Gharama kiasi gani kulisha kuku 500 wa nyama kwa Dar es Salaam mpaka kuuza?

TUPAMBANE

Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
62
Reaction score
88
Habari wadau wa ufugaji

Naomba kujua gharama za kufuga kuku wa nyama idadi 500 kuanzia siku ya kwanza mpaka hadi kufikia mwezi kwa mtu ambaye anafanya shughuli hizo au alishawahi kufanya kwakipindi kisichopungua miezi 8 iliyopita.
 
Du nikipiga napata ju nikipiga napata jumla 3,440,000 sasa nikijaribu kuangalia bei wanaouza ni 5500 au 6000 sasa nikipigia hesabu ya 6000*450=2,700,000 sasa hapo ndipo ninapopata wasiwasi na data zako ziko sahihi hapo bei nimechukua ya 6000 na nikaweka kuku 450 maana sidhani kama wote 500 wanaweza wakapona wote
 
Kuna Mkuu mmoja humu anaitwa Jembekillo ni mtaalamu wa hizi mambo. Mimi alinisaidia sana ila kuna sehemu mambo fulan yakakwama sikumalizana nae. Jaribu kumcheki
 
Rudia hesabu vizuri mkuu.matumizi hayazidi 2500000 hayo
 
Mkuu hawa wadudu nawafuga nawajua vizuri sana,hapo kwanza situmii dawa..ni chanjo tu week mbili za mwanzo.na kuku kumi hawafiki kwenye vifo.
 
Broiler 300 gharama ni 1.2M - 1.3M kwa week 4.

Hiyo ni gharama ya kila kitu. Kuwanunua, madawa na chanjo, chakula, umeme na mkaa, maranda, vitamins na booster. N.k.

Kwa 500 piga mahesabu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…