Ghana Kutolewa Kombe la Dunia Mapema

Ghana Kutolewa Kombe la Dunia Mapema

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Baadhi ya mashabiki wa Afrika tulikuwa na matumaini na Ghana kufika mbali lakini mambo hayakwenda kama yalivyotarajiwa.

Binafsi, naona sababu ya Ghana kutolewa mapema ni Kocha wao kushindwa kupanga kikosi vizuri tangu mechi ya kwanza, na kuwang'ang'nia kina Andre na Jordan Ayew na wakongwe wengine wakati wameishachoka.

Katika mechi ya Ureno, kocha alimuingiza Jordan na kujaribu kupiga chenga ikanaswa na Ureno wakapata goli. Hivyo hivyo, katika mechi na Uruguay, Jordan alipiga chenga ikanaswa, Uruguay wakapata goli. Andre yeye akakosa penati.

Ukichunguza, unaona Ghana kuna majina yanang'ang'aniwa kuweno kikosini ila umri umeenda.

Tumu za Afrika zinahitaji kujiimarisha na kuwatumia wachezaji vijana kama wanataka kufanya vizuri katika mashindano makubwa kama kombe la Dunia.

Kule kombe la Dunia inahitajika kuwa na wachezani wepesi, na wenye pumzi ya kutosha ili kupanda na kushuka kwa kasi.

Ukiwa na wachezaji wazee utashinda kwa tabu sana.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kocha na wachezaji wa Ghana wamezingua Sana, wameshindwa gundua na kutumia udhaifu wa Uruguay kupata ushindi. Uruguay walikuwa na Tatizo kubwa Sana la kuokoa mipira ya cross, cross mbili ambazo Ghana walipiga zilileta kizaazaa golini. Lakini Ghana walikuwa hawapigi cross wanataka kupasua Kati Kati ya goli hapo ndipo walipofeli. Kwa mfano mechi ya Ghana na S .Korea, Korea waligundua udhaifu wa Ghana kwenye kuokoa cross Kama utakumbuka S Korea walikuwa wanamwaga cross golini kwa Ghana Kila Mpira wanaoupata na Hali ilikuwa tete dakika za mwisho langoni mwa Ghana
 
Baadhi ya mashabiki wa Afrika tulikuwa na matumaini na Ghana kufika mbali lakini mambo hayakwenda kama yalivyotarajiwa.

Binafsi, naona sababu ya Ghana kutolewa mapema ni Kocha wao kushindwa kupanga kikosi vizuri tangu mechi ya kwanza, na kuwang'ang'nia kina Andre na Jordan Ayew na wakongwe wengine wakati wameishachoka.

Katika mechi ya Ureno, kocha alimuingiza Jordan na kujaribu kupiga chenga ikanaswa na Ureno wakapata goli. Hivyo hivyo, katika mechi na Uruguay, Jordan alipiga chenga ikanaswa, Uruguay wakapata goli. Andre yeye akakosa penati.

Ukichunguza, unaona Ghana kuna majina yanang'ang'aniwa kuweno kikosini ila umri umeenda.

Tumu za Afrika zinahitaji kujiimarisha na kuwatumia wachezaji vijana kama wanataka kufanya vizuri katika mashindano makubwa kama kombe la Dunia.

Kule kombe la Dunia inahitajika kuwa na wachezani wepesi, na wenye pumzi ya kutosha ili kupanda na kushuka kwa kasi.

Ukiwa na wachezaji wazee utashinda kwa tabu sana.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Tatizo la ghana ni defence. Yule sijui Salisou na Daniel Amartey hamna Kila kitu. Angalia magoli waliyofungwa na Korea kusini. Game tatu wameruhusu gori 7
 
Yaani goal la kwanza tu nikajiambia hapa Ghana wanakula 3-0, yaani wanaingia uwanjana na mental ya south Africa hapo ndipo wakadhani watatoboa ukuta.

Alafu mwishoni wanajipongeza bora tumekosa wote, bladfakeni!.
 
Namkubali sana Luis van Gaal yule jamaa anapanga wachezaji wake kwa takwimu na anaandika kila kitu.
 
Team za afrika wakiwa kwenye mechi muhimu huwa wana panick
Ile mechi ghana alikuwa anatakiwa
Shinda.....

Ova
 
Back
Top Bottom