Serikali ya Ghana imetangaza kuwahamisha raia wake 300 kutoka Afrika Kusini, kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya chuki dhidi ya wageni nchini humo katika wiki za hivi karibuni.
Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa X, Waziri wa Mambo ya Nje, Samuel Okudzeto Ablakwa, alisema Rais John Dramani Mahama ameidhinisha mpango huo.
Hatua hii imekuja baada ya maandamano dhidi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini, pamoja na madai ya mashambulizi na vitisho dhidi ya raia wa mataifa mengine ya Afrika.
Nigeria na Ghana zote zimeelezea wasiwasi wao kuhusu hali hiyo. Hata hivyo, serikali ya Afrika Kusini imekanusha madai yote ya chuki dhidi ya wageni (xenophobia).
Msemaji Magwenya alisema kuwa Afrika inahitaji kutatua migogoro, ukosefu wa utulivu, na visa vya "utawala mbaya" ambavyo ndivyo vinavyochochea mawimbi ya uhamiaji barani kote.
Mwishoni mwa mwezi Aprili 2026, serikali ya Accra ilimwita balozi wa Afrika Kusini kulalamikia matukio kadhaa ya chuki dhidi ya wageni yaliyokuwa yakiwalenga Waghana.
Source: TRT AFRIKA