyo ni picha shemeji yenu anawaacha vipi huko ,bro sio ugomvi ni vijimambo tu
 
Yaan hiyo habari yako bila picha ni kama mvua bila mawingu
 

Hilo ni suala la kuvuta subira tu kwani mji wa Roma ulijengwa kwa siku moja?gesi hapo imeanza kuchimbwa lini?unategemea kwa muda mfupi tu mabadiliko makubwa kiasi hicho, never maendeleo ni process na process yenyewe lazima wananchi waingie la sivyonwatanaki kutoa macho tu waache uvivu wafanye kazi kwa bidii na kutumia fursa za maendeleo zilizopo sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…