Gharama mpya za Bajaj zinaumiza sana!

Gharama mpya za Bajaj zinaumiza sana!

mrlonely98

Member
Joined
Nov 6, 2009
Posts
95
Reaction score
19
Asalaam wana jamii,

Mimi nafanya kazi ya bajaj, hua nanunua na kuziweka kwenye mkataba lakini mwaka moja sasa bajaj kimekua zina panda bei vibaja mno

Mwaka jana nilikua nanunua kwa bei ya 8.1 Million lakini Jan-24 nilipoenda kunnunua tena bei zilipanda hadi 8.6m lakini sasa kiznauzwa 9.7m na wanasema hiyo ni discounted price na bei halisi ni 10,193,000.

Jamani kwa bei hii si tutakua tuna waumiza ma dereva?

Naelewa kama vitu haviezi kua bei zile zile lakini vitu vina panda vipi asilimia 25% kwa muda mfupi?

Mambo yakiendelea hivi itabidi niwache biashara hii ni fikirie mambo mengine.
 
Ni zile za mafuta wameziwekea mtungi wa gesi kama magari wanavyoyafanyia.

Zinakua na ulaji mzuri zaidi.
Naziona kwa wingi sana njiani kwa sasa.
Yes gharama za nishati zitakua almost nusu ya unazotumia kwenye petrol, hivyo hata hesabu inakuwa kubwa.
Hesabu inasimamia ngapi kwa siku?
 
Mkuu biashara ya usafirishaji ni moja ya biashara inayolipa sana hasa kwa Dar es Salaam. Endapo utapata Bajaji mpya ukafunga mfumo wa gesi ukashika usukani wewe mwenyewe ni biashara nzuri sana ukiwa makini.
Bajaji na Pikipiki nishasema iyo biashara siwezi. Imagine Mil 10 hadi irudi.

Labda ununue used nazo naona hazigusiki.
 
Back
Top Bottom