Maendeleo unayoyaona Mtwara ni maendeleo ya kawaida sanaa ambaya hayakuhitaji gesi tu ndio yafanyike, mimi binafsi kwa mtazamo wangu sijaona cha ajabu sana kama watu wanavyoongeza chumvi! Kwa kuanza na hizo hotel yaani hamna kitu kabisa sababu hata hiyo Naf Beach Hotel ni level za kariakoo tuu labda tusubiri hiyo itakayojengwa na jamaa wa Sea Cliff maana nasikia wamenunua eneo kule beach. Nyingi zilizojazana ni Lodges yaani nyumba za wageni za kawaida sana kwa mtu yeyote mwenye exposure ya maendeleo.
Tunapoangalia maendeleo usitazame kwenye burudani na starehe tu, angalia mambo ya mzingi kama shule na afya pia. Mfano Mtwara mbali ya yote uliyoyasifu mpaka sasa hakuna hospitali ya maana yenye uwezo wa kutoa vipimo vya kisasa! Hospitali inayotegemewa ni ya Mission ambayo iko zaidi ya Km 100 nje ya mji! Miundo mbinu kama barabara bado si ya kuridhisha mingi iliyopo ni ya kubabaisha kwana hata kampuni zilijenga ni kampuni uchwara za 10%!
Binafsi sitegemei mabadiliko makubwaa kama inavyowekwa chumvi na wanasiasa wetu sababu hata huko Geita, Mwadui, Bulyanhulu dhahabu imeanza kuchimbwa lini? Na angalia maendeleo yaliyopo kama kuna uwiano wowote na rasilimali zinazotoka maeneo hayo.
Mwisho napenda kusema tuwe makini sana tunapozungumzia haya mambo kwani yanahitaji uchambuzi wa hali ya juu sana tusiyatazame kwa juu juu.