Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Posts
5,551
Reaction score
2,153
Leo Machi 12, 2022 Wakili wa Kampuni ya GSM, Alex Mgongolwa amefanya mkutano na Waandishi wa habari kuanzia saa 6 kamili Mchana, GSM HQ Salamander Tower Samora Avenue.

====

Kilichojiri, full text:

======

Mwanasheria:
Huu hapa ndiyo uthibitisho, nimesema ni kielelezo namba moja, mteja wangu aliponambia nilichukua hatua ya kwenda kukithibitisha Wizara ya Ardhi nao walithibitisha na kithibitisho hiki hakijapatikana mtaani, kimepatikana katika mamlaka ambayo inatambulika.

Ukichukua namba ya kiwanja ukaenda Masjala ya Ardhi matokeao yatakuja mmiliki wa kiwanja hiki ni Ghalib Said Muhamed, na ukifikia Masjala ya Ardhi ukaonesha kiwanja namba ngapi, hati namba ngapi utapata matokeo hayo ambayo nimekueleza, hata hao ambao wanaodai kwamba hiki kiwanja ni cha kwao wakienda watapata matokeao hayo.

Baada ya umilikishwaji huu, mteja wangu alidhamiria kufanya maendelezo kwa kuwa alikuwa na nia ya kufanya maendelezo ambayo ni ya kimsingi yana gharama kubwa, aliamua mnamo tarehe 19, Septemba 2019 kuingia kwenye mkataba wa ujenzi na kampuni ya ujenzi inayoitwa Group 6 Internatinal, na huu ndio mkataba wa ujenzi na unajieleza. Kwa hiyo huingii mkataba wa kuendeleza ujenzi kama kiwanja hicho hakipo kwa jina lako, naomba mziangalie hizo tarehe vizuri nitazieleza baadaye kutokana na upotoshaji wa tarehe ambazo kimsingi hazihusiani kabisa na kiwanja hiki.

Anaendelea:
Kwa kuwa sheria ya nchi hii hazikuruhusu wewe kufanya maendelezo bila kibali, mteja wangu alifuata taratibu za kuomba kibali na kibali kilitoka kuwa ana ruhusa ya kufanya maendelezo na kilitoka 16, Oktoba 2017 na kilitoka kwa jina la Ghalib Said Muhamed, na unapofanya maombi ya kibali lazima mamlaka ijiridhishe kuwa wewe ndiye mmiliki na kama jina litakuwa tofauti hutapata kibali.

Na kwa kuwa mamlaka ya Ardhi Kinondoni ilijiridhisha na kumpa kibali, Mkandarasi akaanza ujenzi na Mteja wangu alilipa fedha zote na hadaiwi na Mkandarasi na kuna Risiti za TRA ili kuonesha kuwa mteja wangu ndiye mmiliki na alianza kumili kiwanja mwaka 2016, alifuata taratibu zote za kumiliki na kujenga na kwamba ana vibali vyote.

Anamalizia:
Kwa kumalizia, upo upotoshaji wa kidhana ambao sio sahihi kwamba ardhi mnaweza mkamilikishana watu wawili kama mtakavyotaka. Hii sio sawa na haiko kisheria, kwanza mmliki wa Ardhi ni Rais na sisi tunafanya upangishaji ambao utatajwa muda kama ni miaka 30, 100 nk. Hivyo ili umiliki Ardhi ni lazima mauziano hayo ya ardhi mamlaka ithibitishe.

Sisi kama wanasheria, mteja wetu ametuagiza kutoa vielelezo vyote ili kuonesha kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa ardhi hiyo na kwamba mtu yeyote anayedai kuwa ni mmiliki wa ardhi hiyo atoe hadharani vithibitisho vya kisheria vilivyothibitishwa na mamlaka husika kuwa yeye ni mmiliki.

Pili, Mteja wangu ametuelekeza kulinda heshima yake ya kibiashara kwa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote anayefanya upotoshaji wowote.

Pia, soma: Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

KATIKA HABARI:

MFANYABISHARA Ghalib Said Mohamed maarufu GSM, ametoa vielelezo kadhaa vinavyoonesha kuhusika katika umiliki wa eneo lenye mgogoro baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa video ambayo Makonda alionekana akidai kuwa eneo hilo ni la kwake huku akiwa amezingirwa na watu akiwemo askari aliyevalia sare za jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 12 Machi 2022, Mwanasheria wa GSM, Alex Mgongolwa, amesema mteja wake amempa maelekezo ya kukanusha umiliki wa Makonda na kuchukua hatua zaidi ikwemo kwenda mahakamani endapo ataendelea kudai eneo hilo ni lake.

“Leo tumewaita hapa ili kuwapa taarifa fupi ya uhalali wa umiliki wa eneo lenye Plot namba 60 lililopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni, Dar Es Salaam,” amesema Mgongolwa.

Mgongolwa amesema Mohammed alinunua ardhi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi tarehe 21 Novemba 2006 na kuonyesha waandishi wa habari nyaraka za udhibitisho.

271608744_467718128056333_5940805006310550358_n-300x189.jpg

Amesema Tarehe 19 Septemba 2017, Mohammed aliingia Mkataba na Kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International wenye thamani ya Sh 640 milioni “na hii ni nakala ya Mkataba huo.”

Aidha, ameongeza kuwa mteja wake aliomba kibali cha ujenzi na Manispaa ya Kinondoni walitoa kibali cha ujenzi tarehe 16 Oktoba 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya kuanza ujenzi wa eneo hilo.

“Baada ya kibali kutolewa, Group Six walianza ujenzi na walipeleka maombi ya malipo ya awali ya ujenzi tarehe 31 Januari 2018 na Ghalib Said Mohammed alitekeleza sehemu ya Mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh 51.9 milioni na kuna kithibitisho cha risiti ya TRA,” amesema.
 
Kijana mwenzetu, Makonda.
Tunajua ulishafanya mengi mabaya katika awamu ya tano ukiwa karibu na Jiwe, ni wakati wa kuwa mpole na kuachia mali ulizozipata kwa dhuluma zirudi kwa wenye nazo.

La sivyo utazidi kujitafutia matatizo makubwa
 
Back
Top Bottom