Ghamara za kulipa Deni la Serikali zimepanda kufikia Tsh. Trilioni 13.13 kutoka Tsh. Trilioni 10.48

Ghamara za kulipa Deni la Serikali zimepanda kufikia Tsh. Trilioni 13.13 kutoka Tsh. Trilioni 10.48

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kiwango cha Fedha zinazotumika kulipa Madeni likiwemo Deni la Serikali kimeongezeka kutoka Tsh. Trilioni 10.48 za mwaka 2023/24 hadi kufikia Tsh. Trilioni 13.13 mwaka 2024/25

Kwa mujibu wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha, Serikali imetenga kiasi hicho cha Fedha kwa mwaka huu ikiwa ni kwaajili urejeshaji wa Fedha za zilizokopwa kupitia Deni la Serikali

Kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hadi kufikia Juni 2023, Deni lilikuwa Tsh. Trilioni 82.25 sawa na ongezeko la 15% kutoka Tsh. Trilioni 71.31 lililokuwepo mwaka 2021/22.

====

Pia soma: Serikali inapanga kutumia Tsh. Trilioni 12.10 kulipa Deni la Taifa, Mishahara Tsh. Trilioni 11.77
 
Attachments

Kiwango cha Fedha zinazotumika kulipa Madeni likiwemo Deni la Serikali kimeongezeka kutoka Tsh. Trilioni 10.48 za mwaka 2023/24 hadi kufikia Tsh. Trilioni 13.13 mwaka 2024/25...
Safi sana na Jana tu tumekopa Korea tril2... bado miez ijao ...bado
 
Ukiongeza na hii $2b za wacheza sinema mwakani itakuwa 15tr
 
Kiwango cha Fedha zinazotumika kulipa Madeni likiwemo Deni la Serikali kimeongezeka kutoka Tsh. Trilioni 10.48 za mwaka 2023/24 hadi kufikia Tsh. Trilioni 13.13 mwaka 2024/25...
Lucas mwashamba huto muona hapa
 
Ukiongeza na hii $2b za wacheza sinema mwakani itakuwa 15tr
Kwahiyo kwa kipindi cha miaka 3, amekopa trilioni 13 tayari?

Na zinaonekana kwenye namba E kama kiashiria cha ukuaji wa uchumi kwa mujibu wa mbobevu waziri sio?

VoA wamesemaje kwani?
 
Kwahiyo kwa kipindi cha miaka 3, amekopa trilioni 13 tayari?

Na zinaonekana kwenye namba E kama kiashiria cha ukuaji wa uchumi kwa mujibu wa mbobevu waziri sio?

VoA wamesemaje kwani?
Hio 13tr ni hela ya ku service deni lote la taifa kwa mwaka,sio hela tuliyokopa. Iliokopwa ni mara 5 ya hio
 
Kiwango cha Fedha zinazotumika kulipa Madeni likiwemo Deni la Serikali kimeongezeka kutoka Tsh. Trilioni 10.48 za mwaka 2023/24 hadi kufikia Tsh. Trilioni 13.13 mwaka 2024/25...
Na mwakani watatumia pesa nyingi kwajili ya kampeni uchwara na kuhonga wapinzani hewa …… sasa nakubakiana na usemi wa spika mstaafu kuwa nchi itapigwa mnada
 
Ukiongeza na hii $2b za wacheza sinema mwakani itakuwa 15tr
Kilichobaki ni kukamatwa kuwa manamba tu baas. Naona deni ni kubwa
 
Attachments

  • Screenshot_20240604_173406_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20240604_173406_WhatsApp.jpg
    562.4 KB · Views: 8
Ninaomba Mhe. Waziri wa Fedha atoe taarifa kwa umma kuwa kufikia tarehe ya leo deni la Taifa ni trillioni ngapi. Je deni letu ni himilivu?.
 
Back
Top Bottom