Ghafla huyu anayejiita Mzee Mpili eti kawa maarufu

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Hii nchi ya Tanzania ukiamua kufa kwa stress au umasikini basi utakua umejitakia mwenyewe.

Unaweza kiutani utani tu ukawa maarufu na ukapiga pesa. Huyu anajiita Mzee Mpili eti kwa sasa ni mtu maarufu Tanzania, anaalikwa hadi na vituo vya redio kubwa maarufu kama wasafi FM.

Anyway hua wanapita, walianza akina Dokta Shika, akaja mchungaji anayekata mauno, akaja Pierre Likwidi, na sasa Mzee Mpili..mnaweza shangaa akapata hadi ubalozi wa kampuni kubwa. Maisha haya bwana! Watu wanajua kucheza na alama za nyakati.
 
Hii nchi ya Tanzania ukiamua kufa kwa stress au umasikini basi utakua umejitakia mwenyewe.

Unaweza kiutani utani tu ukawa maarufu na ukapiga pesa. Huyu anajiita Mzee Mpili eti kwa sasa ni mtu maarufu Tanzania, anaalikwa hadi na vituo vya redio kubwa maarufu kama wasafi FM...
Ni hulka ya binadamu kupenda vitu vipya vyepesi kila uchao.. Vitu vigumu hukimbiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umaarufu bila hela.

Yuko hapo kariakoo anagongea mpaka mihogo ya jero
 
Nakubaliana na wanaosema "Tanzania kuna ujinga mwingi". Kuna kipindi Piere Liquid alikuwa maarufu hadi akalipiwa gharama kusafiri na timu ya Taifa. Leo tena Mzee Mpili kisa tu aliyosema kwamba Yanga itaofunga Simba goli 2 yakiwa machache 1 basi mashabiki wa timu zote wanaimba Mpili Mpili kwa namna tofauti.
 
Na yanga wakishinda tena kgm umarufu wa dingi utazidi hata kama yanga wanashinda kwa kubahatisha tz maajabu hayawezi kuisha.
 
Na kule Kigoma kwa kauli yake mwenyewe mzee mpili anasema Nyuklia zitakuwa zakutosha na sio moja tena
 
Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nikitafakari sana Promo anayopewa Mzee mmoja anayeitwa Mpili.

Ambalo nimekuja kugundua sisi Watanzania ni watu wa kuamini kuwa uchawi/ushirikina ni njia ya kuleta mafanikio.

Wengi hawaamini kwamba kujiamini,kupanga mipango,kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuwa na nidhamu kama misingi ya mafanikio.
Inahuzunisha sana kwa kushabikia ushirikina kama njia ya mafanikio.
 
Inahuzunisha sana kwa kushabikia ushirikina kama njia ya maa
alisikika shabiki wa simba mwenye uchungu na timu yake. ukweli ni kwamba mambo ya mpili ni mind game tu hamna uharisia, ila tu ni ku take attention ya timu pinzani na kuwafanya wapunguze confidence
 
Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nikitafakari sana Promo anayopewa Mzee mmoja anayeitwa Mpili.
Ambalo nimekuja kugundua sisi Watanzania ni watu wa kuamini kuwa uchawi/ushirikina ni njia ya kuleta mafanikio.
Wengi hawaamini kwamba kujiamini,kupanga mipango,kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuwa na nidhamu kama misingi ya mafanikio.
Inahuzunisha sana kwa kushabikia ushirikina kama njia ya mafanikio.
Kwa akili yako ndogo unahisi kila mtu anayemshabikia Mzee Mpili anaamini ushirikina?mfano kwa upande wangu namkubali Mzee Mpili kwa kuongea kwake kwa kujiamini bila kuogopa mtu na kufanya kuleta Raha kwa Yanga na labda nkuulize Manara anavyosemaga Simba itashinda kwa goli 3 na kuendelea dhidi ya Yanga naye pia ni mshirikina?
 
Back
Top Bottom