Ghana: Kitambulisho cha Taifa kitawawezesha wananchi kusafiri bila Visa

Ghana: Kitambulisho cha Taifa kitawawezesha wananchi kusafiri bila Visa

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Makamu wa Rais wa Ghana ametangaza kutambulika ramsi kwa Kitambulisho cha Taifa cha nchi hiyo kama hati ya kusafiria kuanzia robo ya pili ya mwaka 2022.

Hatua hiyo ya Ghana inatokana na kutambuliwa kwake kama mwanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO), ambapo Kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kitatumika kama hati ya kielektroniki ya kusafiria.

Zaidi ya nusu ya wakaazi wote nchini Ghana wamepata vitambulisho vya taifa, lengo likiwa kuwasajili wananchi wengi inavyowezekana kufikia mwishoni mwa mwaka 2022.

Taifa hilo la Magharibi mwa Afrika litakuwa moja ya nchi chache duniani zinazotumia kitambulisho cha taifa kama hati ya kusafiria. Kitambulisho cha Taifa nchini humo kinatumika pia kusajili laini ya simu huku serikali ikipanga kutumia kitambulisho hicho kwa shughuli zote za manunuzi ya kidigitali.

Chanzo: 3News Ghana


Ghana-card.jpg
 
Visa au passport?
Walichofanya ni integration ya national ID na Passport kwenye card moja inayowawezesha kusafiri nchi za dunia nzima kwenye visa free countries kwa waghana hata kwetu yawezekana ni kuwaambia tu walipie extra cost kuvipata
 
Kifupi ku intergarate Nation ID na passport wamefanya kitu kikubwa sana sababu kwetu watanzania tuna vitambulisho viwili Nation ID ni kwa ajili ya ndani ya nchi tu ukisafiri kitambulisho Cha kimataifa kinakuwa passport huwezi waonyesha national ID .Ku intergrate ni kuzuri zaidi kuipa hadhi national ID kimataifa pia .Unabeba National ID tu inatosha sababu information zote za passport after all ziko kwenye National Id ni repeation of work tu NIDA wangekuwa wanamaliza kila kitu wanatoa National ID na passport kwenye kitambulisho kimoja
 
Muhuri utagongwa wapi?
Swali la msingi sana, zile Exit na Arrival.

Au labda inachomemkwa mahali kisha inasoma kwenye mashine then unajaziwa tu kama ni Umetoka ama umeingia na tarehe husika.
 
Ulaya unaweza kusafiri kwa kitambulisho cha uraia au ukaazi kwa nchi karibia zote za ulaya (UK wanahitaji viza, basi lazima upate paspoti na viza, hii ni kwa wale wenye id za ukaazi).

Ukitoka nje ya Ulaya inabidi utumie paspoti aidha ya ya kwenu au kama unayo ya Ulaya utatumia hiyo. (ukiwa na kitambulisho cha Ulaya, kuna baadhi ya NCHI nahisi kama Uturuki , Misri na hata Moroko wamekubalina na EU wawaruhusu watumie id, ila hili sijalijua vyema- Watakuja wajuzi, nitasoma zaidi).

Sasa sijui hichi cha Ghana kitatumikaje au CDAO/ ECOWAS Wanaruhusu kutumia digital id ?
Mwanzo mwema. Wacha sisi tuburure miguu tu.
 
Back
Top Bottom