Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Hayati John Magufuli alipambana sana Uzalishaji wa mgodi wa Nickel wa Kabanga Nickel uanze uzalishaji akiwa hai. Mipango ya Mungu huwa ina tofauti na ile ya binadamu.
Hakuweza kuishi mpaka kuona haya yanayoendelea hivi sasa. Angeridhika kwa asilimia mia moja. Utoke jasho kuupigania mradi mkubwa wenye maslahi ya kiuchumi halafu ufanikiwe, na wewe usiwe na sababu ya kugongesha glasi za mvinyo na marafiki zako, hiyo haiwezekani.
Lengo la JPM lilikuwa ni uanzishwaji wa Mkoa mpya unaojumuisha Chato na wilaya zote zilizo karibu. Utajiri wa mradi wa Nickel utauhakikishia mkoa huo mapato ya uhakika. Ndio maana hayati akapigana kadri alivyoweza na alipofariki akaacha hatua za mwishoni za ukamilishaji wa uanzishwaji wa mradi.
Kichekesho ni huu upendo 'mpya' unaoonyeshwa na baadhi ya wabunge ya kuwataka watu wa Ngara wasiunge mkono nia ya kuwa na mkoa watakaokuwa na ushawishi na pengine maendeleo ya kweli. Bukoba ni kilomita 320 kutoka Ngara, ni mbali kulinganisha na Chato.
Wanakuja na utetezi wa kihistoria ambao hauna faida yoyote zaidi ya kuendeleza 'status quo' ya siku zote. Wanataka waendelee na kujikweza na kujitukuza kupitia uwepo wa Bukoba kama makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Ni mawazo yale yale ya kuendeleza 'ubwenyenye' ule ule wa miaka yote. Ni aina ya mawazo yeny dharau za kikabila ya kutaka ustaarabu ubakie ule ule wa miaka yote.
Miaka imepita kwa kasi na sasa kama taifa tunaitafuta miaka 60 ya Tanzania. Kama ni mtu tayari keshakuwa mtu mzima, hawezi kuishi kwa kukariri akiongozwa na falsafa zile zile za kale. Baadhi ya mikoa inajikuta ikikumbatia umaskini kwa sababu ya wanasiasa kuamini katika utamaduni ule ule wa siku za nyuma, pasipo kukubaliana na mabadiliko yanayokwenda sambamba na ukuaji wa miaka 60 ya Tanzania.
JPM alipambana mpaka mradi wa Nickel umeanza kazi. Mkoa wa Kagera unahitaji changamoto mpya ili uweze kuondokana na kuongozwa na hulka zile zile zisizoyagusa maisha ya mtu mmoja mmoja. Tuondokane na hizi imani potofu za kisiasa zinazodumaza maendeleo ya ukanda ule. Ni wakati wa baadhi ya watu wa Kagera kuanza kufikiria upya uwepo wa mkoa mpya wenye kila sababu za kisasa za uwepo wake.