Asante sana Malila uko sahihi kabisa. Ni kweli LPG (liquified petroleum gas) ina calorific value zaidi ya natural gas kwa mbali tu. Sijui kiswahili sahihi cha calorific value lakini tunaweza sema ujoto wake unaotoa ikiungua na oksijeni. Hivyo kwa kifupi moto wa LPG (oryx, mihan, Bp, Lake gas) ni mkali zaidi kuliko natural gas.
Methane has just a single carbon atom and four hydrogen atoms (CH[SUB]4[/SUB])
Butane has four carbon atoms and ten hydrogen atoms (C[SUB]4[/SUB]H[SUB]10[/SUB])
Propane has three carbon atoms chained together with eight hydrogen atoms (C[SUB]3[/SUB]H[SUB]8[/SUB])
Kikubwa nadhani watu wengi hatuna elimu ya gesi au ufahamu japo kidogo. Ni kweli gesi ya oryx, lake gas na mihan zinatoka uarabuni kama mchangiaji hapo juu alivyosema. Zinatoka Uarabuni sababu ni zao la petroleum na huko ndiko inapopatikana. Hivyo kufikia hapa tuondoe notion kichwani kuwa mbona oryx Gas mjini bei juu wakati tunaichimba Mtwara, gesi inakuwa imported na meli kama yalivyo mafuta mengine hivyo mafuta kwenye soko la dunia yakipanda lazima gesi nayo ipande. LPG ni zao la kwanza petroleum inapoingizwa kwenye refinery kuwa heated. Inaanza propane na butane at just 20c then inafuatia petrol, mafuta ya taa, dizeli nk. Mtungi wa gesi ulionao nyumbani ni mchanganyiko wa butane na propane. Kama ni mteja wa oryx unaweza kusoma kwenye kola ya mtungi utaona wamekuandikia all technical details pale. Kama oryx wao butane ni 80% na Propane ni 20% (hapa ikumbukwe propane is more expensive and calorific ndio maana margin yake iko chini kidogo)
Lpg ukiiCompress kwenye mtungi inageuka liquid hivyo safe kusafirisha hata misukosuko inahimili ndio maana tukienda kununua tunanunua kwa kilo. Natural gas ni tofauti kuicompress ni mbinde na haiwezi kuwa total liquid zaidi ya just compressed gas na huwezi kuiweka kwenye mtungi wa chuma wa kawaida tu kama gesi nyingine. Compressed natural gas kwenye cylinder ni bomu tosha. Mtungi wake ni expensive kama utataka uiweke kwenye mtungi maana umetengenezwa kama thermos ya chai, yani several layers kabla ya kufikia kichupa cha gesi yenyewe.. Hivyo natural gas ina changamoto zake vilevile.
Kama mlaji nafurahia uwepo wa gesi asilia ambayo itasambazwa majumbani kwa bei nafuu kama wanavyosema. Lakini kikubwa kwangu ni usalama. Tumejipanga vipi katika suala zima la kuhakikisha kuwa tuko salama na ajali zihusianazo na milipuko ya gesi kama tumeshindwa kujipanga katika miundo mbinu mingine isiyolipuka hapa hapa mjini. Tazama mifuniko ya barabarani inavyoibiwa, nyaya za umeme mchana kweupe, mabomba ya maji yanavyokatwa na watu kujiunganishia, alama za kuonyesha bomba la gesi la sasa linapita nyingi zishaibiwa tayari nenda gerezani watu wanaziyeyusha kutengeneza spacer za magari za aluminium. Je kwenye mabomba ya gesi itakuwaje? Kibaka Athumani ataelewa kuwa hili ni bomba la gesi liko nje nje nisilikate au nilikate niuone mchana...