Ghafla huyu anayejiita Mzee Mpili eti kawa maarufu

Ghafla huyu anayejiita Mzee Mpili eti kawa maarufu

Ushirikina upo uamue kuamini au usiamini upo?

Tulizoea kuona wachawi wakiukana hadharani na wakiufanya gizani ndo maana hatuwaoni, sasa huyu mzee anajisema waziwazi ndo hicho kimekua habari kubwa.

Wewe akili weka kichwani mwako usiangukie tu huko na kuanza kuupractice!! Ila upo.
 
alisikika shabiki wa simba mwenye uchungu na timu yake. ukweli ni kwamba mambo ya mpili ni mind game tu hamna uharisia, ila tu ni ku take attention ya timu pinzani na kuwafanya wapunguze confidence
Hahaha...ww una akili ndugu,
Lkn tusifanye mind game kwa kutukuza ndumba.
 
Kwa akili yako ndogo unahisi kila mtu anayemshabikia Mzee Mpili anaamini ushirikina?mfano kwa upande wangu namkubali Mzee Mpili kwa kuongea kwake kwa kujiamini bila kuogopa mtu na kufanya kuleta Raha kwa Yanga na labda nkuulize Manara anavyosemaga Simba itashinda kwa goli 3 na kuendelea dhidi ya Yanga naye pia ni mshirikina?
Jifunze kujenga hoja bila kumdharau unayepingana naye,itakusaidia maishani.
 
Umeegemea upande mmoja tu wa ushirikina, huenda ndiyo lengo la hoja yako.

Kwangu mimi naiona hii promo ni upepo tu kama kina Pierre Likwidi na Dr Shika.

Hapo ndo unaona Watanzania ni watu wa matukio ya aina gani, na hata vyombo vyetu vya habari ni kukuza upuuzi tu 24/7.

Leo Mzee Mpili mahojiano kila kona na hachelewi kuwa balozi wa kampuni fulani fulani uchwara.
 
Hii nchi ya Tanzania ukiamua kufa kwa stress au umasikini basi utakua umejitakia mwenyewe.

Unaweza kiutani utani tu ukawa maarufu na ukapiga pesa. Huyu anajiita Mzee Mpili eti kwa sasa ni mtu maarufu Tanzania, anaalikwa hadi na vituo vya redio kubwa maarufu kama wasafi FM.

Anyway hua wanapita, walianza akina Dokta Shika, akaja mchungaji anayekata mauno, akaja Pierre Likwidi, na sasa Mzee Mpili..mnaweza shangaa akapata hadi ubalozi wa kampuni kubwa. Maisha haya bwana! Watu wanajua kucheza na alama za nyakati.
Mzee Mpili si ameingia na kiki ya mzee wa kazi 😅😅😅
 
Kuna wajinga wataenda hadi uko ikwiriri akawatatulie shida zao kwa njia za kishirikina,na hivi ana sauti Fulani ya mkwara ya kuita majini,lazima awapige wazembe uyu muhuni wa mzizima, hawezi kuwaacha salama, kama babu wa loliondo.
Hahahaahahaha atawatandika hela kweli
 
'Watu wake' wameshamaliza mchezo!
20210706_120259.jpg
 
Back
Top Bottom