Ghana na Ivory Coast wapokea chanjo za bure

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Nchi jirani za Afrika ya Magharibi za Ghana na Ivory Coast wiki hii zimepokea mzigo wa chanjo za bure aina ya Covax na kuanza kuwachanja raia zao.

Wa mwanzo kuonesha mfano wa kupokea chanjo hizo alikuwa ni raisi Nana Akufo-Addo Ghana. Mara baada ya kuchanjwa raisi hiyo alisema anataka aoneshe mfano kwa wengine kwamba chanjo hiyo ya Covax ni salama.

1614693512425.png
 
Hata wawe wanatoa na pesa, hawanipi hiyo chanjo zao. Waanze leta chanjo za magonjwa mengine kwanza yaliyo korofi hapa african
 
hivi haya ndo yale mataifa maskini,ambayo walisema yatawezeshwa kupata chanjo bule au.[emoji848].
 
Mbona kavaa hilo dude puani kama kashapokea chanjo?

Au picha haina uhusiano na upokeaji chanjo?
Ni ya siku hiyo hiyo.Bado hajaamini. Mwwngalie macho yake alivyoyatoa.Unamuhisi hivi hivi hapati oksijen ya kutosha.
 
Kwa kweli sijui ni nani lakini wamejificha sana kwenye kicha cha Who.Inaonekana hii chanjo imeelekezwa zaidi Afrika.
Pengine hata majaribio yao ya mwanzo yanaanzia huku.
Nadhani COVAX siyo chanjo yenyewe bali ni mpango wa upatikanaji wa chanjo kwa usawa. Yaani mashirika na mataifa duniani wameanzisha huu mpango ili kuhakikisha nchi zote zinakuwa na nafasi ya kupata chanjo kwa urahisi na kwa unafuu.

Kwa mfano, Ghana wao chanjo walizopokea ni AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech

Hiyo chanjo ni ya lazima. Hakuna kukwepa.

Chanjo ya surua, pepo punda, polio, ukoma, kifafa, circle cell, sijui magonjwa gani zinazotengenezwa na wazungu hazina shida ila ya corona ndio iwe na shida kuja kuwamaliza waafrika, wazungu walishindwa kutumaliza kwenye hizo chanjo nyingine ambazo zimetusaidia miongo na miongo?

Leo hii zadi ya 90% ya watanzania tuna chanjo ya ndui hata sasa hivi watoto wanachomwa ndui na chanjo hiyo inatengenezwa na wazungu, walishindwa kutumaliza tukiwa vichanga na hizo chanjo waje kutumaliza leo na corona?

Mimi binafsi na familia yangu tunaisubiri hiyo chanjo kwa ham sana.
 
Mbona kavaa hilo dude puani kama kashapokea chanjo?

Au picha haina uhusiano na upokeaji chanjo?
Kuvaa barakoa bado ni mandatory, nina wasiwasi inaweza kuwa compulsory kwa healthcare workers wakiwa kazini.
 
Hiyo chanjo ni ya lazima. Hakuna kukwepa.

Chanjo ya surua, pepo punda, polio, ukoma, kifafa, circle cell, sijui magonjwa gani zinazotengenezwa na wazungu hazina shida ila ya corona ndio iwe na shida kuja kuwamaliza waafrika, wazungu walishindwa kutumaliza kwenye hizo chanjo nyingine ambazo zimetusaidia miongo na miongo?

Leo hii zadi ya 90% ya watanzania tuna chanjo ya ndui hata sasa hivi watoto wanachomwa ndui na chanjo hiyo inatengenezwa na wazungu, walishindwa kutumaliza tukiwa vichanga na hizo chanjo waje kutumaliza leo na corona?

Mimi binafsi na familia yangu tunaisubiri hiyo chanjo kwa ham sana.
Hilo la kuwamaliza waafrika si hoja ya msingi.Na pia usishangae ikawa mioyoni mwa baadhi ya wazungu hivi leo hata kama hapo juzi hawakuwa na dhana hiyo kwani akili za binadamu kila siku zinabadilika kuelekea mawazo ya kishetani. Muangalie mtu kama Trump na wafuasi wake wewe mshamba wa Tanzania una uhakika gani kuwa hawawezi kutafuta chanjo ya kuwamaliza watu weusi baada ya kuwa imekuwa shida kufanya hivyo kwa njia za kawaida na kwa nyanya ya siasa.Kila siku wanadhihirisha kukereka kwao kwanini Mungu hakuumba watu wote weupe kama wao.
Lakini kubwa zaidi ukiondoa dhana hiyo ni biashara na kujitajirisha.Wako wanaotangaza chanjo haraka haraka ili na wao kwa kujua ukubwa wa soko waweze kupata nafasi ya kuinuka kiuchumi.Nchi za namna hiyo ziko nyingi huku Ulaya na walengwa wakubwa ni huko Afrika.Hawajali kama watu watakufa au watakuwa matasa muhimu kwao kuingiza pochi kibindoni mapema.Kipi kitakushangaza katika hili wakati kuna madawa kibao tena maarufu kama aspirini na panadoli na chlorokwin,kila siku wanakuja na madai mapya ya kutokufaa kwake wakati tumeshatumia miaka mingi.Ajabu iko wapi kuwa chanjo za corona ni mpya sana kujua matokeo yake hata ya miaka 2 ijayo.
Kule Marekani kanila katoliki jimbo fulani wameshakataza watu wao kuchanjwa hasa kwa kutumia chanjo za Johnson ambazo zinatengenezwa kwa vimelea vya mimba zilizofuia tumboni.
 
Jifunze kuandika vizuri kwanza ndio uje tujadiliane.
 
Dalili huna jibu.Usingekosa kudondoa hapa na pale ukapata cha kuandika hata kama sikuandika kwa lugha uliyoizoea wewe. Mbona mimi hata ukiandika kwa lafdh ya kisukuma nakufahamu.
 
Baada ya chanjo huenda mahanithi yakaongezeka na uzazi ukapungua kabisa afrika
 
Attachments

  • ISRAEL SECRET REC.jpg
    ISRAEL SECRET REC.jpg
    17.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom