Gharama na utaratibu wa ujenzi wa nyumba ya kuishi - (residencial)

dotnet

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2013
Posts
393
Reaction score
153
Habari zenu ndugu,

Naomba kuuliza kwa mtu mwenye uzoefu na masuala ya ujenzi kwa hapa Dar es Salaam au hata sehemu nyingine za nchi hii. Kwa mtu aliyenunua "shamba" kwa kuuziana na mtu kupitia serikali ya kijiji, anatakiwa kufuata taratibu gani kabla hajaanza kujenga nyumba yake hapo aliponunua ili kuepuka kujenga mahali ambapo huenda serikali imepahifadhi kwa matumizi mengine yasiyo ya makazi kama barabara au shule?

Pili, kama mtu ana mil. 60 TZS, anaweza kujenga nyumba ya kuishi "ya kawaida" ikakamilika?

Nawasilisha.
 
Aisee we ni nouma yaani una milioni sitini halafu unakuja kuonyesha dolidoli hapa mie nilifikiri una milioni mbili au milioni sita? Hiyo nyumba ya kawaida ya hiyo gharama ikoje? Mbona unajenga na chenji inabaki labda kama unataka jenga gorofa au bangaloo .
 
Mkuu moja ni "Residential" na si "Residencial".
Pili, kwa sejemu husika mfano manispaa au jiji, ni vyema kuwaita wapimaji, kupitia ramani ya jiji/mji husika ili kujua nini kiko wapi na pengine kutambua sehemu kutakazokuwa na huduma muhimu za kijamii.

Tatu, kwa milioni 60, unajenga nyumba nzuri na iliyokamilika hapa hapa Dar es Salaam.
 
Sijawahi kujenga ndugu hivyo sijui lolote hapa nilipo. Mawazo au ushauri wako muhimu sana. Kuna kitu kinaitwa BOQ una idea nacho?
 
Mkuu moja ni "Residential" na si "Residencial".
Pili, kwa sejemu husika mfano manispaa au jiji, ni vyema kuwaita wapimaji, kupitia ramani ya jiji/mji husika ili kujua nini kiko wapi na pengine kutambua sehemu kutakazokuwa na huduma muhimu za kijamii.

Tatu, kwa milioni 60, unajenga nyumba nzuri na iliyokamilika hapa hapa Dar es Salaam.

Asante sana ndugu
 
Naongezea kwa hippo hapo juu! Gharama za ujenzi per square metre laki nne - laki 600 unaweza kukokotoa myumba ya aina gani unayotaka
 
mmmmhhhh!!!!hilo si bonge la jumba tena mbili za nguvuuu duu
ila km za kule kwa mfuga mbwa mtaa mzima
 
Plan yangu ni nyumba ya vyumba vitatu vya kulala kimojawapo kikiwa master bedroom, sitting room, dining na kitchen. Basic yaani.

Sasa mtu ukisema unajenga mbili inakuwa shida kuelewa, plot tayari ninayo. So question iko kwenye beginning from scratch yaani hata ramani sina na nadhani ningepata ramani na BOQ ingekuwa ideal.
 
Mkuu moja ni "Residential" na si "Residencial".
Pili, kwa sejemu husika mfano manispaa au jiji, ni vyema kuwaita wapimaji, kupitia ramani ya jiji/mji husika ili kujua nini kiko wapi na pengine kutambua sehemu kutakazokuwa na huduma muhimu za kijamii.

Tatu, kwa milioni 60, unajenga nyumba nzuri na iliyokamilika hapa hapa Dar es Salaam.

Ni sehemu husika, sio sejemu mkuu
 
Una 60m na unataka yote uzamishe kwenye nyumba ya kuishi! Watanzania acheni uoga wa maisha,why can't you take a little risk and investment part of it? If
you managed to make that much money na shamba tayari unalo you can use that or part of it to make more money labda kama ni pesa ya urithi.
 
Raha ya kuchukua risk ni endapo una kwako kwa kuishi,hata mambo yakienda vibaya mwisho wa siku una sehemu ya kulaza ubavu bila bugudha ya kodi

Halafu pia una uhakika gani kama haja wekeza? Kila mtu ana mipango Yake mkuu,na hukana asiyejua faida za kuwekeza

Mkuu dotnet (bila shaka wewe ni programer mwenzangu kwa hili jina lako),kwanza tafuta surveyor aende akuchukue coordinates za eneo lako, then ata zipeleka ardhi ambapo watacheki kama kwenye hilo eneo kuna mchoro wa mipango miji.

Kama hakuna mchoro hapo itabidi uanze mchakato wa kuchora ambayo ni Gharama sana na inategemea na eneo lilipo maana manispaa inaweza isipitishe mchoro.

Mara nyingi manispaa huwa wanapitisha mchoro ambao ni wa eneo kubwa kuanzia ekari 50 au at least Ekari 10,ndio maana watu huwa wanajiunga wawe wengi ndio wanaanza kupima.

Eneo likishakuwa na mchoro wa mipango miji then ndio mchakato wa kupima ili upate hati ndio unaanza.
 
Last edited by a moderator:
Kama una ramani tayari ni pm. Kama huna niambie. Nyumba inategemeana na mahitaji yako. Niambie unataka vyumba vingapi? Ni pm Mimi ni mtaalamu kwenye hiyo fani.
 
Tafuta saveya wachukue vipimo gprs wakaangalie eneo limetengewa nini....usijejenga kwenye hifadhi ya barabara buuuure

Hakafu ml 60 ukiisimamia nyumba mbona inaisha??
 
Una 60m na unataka yote uzamishe kwenye nyumba ya kuishi! Watanzania acheni uoga wa maisha,why can't you take a little risk and investment part of it? If
you managed to make that much money na shamba tayari unalo you can use that or part of it to make more money labda kama ni pesa ya urithi.

Ushauri wako mzuri. Lakini kila kitu kina plan na nyakati zake. Kumbuka maisha bora hayapimwi kwa kuwa na pesa nyingi au miradi mingi inayotengeneza faida kama pesa au faida hiyo haiwi converted ku-reflect ubora wa maisha yako na ya jamii yako. Ishi nyumba bora, kula lishe bora, vaa mavazi bora na uishi na watu kwa ubora (upendo na ustaarab na kusaidia wengine kadri unavyoweza). Kwangu mimi hayo ndio maisha. Ila kuhangaika na maisha wee then unakuja kujenga umezeeka au unajenga nyumba isiyo bora ili pesa nyingine uwezeke Nafikiria tofauti.

Hata hivyo, kila mmoja ana plan zake, ushauri wako ni mzuri na naulibali. Asante sana.
 
Back
Top Bottom