Ghana yakataa Msaada wa Marekani wa dola Milioni 109 za ufadhili wa Afya

Ghana yakataa Msaada wa Marekani wa dola Milioni 109 za ufadhili wa Afya

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Ghana imejitoa kwenye mazungumzo ya mkataba wa msaada wa miaka mingi kutoka Marekani. Hatua hii imekuja baada ya Washington kudai kupewa ruhusa ya kupata taarifa binafsi za raia wa nchi hiyo, kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na serikali ya taifa hilo la Afrika Magharibi kilichozungumza shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mazungumzo hayo yalikwama baada ya serikali ya Ghana kukataa ombi hilo. Inasemekana kuwa baada ya Ghana kukataa, upande wa Marekani ulionyesha "uadui" na kuanza kuongeza shinikizo zaidi.

Inaripotiwa kuwa msaada huo ulikuwa na thamani ya dola milioni 109 kwa kipindi cha miaka mitano, na kilitarajiwa kufadhili sekta ya afya. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imekataa kuingia ndani zaidi kuhusu undani wa mazungumzo hayo, lakini imeeleza kuwa fedha hizo zingesaidia katika mapambano dhidi ya UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu na Magonjwa mengine ya kuambukiza

Kuvunjika kwa mazungumzo haya kumetokea wakati huu ambapo Washington inasaini mikataba mipya ya misaada ya afya barani Afrika chini ya mkakati wake wa "America First Global Health Strategy," kufuatia kuvunjwa kwa shirika la USAID

Ghana si nchi ya kwanza kuchukua hatua hii; Zimbabwe na Zambia tayari zimeshakataa mapendekezo kama hayo. Nchini Kenya, makubaliano kama hayo yalisimamishwa na mahakama kutokana na hofu hiyohiyo ya usalama wa taarifa za raia.

Licha ya kuwepo kwa dalili za kuimarika kwa uhusiano kati ya Accra na Washington hivi karibuni, Ghana imeamua kusitisha mazungumzo hayo kabisa. Kwa upande wao, Marekani imesema bado ina nia ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

1777447822914.png

Soma pia
 
Ingekuwa kule kijijini kwetu Sungangwanda,uongozi ungekubali ombi la Marekani.Kama kuhudumia tu raia wake kwenye balozi nje ya nchi na kuwasaidia changamoto zao ni shida,je,wangeshindwa kuwauza kwa mataifa?
 
Huku Malawi mbona hatujasikia wao wakikataa huo mkopo !! Itakuwa wameshatuuza raia wao Tayari sio bure
 
Kweli Trump ni ni wa moto, hapo amesave pesa nyingi sana za wamerekani ambazo zingepotea tu kwa kisiongizio cha ufadhiri, wakati kumbe wanachakata takwimu na upuuzi mwingi. Amekinukisha and the results has been going on his side, ni mfano wa kuigwa hata kwetu, kuwa na ajenda na itimize ikibidi hata kwa vitisho ila kwa kumaanisha.
 
Yule mpumbavu wa Tz pamoja na jopo la vilaza wenzie, watakua kimbelembele kukubali mapendekezo ya aina hiyo, sijui kwanini hii serikali malaya ya huyu Rais imekuwa ya hovyo ktk kila jambo.

Hakuna mahala tumewai kuona hii serikali ikitilia shaka baadhi ya mikataba au hata madeal machafu, wao kila jambo ni twende mbele chamsingi wapate pesa
 
Trump Yuko sahihi kabisa ✅.

USA wanataka kufanya monitoring ya fedha wanazotoa, sio kutapanya TU pesa ovyo.

Sasa taarifa za wenye ukimwi , USA atazipeleka wapi kwa mfano ? Labda kuwataja viongozi wa CCM wenye ukimwi ?.

Badala ya taarifa kubaki wizarani pekee, Sasa Zina kuwa accessable na marekani Moja kwa Moja , Yan hakuna janja janja.
 
Back
Top Bottom