Geza Ulole

Geza Ulole

Sam GM

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
535
Reaction score
30
Geza Ulole

Kuna baadhi yetu wakati tunakuwa (growing up) tulisikia sana neno Geza Ulole, hata wakati mwingine tuliweza kuimba mashuleni kuhusu Geza ulole, baadhi yetu hatukuelewa maana halisi ya geza ulole. Kulikuwa na bendi kadhaa za muziki ambazo ziliimba kuhusu watu wahame kwenda Geza ulole, nafikiri hii ilikuwa kipindi cha vijiji vya ujamaa kama sikosei.

Wengine tumeishakuwa watu wazima ila maana halisi ya Geza ulole, ilitoka wapi, ilimaanisha nini na iliishia wapi bado ni kitendawili. Pamoja na kuwa hii sio issue ya kuleta maendeleo na mabadiliko ya nchi yetu, lakini kwa baadhi yetu itatusaidia kujua tumetoka wapi na vipi na kuijua historia ya nchi yetu.

Kama kuna anayejua hali halisi na mazingira yote ya Geza ulole basi ni ombi atusaidie kutupa ufahamu zaidi wa hii Geza ulole.

Natanguliza shukrani.
 
Kwanza Geza Ulole ni sehemu kusini mwa Dsm,kwa sasa kuna makabila mchanganyiko pale,kuna kilimo cha kutia moyo. Zaidi ya Gezaulole kulikuwa/kipo kijiji cha Kibugumo. Vijiji hivi vilipokea watu kutoka Dsm mjini ili wakaanzishe/wakafanye kazi za kilimo ktk maeneo hayo badala ya kuzurula Dsm.

Kama sijakosea hizo zilikuwa enzi za Mkuu wa mkoa Mzee Songambele,kwa hiyo bendi na nyimbo nyingi ziliimbwa ili kuhamasisha zoezi la kila mwenye nguvu akafanye kazi.

Kwa sehemu nimechangia mkuu.
 
Tafuta mchezo wa kuigiza unaoitwa GIZA LIMEINGIA, umeisawiri zahama ya Gezaulole!
 
Geza ulole mamaa, Geza Ulelo
Nakwenda mpaka Kibugumo na mwana dilatu

Kulikuwa na wimbo unatamba sana enzi zile sikumbuki ulipigwa na nani, Mlimani Park, UDA Jazz?
 
Malila,

shukrani sana kwa hiyo info.
 
Masatu,

Shukrani mheshimiwa, sina uhakika hii ni lugha gani, ila baso sijakuwa na mwangaza wa kutosha walitakiwa kuiga nini au kutoka wapi. Thanks!
 
Kama alivyosema mkuu hapo juu

Geza Ulole = Geza Uone, sijui context yake ni nini, inawezekana unahamasishwa kuishi maisha ya kijiji cha ujamaa ili uone uzuri wake, au inawezekana ilitoka kabla ya ujamaa kwenye context ya warning a la "muiga tembo kunya hupasuka msamba".

Hii ni lugha ya Kizaramo, wakazi wa asili wa maeneo haya ni Wazaramo lakini maneno haya , kama maneno mengi ya lugha zetu za kikabila, yako common katika kabila nyingi (lola = ona, ulole = uone)
 
Geza Ulole

Kuna baadhi yetu wakati tunakuwa (growing up) tulisikia sana neno Geza Ulole, hata wakati mwingine tuliweza kuimba mashuleni kuhusu Geza ulole, baadhi yetu hatukuelewa maana halisi ya geza ulole. Kulikuwa na bendi kadhaa za muziki ambazo ziliimba kuhusu watu wahame kwenda Geza ulole, nafikiri hii ilikuwa kipindi cha vijiji vya ujamaa kama sikosei.

Wengine tumeishakuwa watu wazima ila maana halisi ya Geza ulole, ilitoka wapi, ilimaanisha nini na iliishia wapi bado ni kitendawili. Pamoja na kuwa hii sio issue ya kuleta maendeleo na mabadiliko ya nchi yetu, lakini kwa baadhi yetu itatusaidia kujua tumetoka wapi na vipi na kuijua historia ya nchi yetu.

Kama kuna anayejua hali halisi na mazingira yote ya Geza ulole basi ni ombi atusaidie kutupa ufahamu zaidi wa hii Geza ulole.

Natanguliza shukrani.

  • Gezaulole maarufu kama GEZA ni km 12 tu toka feri-kigamboni.
  • Kibugumo ni km 10 tu toka feri-kigamboni.
  • Kwa jinsi ilivyokuwa inasikika zamani ilionekana kama ni vijiji ambavyo viko mbali sana na mji, lakini kwa kweli ni karibu sana.
  • Toka feri mpaka gezaulole ni lami tupu na pembeni mwa geza kidogo upande wa beach zimejengwa nyumba nzuri sana zilizokuwa zinauzwa kama milioni 300, ziko kama 80 hivi na nafikiri zilizinduliwa na magufuli by then akiwa waziri wa ardhi.
  • Sehemu hii kuna ndugu zake na nyerere wengi sana, kama mnavyojua tena nyerere hakupenda kujuana sana, kwa hiyo ndugu zake waliojipendekeza kuja kwake aliwapeleka pale GEZA wakalime, na kwa kweli wanamashamba makubwa sana ambayo kipindi yalikuwa haya thamani kabisa ila siku hizi GEZA ni sehemu amabyo ni ghali kwelikweli.
  • Ukienda mbele kidogo kuna viwanja vya mradi vilivyogawiwa nafikiri ilikuwa mwaka 2004-05 (Viwanja vya Dungu).Kijiji kinachofatia ni MWONGOZO(17km) nako kuna viwanja vya mradi pia. Viwanja hivi bado havijajengwa sana ila mtu mmoja mmoja na vingi ni vya WAKULU waliowawekea vitukuu vyao.Viko baharini kabisa. sababu nyingine kubwa ni kukosekana kwa umeme ingawa GEZA-center umeme tayari umefika. Umeme huu pia unapelekwa kimbiji ambako kunategemewa kujengwa kiwanja cha cement. Nguzo za umeme tayari zimesimama.
  • Geza ndio hoteli moja inaitwa BAMBA Beach, maarufu sana kwa wekundu wa Msimbazi kuweka kambi yao pale.
  • Ukienda mbele-kimbiji, kama 30km kuna hoteli kubwa mbili, Amani ngovu, na raskutani. hoteli hizi zinajulikana ulaya zaidi kuliko kwa wazawa na kuna kiwanja cha ndege kidogo pale. kwa hiyo wazungu wakifika "kwa wazee wa kipawa" wanaruka moja kwa moja mpaka kwenye hizi hoteli.
  • Kitu kingine muhimu cha kufahamu pale GEZA ni kuwa kuna heka 700 zilizokuwa za nafco ambazo alikabidhiwa mzee wa YEBOYEBO-MANJI (usione waisilamu wanalia pale chang'ombe wamekutana na mtaalamu) Ziko kati ya GEZA na KIBUGUMO. Kwa hiyo manji ana heka zake 700 pale safi ingawa kuna tetesi kuwa kishazipiga bei kwa hela ndefu mnooooo, of course makamba alikuwa na share yake.

Kama kuna swali jingine kuhusu geza na Kigamboni yake wewe uliza tu mkuu.
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana,mitaa ya Kibada,kisarawe Two,Mwasonga nk. Bila shaka muuliza swali amepata majibu,zaidi ya hapo aende mwenyewe huko Geza.
 
Geza Ulole wapo ndugu wengi wa Nyerere,on the distaff side,yaani,ndugu wa Mama Maria Nyerere.
 
Ni kweli kabisa mkuu, hata kaburi la dada yake maria nyerere liko pale.

Harafu kitu kingine ni kuwa, mchakato wa kupima viwanja pale umeanza ingawa kwa manji heka zake 700 hawagusi!!!!!!!!. Ni kwa hao walalahoi ambapo manispaa wameshabandika matangazo kuwa watu wajiandae kutafuta vijiji vingine, pale hapawafai tena.
 
Na ajabu ni kwamba ndio sehemu iliyoendelea na kilimo na hakuna njaa..Leo hii wakubwa wote wanataka kuhamia pale viwanja bei mbaya!...Ama kweli GEZA ULOLE weee!
 
Naami mwenye jina ndo mimi, vp kuna tatizo humu ndani? Geza=Iga Ulole=Uone unakaribishwa
 
Bluray,
Thanks. Umeniwahi nilitaka kusema hivyo. Na kilikuwa na ufanisi mkubwa. If only other villages had followed the example of Geza Ulole. Au hawa viongozi baada ya Nyerere wasingekuwa mafisadi.................
 
Back
Top Bottom