Ghana, Senegal zafuzu World Cup 2022; Misri na Nigeria zatupwa nje

Ghana, Senegal zafuzu World Cup 2022; Misri na Nigeria zatupwa nje

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
GHANA YAFUZU WORLD CUP 2022

Timu ya taifa ya Ghana imefanikiwa kufuzu kwenda kucheza World Cup 2022 licha ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi Nigeria katika kipute kilichopigwa Nchini Nigeria.

Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0, kwa matokeo ya 1-1, hivyo Ghana imepata faida ya bao la ugenini.

SENEGAL YAFUZU KWA PENATI
Senegal imefuzu kucheza Kombe la Dunia 2022 kwa njia ya penati 3-1 dhidi ya Misri.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ulipigwa kwenye Uwanja wa Cairo International ambapo Misri ilishinda kwa bao 1-0 mnamo Machi 25, 2022.

Mchezo huo wa pili ulipigwa Machi 29, 2022 kwenye Uwanja wa Baba Yara Jijini Diamniadio Olympic chini ya mwamuzi Mustapha Ghorbal wa Algeria, matokeo yalikuwa bao 1-0 kwa Senegal kushinda, hivyo mwamuzi kumua mshindi apatikane kwa matuta.

Mshambuliaji na nahodha wa Misri, Mohamed Salah alikosa penati yake ikiwa ni ya kwanza kwa timu yake, wakati Sadio Mane alifunga penati ya mwisho na kuipeleka timu yake Qatar.

836947a9-2ae2-4bfe-a11e-15aaf65cd1a6.jpg
 
Daah, Senegal wame prove kuwa ni wababe wa Misri kwani hata ktk AFCON iliyoisha juzi waliwatandika ktk fainali na kubeba ndonga.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Senegal safi, ila nafasi za wazi wanazokosa hizi mmmh,wasiporekebisha hilo hali yao itakuwa mbaya huko world cup.
 
Senegal safi, ila nafasi za wazi wanazokosa hizi mmmh,wasiporekebisha hilo hali yao itakuwa mbaya huko world cup.
World cup wazungu Wanapendelewa na marefaa[emoji35][emoji35]
 
GHANA YAFUZU WORLD CUP 2022

Timu ya taifa ya Ghana imefanikiwa kufuzu kwenda kucheza World Cup 2022 licha ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi Nigeria katika kipute kilichopigwa Nchini Nigeria.

Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0, kwa matokeo ya 1-1, hivyo Ghana imepata faida ya bao la ugenini.

SENEGAL YAFUZU KWA PENATI
Senegal imefuzu kucheza Kombe la Dunia 2022 kwa njia ya penati 3-1 dhidi ya Misri.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ulipigwa kwenye Uwanja wa Cairo International ambapo Misri ilishinda kwa bao 1-0 mnamo Machi 25, 2022.

Mchezo huo wa pili ulipigwa Machi 29, 2022 kwenye Uwanja wa Baba Yara Jijini Diamniadio Olympic chini ya mwamuzi Mustapha Ghorbal wa Algeria, matokeo yalikuwa bao 1-0 kwa Senegal kushinda, hivyo mwamuzi kumua mshindi apatikane kwa matuta.

Mshambuliaji na nahodha wa Misri, Mohamed Salah alikosa penati yake ikiwa ni ya kwanza kwa timu yake, wakati Sadio Mane alifunga penati ya mwisho na kuipeleka timu yake Qatar.

View attachment 2168648
Hongera zao Senegal and Ghana
 
Morocco pia wamefuzu baada ya kuicharaza Congo DR 4-1 (5-2 Aggr); Tunisia pia wamefuzu kwa (1-0 Aggr) dhidi ya Mali; Cameroon nao wamefuzu dhidi ya Algeria kwa ushindi wa (3-2 Aggr) wakibebwa na goli la ugenini.

Hivyo zilizofuzu ni:

1. Ghana
2. Morocco
3. Senegal
4. Tunisia
5. Cameroon
 
Hapo angalau kidogo muwakilishi mzuri ni senegal tu hawa wengine sana sana waarabu wanaenda Kuuza sura tu
 
Senegal na Morocco wana uhakika wa kutuwakilisha vizur
 
Nigeria kulinuka uwanjani
Mashabiki hawakuelewa

Ova
 
Senegal walivunja rekodi kwa fitina! Maana zile tochi kwa wachezaji wa Misri zilikuwa too much!

Na uzuri wao wenyewe ndiyo waanzilishi wa huo upuuzi, basi limekuwa ni jambo jema sana. Maana wamevuna walichopanda.
 
Black Stars wanaenda kuuza sura tu Qatar. Wameunga unga sana tangia group stage
World Cup ya 2006 pia walikuwa hivyo hivyo waliposhiriki kwa mara ya kwanza lakini walifika kwenye round of 16 na kutolewa na Ujerumani.

Kwenye mpira wakati fulani timu inabadilika ghafla kutokana na muda na kama wana great deal of concentration at the material time.
 
World Cup ya 2006 pia walikuwa hivyo hivyo waliposhiriki kwa mara ya kwanza lakini walifika kwenye round of 16 na kutolewa na Ujerumani[/red].

Kwenye mpira wakati fulani timu inabadilika ghafla kutokana na muda na kama wana great deal of concentration at the material time.

Uruguay
 
Back
Top Bottom