Ghana kuipiga kando dola ya Marekani katika ununuzi wa mafuta

Ghana kuipiga kando dola ya Marekani katika ununuzi wa mafuta

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Nov 26, 2022 02:33 UTC

Serikali ya Ghana inaanda sera mpya ya kununua bidhaa za mafuta kwa kutumia dhahabu badala ya sarafu ya dola ya Marekani.

Makamu wa Rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia amesema katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa Facebook kuwa: Iwapo mpango huu utatekelezwa barabara kama ilivyopangwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, tutabadilisha mlingano wa mbinu za malipo na tupungeze kushuka kwa thamani ya sarafu yetu.

Mpango huo unakusudia kukabiliana na suala la kupungua kwa akiba ya sarafu za kigeni nchini humo, hatua ambayo mbali na kusababisha kuendelea kupoteza thamani sarafu ya Cedi ya Ghana, lakini pia imepelekea kuongezeka kwa gharama za maisha nchini humo.

Makamu wa Rais wa Ghana amefafanua kuwa, kutumia dhahabu kulipia bidhaa za mafuta zinazoagizwa na nchi hiyo kutazuia bei ya safaru za kigeni kuathiri bei za mafuta na bidhaa nyingine nchini humo.

Ameeleza kuwa, kwa kutumia dhahabu, wauzaji wa bidhaa za mafuta nchini humo hawatalazimika tena kuagiza bidhaa hizo kwa kutegemea kupanda na kushuka kwa sarafu ya dola.

Ghana inazalisha mafuta ghafi, lakini inategemea bidhaa za mafuta yaliyosafishwa kutoka nje, tangu kiwanda chake cha kusafisha mafuta kifungwe mwaka 2017, kutokana na mripuko.

4c0v55c47d54c52465a_800C450.jpg
 
Gad
Lkn wajipange, maana nadhani hiki ni miongoni mwa vitu vilivyompoza Gaddafi.
Gaddafi aliponzwa na kuwanyima mafuta na kutaka kuiweka kauzibe ufaransa na mchezo wake wa gold reserve za francophone Africa kupeleka France,plus kutaka kuanzisha benki ya kuzikopesha nchi za Afrika bila riba, wamba wakaona anataka kulikomboa Bara la malighafi zetu.
 
28 November 2022

Probing Ghana's Gold For Oil Barter Deal - The Probe with Emefa Apawu


Ghana has a total gold reserve of 8.7 tonnes according to the central Bank of Ghana latest report , GTG Government to Government arrangements with UAE govt for gold for oil option.. is on the table for discussions..

To explain how this move will work, JoyNews invites Dr. Mohammed Amin Adam deputy energy minister, Dr. Kwabena Donkor member - mines and energy Committee of Parliament and Dr. Sulemanu Koney CEO of Ghana chamber of mines ... and behind the scene government is engaging stake holders in oil industry .... is there enough gold reserve and does the sellers of oil in the international market ...
Source : Joy News
 
MJADALA WA BIASHARA YA DHAHABU KWA MAFUTA WAPAMBA MOTO NCHINI 🇬🇭

Mjumbe wa kamati ya migodi na nishati ya Bunge nchini Ghana, Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.

Kujaribu biashara ya mali-kwa-mali (barter trade) ya kubadilisha dhahabu kwa mafuta ya petroli / dizeli kimataifa ni dalili ya serikali kushindwa kusimamia uchumi anasisitiza mbunge na mjumbe huyo wa kamati ya bunge Dr. Kwabena Donkor ambaye aliwahi kufanya kazi ktk sekta ya petroli.


Dr. Kwabena Donkor akishiriki ndani ya mjadala exclusive wa kituo cha JoyNews amekwenda ndani zaidi kwa kuhoji ni nani anayemiliki migodi hiyo, na inajulikana ni makampuni makubwa ya kigeni hivyo watawalipa nini wenye migodi je ni kwa pesa za madafu yaani sarafu ya cedis ya Ghana au dollars za Kimarekani ambazo serikali ya Ghana haina fedha hizo za kigeni.

Anaongeza hoja Dr. Kwabena Donkor, pia kama serikali italenga kununua kwa wachimbaji wadogo wadogo itaweza kushindana na bei ya dhahabu ya soko la dunia? Maana itapelekea wachimbaji hao wadogo kutorosha dhahabu kupitia njia za panya za mipakani.

Hii ni kutokana na serikali itashindwa kuwalipa bei nzuri wachimbaji wadogo au kuwalipa kwa dollar za marekani wachimbaji wadogo kulingana na bei ya soko la dunia kwani serikali haina hifadhi ya kutosha ya fedha za kigeni.

Kimsingi katika mada hii moto ya kituo cha TV JoyNews pia mtendaji mkuu (CEO) wa chemba ya migodi ya Ghana, Dr. Sulemanu Koney naye ktk mahojiano ametoa kauli juu ya changamoto ya jinsi ya uhalisia wa uwezekano wa sera hiyo mpya ya biashara ya mali-kwa-mali kuweza kutekelezeka, kwani kuna mengi ya kuyafanya kabla ya sera hiyo kuweza kutekelezeka ingawa chemba hiyo milango yake ipo wazi kwa majadiliano na serikali ya Ghana.
Source : JoyNews
 
03 October 2022

JINAMIZI LA DHAHABU PART 1

Serikali ya Ghana yapambana na wachimbaji wadogo inaowatuhumu wanaharibu mazingira, mito ya maji safi. Hivyo serikali kuingia porini kuwasaka wachimbaji hao na kuiponda kwa nyundo mitambo kama generator, pump za maji na kuchoma moto excavators huku operation Vanguard ikizidi kuwaandama wachimbaji wadogo ...


DESTRUCTION FOR GOLD PART 1


Source : JoyNews


31 Oct 2019 — Operation VANGUARD is a Ghanaian Presidential initiative aimed at ending an illegal mining activities otherwise referred to as “galamsey ...
LAUNCH OF OPERATION VANGUARD
Ghana Ministry Of Defence
https://mod.gov.gh › 2019/10/31

17 October 2022
Destruction for Gold Part 2




Source: JoyNews
 
Petrodollar ilimuondoa Sadam Hussein na Gadaf,, so ajipange kukabiliana na fitna za hawa jamaa (USA) na wakikuona mkaidi wanakuua.
 
Ghana na Tanzania hatupishani mbali kwa rasilimali ya dhahabu ghafi iliyoko ardhini. Mwelekeo inaouchukua Ghana ni sahihi kwa wakati wote hasa ukizingatia kuwa Ghana ni mzalishaji wa dhahabu Duniani. Kuifungia nanga sarafu ya Ghana kwenye dhahabu badala ya Dollar ni mapinduzi ya meza yatakayoifanya Ghana kukaa kwenye nafasi nzuri kiuchumi.

Najiuliza sana, sijui kwenye sera zetu za fedha, BOT wanafuatilia mapinduzi haya yanayoirudisha Dunia kwenye dhahabu, thamani yake kuwa kigezo cha kubadilishana pesa za kigeni na hasa kutunza thamani ya shilling yetu?

Kwa kuwa tuna kiwanda cha kuchenjua dhahabu Mwanza, na Chunya na Geita...kuna hazina kubwa ya rasilimali hiyo, nashauri Serikali ianze kununua dhahabu yote inayozalishwa nchini na kuiweka kama akiba ya nchi badala ya kuhodhi Dollar za kimarekani.
 
Hata hapo watalia tu maana Marekani ndiyo anaongoza Kwa gold reserve 8133 tones huku Ghana akiwa na only 8.1 tonnes hapo wanatafuta kuumia zaidi.
 
Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.

Benki Kuu ya Zimbabwe yatambulisha sarafu za dhahabu kama hifadhi ya thamani huku kukiwa na mfumuko mkubwa wa bei​

Julai 28, 2022
Benki Kuu ya Zimbabwe yatambulisha sarafu za dhahabu kama hifadhi ya thamani huku kukiwa na mfumuko mkubwa wa bei
Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mangudya akionyesha sarafu mpya ya dhahabu kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, Zimbabwe, Julai 25, 2022. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)​

HARARE - Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mangudya Jumatatu wiki hii alitambulisha sarafu mpya za dhahabu ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika kama hifadhi ya thamani na kupunguza mahitaji ya dola za Marekani wakati nchi hiyo ikipambana kudhibiti mfumuko wa bei unaoongezeka.

"Benki hii leo imeingiza sokoni kundi la kwanza la sarafu 2,000 za dhahabu za Mosi-oa-Tunya (Moshi unaovuma). Mashirika ya ndani yalianza kuuza sarafu hizo za dhahabu kwa misingi ya uwakala kwa bei ya awali ya dola za Kimarekani 1,823.83 kwa kila sarafu ya dhahabu au dola za Zimbabwe 805,745.35 kwa kutumia viwango vya bei vinavyokubaliwa na mnunuzi na muuzaji vya Ijumaa (wiki iliyopita)," Mangudya amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, mji mkuu wa Zimbabwe.

Miongoni mwa sifa nyingine, sarafu hiyo ya dhahabu itakuwa na thamani ya ukwasi wa mali, thamani ya mali iliyowekwa, inaweza kutumika kama dhamana, kuuzwa na kununuliwa kwa idhini ya mmiliki.

Watu binafsi, makampuni ya ndani ikiwa ni pamoja na wawekezaji wa kitaasisi wataruhusiwa kununua sarafu hizo za dhahabu kwa fedha za ndani pamoja na fedha za kigeni, wakati wanunuzi wa kimataifa watanunua tu sarafu hizo kwa fedha za kigeni ambazo ni pamoja na dola ya Marekani, Randi ya Afrika Kusini na Pauni ya Uingereza miongoni mwa nyinginezo.

Bei ya sarafu inategemea bei ya kimataifa ya dhahabu pamoja na asilimia 5 ili kufidia gharama ya uzalishaji na usambazaji wa sarafu kwa malipo dhidi ya utoaji.

"Sarafu za dhahabu kama tulivyoshauri hapo awali, ni bidhaa mbadala nzuri ya uwekezaji kwa wale wanaotaka kuhifadhi thamani. Dhahabu ni mali ya akiba iliyo salama na ya kutegemeka duniani kote," amesema Mangudya.

Pia amesema wanunuzi binafsi na wa kitaasisi wanatakiwa kushikilia sarafu hizo kwa angalau siku 180 kabla ya kuziuza, na kuongeza kuwa mauzo yote yatakuwa chini ya Mfahamu Mteja Wako na wanunuzi wanatakiwa kutangaza chanzo cha fedha zao.

Kuanzishwa kwa sarafu hizo za dhahabu ni sehemu ya hatua za Serikali ya Zimbabwe za kukabiliana na mgogoro wa sarafu ya nchi hiyo ambao umepelekea dola ya ndani kushuka kwa kasi.

"Tunachotarajia kuona ni kwamba tunashuhudia utulivu katika kiwango cha ubadilishaji na kwahivyo kwa kuongeza athari za kupita kwenye mfumo wa bei, viwango vyote vitashuka. Kwa hivyo tunatarajia kuona utulivu wa bei katika uchumi," Mangudya amesema.

Kufuatia miaka mingi ya mfumuko mkubwa wa bei, Zimbabwe iliachana na sarafu yake ya dola Mwaka 2009, na kuamua kutumia fedha za kigeni, hasa dola ya Marekani.

Serikali ilirejesha sarafu ya ndani Mwaka 2019, lakini imepoteza thamani kwa haraka, na hivyo kurudisha kumbukumbu za kipindi cha mfumuko wa bei ambao ulipunguza akiba za watu wengi
 
Sarafu ya Khilafah ya Dhahabu na Fedha Itamaliza Mfumko
wa Bei, Unaosababishwa na Uchapishaji Pesa ili Kukidhi
Matumizi ya Serikali.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Afisi ya Habari
Wilayah
Pakistan

KUMB: 22/1443 Jumatatu, 10 Rabi’ II 1443 H 15/11/2021

Nchini Pakistan, kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2021, rasilimali iliyo katika mzunguko ilipanuka kwa bilioni 2,300, huku amana za benki ziliongezeka kwa bilioni 6,000. Rupia bilioni 8,300 zilifurika ndani ya mfumo katika miaka mitatu tu pekee, huku pato la taifa halikupanda kuendana na ongezeko hilo, kwa kiasi kikubwa likibaki palepale.

Matokeo yasiyoepukika yalikuwa ni dhoruba ya mfumko wa bei, kwani nguvu ya ununuzi ya Rupia ilipungua.

Bei za bidhaa zote zilipanda sana, na kuwanyima maskini uwezo wa kununua mahitaji ya kimsingi. Tabaka la kati sasa linazama kwenye deni, huku tabaka la chini likilazimika kuomba omba. Hata manufaa ya ongezeko la kawaida la Pato la Taifa
yalikuwa kwa kipote maalum, kutokana na mkusanyiko mkubwa wa mali katika mfumo wa kirasilimali.

Kwa hivyo, Enyi Watu wenye Nguvu, ni nani atakayejitokeza kuizika maiti hii iliyooza ya mfumo?

Katika Uislamu, hakuna dhana ya sarafu ya karatasi, isiyo na thamani ya ndani. Dinar ya dhahabu ya Khilafah na dirham ya fedha ndizo sarafu za dola. Katika Shariah dinar moja ni gramu 4.25 za dhahabu, huku dirham moja ni gramu 2.975 za fedha.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «َ
َ ْه ِل َ م َّكة
ْ َو ْز ُن َ و ْز ُن أ
وال” « َNa uzani ni uzani wa
watu wa Makkah.” (An-Nisai).

Sarafu inayotokana na msingi wa dhahabu na fedha huweka nidhamu katika matumizi ya serikali, kwani serikali haiwezi tu kuchapisha sarafu ya karatasi ili kufidia gharama.

Kwa hivyo, sarafu thabiti ya dhahabu na fedha ya Khilafah inalinda watu dhidi ya mfumko wa bei wa jumla unaoonekana katika uchumi
unaotegemea sarafu ya karatasi, isiyo na thamani ya kindani ambayo hupoteza nguvu yake ya kununua huku zaidi zikiendelea kuchapishwa.


Kupungua tu kwa usambazaji au ongezeko la mahitaji ya bidhaa ya mtu binafsi kunaweza kuongeza bei peke yake, huku dola inaweza kuchukua hatua stahiki ili kurekebisha upungufu unaotabirika wa
usambazaji, mapema kabisa, kama sehemu ya usimamizi wake wa watu.

Hadi leo, karibu dhahabu na fedha zote zinazozalishwa duniani ziko salama, imara na zinaimarika. Katika karne ya 18 na 19, licha ya kushuka kwa kasi kwa uzalishaji, sarafu ya dhahabu na fedha ilisaidia bei thabiti.

Kwa kuwa sarafu ya dhahabu na fedha ni adimu na ya thamani sana, inabaki na uwezo wake wa kuleta utulivu leo. Pia ni sarafu hii
ndiyo itakayomaliza utawala haramu ulioanzishwa wa dolari duniani.

Amerika hununua kutoka kwa masoko ya dunia kwa pesa zake za karatasi, huku dunia nzima ikilazimika kupata dolari ili kuagiza bidhaa.

Pakistan inakabiliwa na dhoruba ya mfumko wa bei, huku uchapishaji wa noti ili kukidhi matumizi ya serikali unadhoofisha sarafu mbele ya
dolari. Kisha, kushuka kwa thamani ya Rupia dhidi ya dolari huongeza gharama ya kiasi cha kila uagizaji.

Ili kukidhi upungufu wa akiba ya dolari, watawala wa Pakistan huigeukia IMF, ambayo inapanua udhibiti wake wa uchumi wa
Pakistan, kupitia mikopo ya riba, iliyo na masharti ya kukandamiza. IMF kisha huusakama uchumi wetu, na kuifanya Pakistan kuwa tegemezi kwa Magharibi na kujinyeyekesha kwake kiuchumi na kisiasa.

Kando na Khilafah kwa Njia ya Utume, ni mfumo upi mwengine unaoweza kumaliza janga la mfumko wa bei duniani?

Ikiwa tajiri wa rasilimali kuu za nishati na madini duniani, Khilafah itatumia dinar za dhahabu na dirham za fedha katika biashara ya kimataifa, kurudisha uchumi wa dunia kwenye uwanja thabiti wa sarafu ya dhahabu na fedha.

Ulimwengu umeteseka chini ya urasilimali kwa muda mrefu sana na unatazamia kurudi kwa Khilafah pamoja na Uislamu wake, kueneza ustawi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «ُ
ُ ُّده
َع
َ ْق ِس ُم َ المال وال ي
ٌ ي
َة
َ ُ كون ِ في آخِر َّ الز ِ مان َ خِليف
«ي
“Katika zama za mwisho kutakuwepo na Khalifah itaigawanya mali wala haitaiihesabu.” (Muslim). Kando na
Hizb ut Tahrir, ni uongozi gani mwengine unaoweza kutawalisha Uislamu kivitendo? Basi watu wenye nguvu nawatoe
Nussrah yao kwa Hizb ut Tahrir ili kuiregesha dunia kwenye njia iliyo sawa.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
 
Najiuliza sana, sijui kwenye sera zetu za fedha, BOT wanafuatilia mapinduzi haya yanayoirudisha Dunia kwenye dhahabu,

HALI YA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MWAKA 2021

Thamani ya mauzo ya dhahabu ilipungua kwa asilimia 7.2 na kufikia dola za Marekani milioni 2,743.1 mwaka 2021 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 2,957.5 mwaka
2020.

Hii ilitokana na kupungua kwa uzalishaji wa dhahabu ambapo uzalishaji katika migodi mikubwa ilipungua kutoka tani 44.8 mwaka 2020 hadi tani 39.7 mwaka 2021.

Hata hivyo, bei ya dhahabu katika soko la dunia iliongezeka kutoka wastani wa dola za Marekani 1,770.3 kwa wakia moja mwaka 2020 hadi wastani wa dola za Marekani
1,799.6 kwa wakia moja mwaka 2021.

Aidha, mapato ya mauzo ya madini yalichangia asilimia 53.8 ya mauzo ya bidhaa zisizo asilia na mauzo ya dhahabu yalichangia asilimia
88.4 katika mauzo ya madini mwaka 2021.

Soma zaidi : source :
Ministry of Finance and Planning
https://www.mof.go.tz › sw-1...PDF
HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2021


10 Jun 2022 — HALI YA UCHUMI WA DUNIA NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA . ... Thamani ya mauzo ya dhahabu ilipungua kwa asilimia ...
 
30 November 2022
Dar es Salaam, Tanzania

Tanzania Government debt hits Tshs. 71.98 trillion

The Central Government Debt stock of the United Republic of Tanzania stood at 71.98 trillion shillings (USD 31,188.07 million) at the end of September 2022. About Tsh. 25.54 trillion shillings equivalent to 35.5 percent is domestic debt and 46.44 trillion shillings equivalent to 64.51 percent is external debt.

The latest figures released by the Ministry of Finance shows that the debt has increased by 8.34 trillion shillings equivalent to a 13.01 percent increase compared to the period ending September 2021. This increase has been associated with government commitment to finance development projects.

The critical challenge that faces Tanzania at the moment is the dwindling of its foreign exchange reserve resulting from the shocks brought by the Ukraine-Russia war. Tanzania foreign exchange reserve by September 2022, stood at USD 4.9 billion sufficient to cover 4.2 months of import.

Due to the increased cost of import of fuel and fertilizers Tanzania’s current account has recorded a deficit of USD 1.7 billion between July 2022 and September 2022, compared to a deficit of USD 331.3 million during the same period last year.

While export of goods and services had a modest increase to USD 3.4 billion from USD 2.7 billion. Import of good and services has increased by 69 percent to USD 5 billion recorded between July 2022 and September 2022, from 2.9 billion recorded in 2021.

This means increased stress to Tanzania in meeting its debt obligation as well as its import demand.

The International Monetary Fund (IMF) report published in early August 2022 mentioned that Tanzania’s risk of external debt distress remains moderate. The IMF suggests that the government should revamp revenue mobilization and investment projects which have socio-economic payoffs in order to maintain fiscal and debt sustainability.


More info :

Mobilizing domestic resources, such as taxes, can help countries finance their own development and lessen their dependence on foreign aid. At $5.5 trillion annually, DRM makes up the largest source of total resources available to developing countries .....https://www.mcc.gov/initiatives/initiative/domestic-resource-mobilization
 
Back
Top Bottom