Kuna kijana - wa umri wa A level hivi - ana tatizo la kiafya linalomkera sana na kumfanya hata kusoma darasani imnyanyase sana. Gesi nyingi hutengenezeka tumboni na mbaya zaidi inajitokea inavyotaka makalioni bila control.
Wadau naomba yeyote mwenye ushauri kuhusu kushughulikia hali hii asaidie. Kaishafika hospitali kadhaa lakini mafanikio bado.
Pole kwa shida hiyo ambayo haikondeshi ila inatia aibu, na hivyo yaweza kukuletea sonono.
Sababu yake
Kitalaamu hali hiyo inaitwa Flatulence. Watu wote na karibu wanyama wote wanapata flatulence (kiswahil kujamba), na kila mtu ambaye ni mzima aweza ajambe angalu mara ishirini kwa siku (yaani katika saa 24). Katika hali ya kawaida kutoa hewa kwa njia ya nyuma kunatokana na baadhi ya hewa huingia tumboni wakati wa kula na kumeza chakula. Na japokuwa baadhi ya hewa hiyo hufyonzwa na kuingia kwenye damu na baadae kutoka nje kupitia mapafu, sehemu ya hewa hiyo hubaki tumboni na ndio hiyo hupitia njia ya nyuma. Pili inafahamika tumboni kuna Organism wengi hasa aina ya bakteria. Pamoja na kazi nzuri yenye manufaa wanayoifanya lakini pia huchachusha baadhi ya vyakula vilivyoliwa, Na hivyo kutengeneza hewa (gas) hasa aina ya oxyegen, carbondioxide, methane,nitrogen nk.
Hata hivyo pamoja na sababu hizo hapo juu ambazo ni za kibiologia mtu aweza apate shida ya kujamba kuliko ilivyo kawaida. maradhi mengi yaweza sababisha hali hiyo. Hata hivyo shida ambayo imeonekana kusababisha hali hiyo kwa watu wengi ni mfumo wa uyeyushaji chakula kushindwa kuyeyusha vyakula aina ya wanga (carbohydrate) kikamilifu. Kama upo A level kama ulivyosema basi utakumbuka wanga huliwa ukiwa katika hali ya Polysaccaride, then huanza kumeng'enya tangu ukiwa mdomoni na kuwa disaccaride, na halafu ukiwa tumboni humeg'enywa na kuwa monosaccaride (yaani glucose) na hivyo kufyonzwa (absorbtion)kwenye utumbo na kuingia mwilini. Kuna kemikali zinaitwa mimeng'enyo
(enzymes or digestivu juice) ndio ambazo hufanikisha shuhuli hiyo. Kuna baadhi ya watu wana upungufu wa hiyo mimeng'enyo tumboni, na hivyo vyakula vya aina ya wanga huwa haviyeyushwi kikamilifu kufikia ile hali ya mwisho inayofyonzwa na mwili yaani monosaccaride. Hivyo masalia ya chakula aina ya wanga ambacho hakijayeyushwa kufikia monosaccaride hubaki kwenye utumbo na hivyo kuchachuswa ( fermentation) na hao organism wa tumboni na hivyo kuzalisha gas nyingi. Gas hizo hazina mahali pakutokea bali njia ya nyuma.
Nini cha kufanya?
Kwanza kuna baadhi ya vyakula ambavyo huzidisha shida hiyo, kama inawezekana itabidi upunguze kuvila, naamini unavifahamu. Chakula ambacho kikiliwa hakina gas hata kama una shida niliyoitaja hapo juu ni wali peke yake. Bahati mbaya huwezi kula wali peke yake!!??
Hata hivyo bahati nzuri ni kuwa uyeyushaji wa vyakula vya wanga huanzia mdomoni (kumbuka salivary amylase) hivyo hata kama una upungufu wa enzymes zingine hiyo iliyo kwenye mate yaweza kusaidia sana. Hivyo basi hakikisha
unapokula chakula unatafuna polepole na kwa muda mrefu mpaka tonge lote au funda lote la kinywaji kama chai, soda nk. vimechanganyika vyema na mate ya kutosha. maana yake ni kwamba hivyo vyakula aina ya wanga vinapofika tumboni vitakuwa vimeyayuswa kiasi cha kutosha na hivyo kuanza kufyonzwa, kwa maana hiyo hao intestinal organism hawatakuwa na wanga wa ku ferment, na shida yako yaweza kwisha.
Hongera kwa kuiweka shida yako wazi.