Gesi nyingi zaidi yagundulika bahari kuu Tanzania

Gesi nyingi zaidi yagundulika bahari kuu Tanzania

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Kampuni ya Statoil yaendelea kugundua gesi bahari kuu:

Oystein%20Michelsen.jpg

Meneja wa Statoil Tanzania, Oystein Michelsen


Kampuni ya Statoil na mshirika wake, Exxon Mobil, imetangaza matokeo mazuri ya majaribio ya gesi kwenye kitalu namba mbili katika kina kirefu cha bahari kisima cha Zafarani-2.

Kwa mujibu wa Meneja wa Statoil Tanzania, Oystein Michelsen, majaribio hayo kwenye kisima cha Zafarani-2, kimeonyesha kuwa na uwezo wa kutiririsha futi za ujazo milioni 66 kwa siku.

Alisema takwimu zilizopatikana kwenye majaribio hayo, ni muhimu kwa ajili ya kupunguza shaka inayoweza kuwapo siku za usoni kuhusu gesi iliyoko ya kina kirefu cha bahari na gesi ya kusindikwa hapa nchini.

Alifafanua kuwa majaribio ya uchimbaji yalifanywa katika kisima cha Zafarani-2 urefu wa mita 2,400 ndani ya kina kirefu cha bahari na ikiwa ni umbali wa kilomita 80 kwenda nchi kavu.

Alieleza kuwa baada ya majaribio ya kisima cha Zafarani-2 , kutafuatia uchunguzi wa kiwango cha gesi kwenye kisima cha Zafarani-3, ambacho ndicho cha mwisho kwenye utafiti katika hifadhi ya gesi kwenye kitalu namba mbili.

Alisema kutangazwa kwa matokeo ya majaribio ya kisima cha Zafarani-2 kunafuatia ugunduzi kwenye kisima cha Mronge-1 kulikofanyika Desemba 2013, ambako kunafanya ugunduzi huo kuwa kisima cha tano kwa utafiti unaofanyika kwenye kitalu namba 2.

Alisema ugunduzi huo umefanya jumla ya kiasi cha gesi iliyogundulika kufikia futi za ujazo wa kati ya trilioni 17-20 (Tcf).

Alisema kabla ya ugunduzi uliotokea kwenye kisima cha Mronge-1 kulikuwa na ugunduzi mkubwa gesi wakati wa uchimbaji wa awamu ya kwanza kwenye kisima cha Tangawizi-1, Zafarani-1 na Lavani-1, na ugunduzi mwingine kwenye kisima cha Lavani-2.

Kampuni ya Statoil ina leseni ya kufanya utafiti katika kitalu namba mbili kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), ikiwa na asilimia 65 wakati mbia wake kampuni ya ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Ltd ikichukua asilimia 35.

Kampuni ya Statoil imekuwa Tanzania tangu mwaka 2007, ilipopewa leseni na serikali kwa ajili ya kufanya utafiti kwenye kitalu namba 2.


CHANZO: NIPASHE
 
Mafisadi walikwishaingia mikataba ya gesi hata kabla haijagunduliwa. Bila CCM kuondoka madarakani, watanzania waendelee tu kuhesabu maumivu ya ufukara! Hakuna nafuu ya maisha!
 
Tanzania ni nchi tajiri kupindukia lakini wanasiasa wetu wamekosa maadili na uzalendo! Maliasili kibao! Lakini kila wakati tunalia njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka!
 
mara zafarani,mara tangawizi,mtatuambia sasa pilipili,hayo maeneo mbona hayasemwi yapo mikoa ipi,au utafiti huo ni siri?
 
Hizo hadithi za mali asili mbona zipo kila cku? Tatizo ni uongozi mafisadi na watoto wao ndo wanafaidi wakati akina ritiz wanaambulia kofia na T shirt
 
Matunda ya nnchi hii tutayafaidi vizuri endapo tutatumia kura zetu vizuri kumchagua rais ajaye.lasivyo kwa aina ya watawala tulio nao hata tukigundua kisima cha kuchimba dola,wananchi tutaendelea tu kulalamika,Mungu ibariki Tanzania
 
ha! ha! ha! a/c za uswiss na new jersey zimefurika!sasa kwa neema hii mpya sijui tukafiche wapi?
 
Hiyo gesi iliyovumbuliwa itatufaidisha vipi wananchi wa kawaida?
 
Mungu ulikwisha ibariki Tanzania , tunakuomb usije iondoa baraka hi na kutuletea laanaa
 
Mi nijuavyo ugunduzi wa kila kitu hapa Duniani ulifanywa miaka 100 na zaidi iliyopita. Hawa wazungu wanaijua dunia yote kila penye kila kitu, just wanafanya usanii wa kujustify gharama zitakazokuwa implanted kwa kisingizio cha kugundua ilihali wanasoma ramani za mababu zao tu zinazoeleza ugunduzi uliofanywa kitaaaambo.
 
"Sasa hivi tunazungumzia Uchumi wa gesi Tanazania", mwisho wa kunukuu!
 
Back
Top Bottom