Gesi tumboni

Gesi tumboni

Green Apple

Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
84
Reaction score
10
Please doctors nahitaji msaada,nina tatizo la gesi kujaa tumboni kupita kiasi as a result tumbo linatoa muungurumo. Hospitals nikienda napewa dawa za minyoo they never help and even if they did ni temporary. Help me jaman nakosa raha
 
kanunue dawa inaitwa MUCOGEL.....itakusaidia
 
Acha kula machipsi ya mitaani na maharage. Tumia PPI kwa mwezi 1 na Antiacids masaa 2 kabla ya mlo na masaa 2 baada ya mlo na unapoenda kulala.
 
Ni vyema ukajua tatizo linaanzia wapi. Kwa ninavyofahamu, gesi ya tumboni huwa ni kiasi kidogo tu ambacho huingia wakati tunakula. Unapoona inafikia kuwa kero kubwa mpk unashindwa kukaa vyema basi upo uwezekano ikawa ni dalili za vidonda vya tumbo.

Fanyia utafiti hilo, jaribu kula pilipili au kukandamiza bia ukiwa na njaa, ukiona maumivu na viungulia ujue hivyo ni vidonda vya tumbo.
 
Ni vyema ukajua tatizo linaanzia wapi. Kwa ninavyofahamu, gesi ya tumboni huwa ni kiasi kidogo tu ambacho huingia wakati tunakula. Unapoona inafikia kuwa kero kubwa mpk unashindwa kukaa vyema basi upo uwezekano ikawa ni dalili za vidonda vya tumbo.

Fanyia utafiti hilo, jaribu kula pilipili au kukandamiza bia ukiwa na njaa, ukiona maumivu na viungulia ujue hivyo ni vidonda vya tumbo.

pilipili nakula ila sometimes naumwa na tumbo,bia sinywi nijaribu kitu gan?
 
Kuondosha Gesi tumboni kwa Dawa za Kienyeji, Gesi na Indegestion:
Kunywa juisi ya pea iliyochanganywa na tembe 3 za kitunguu Saumu kabla ya kulala kila siku.
 
hili tataizo ni kubwa siku hizi,inshakunywa sana maginisium lakini wapi
 
Mimi nilipata hayo matatizo kuna wakati kutokana na majukumu niliokuwa nayo wakati huo hata lunch zikawa zinanipita nilikuja kuumwa na tumbo balaa. Mwisho nikaenda hospitali wakaniandikia suspension fulani ambayo ndani kuna kama chenga chenga unatikisa unakunywa ni antiacid inaondoa ma gesi gesi, maana tumbo lilikuwa linanguruma utafikiri mtu anachemsha maji sijui kitu gani.Hii dawa ipo over the counter kwenye pharmacy.

NIlipopiga na mazoezi nikawa fiti.
 
GESI TUMBONI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.
 
Pole sana mkuu hizo ni dalili za vidonda vya tumbo. nenda hospital ucheck kipimo kinaitwa H-PYROL ili kujua tatizo ni nini usikimbilie dawa bila kujua chanzo cha ugonjwa. ila ni dalili tosha ya vidonda vya tumbo.... Pole sana
 
Back
Top Bottom