GE2025 Gharama ni nafuu zaidi kubadili utawala kabla kuliko baada ya Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
22,898
Reaction score
33,309
Nalenga gharama za uhai, maisha, damu na mali za waTanzania. kutishiwa maisha kwa watanzania. Sote tunaelewa ilivyo kawaida siku hizi; Watanzania kutishiwa maisha yao wanapotaka kudai haki zao kwa kufanya maandamano ya amani.

Polisi ndio wako mstari wa mbele kutishia uhai wa watu endapo watafanya maandamano. Wanasiasa na viongozi wa serikali wao wanadai polisi na jeshi watafanya usafi. Hii yote ni kuwanyima waTanzania haki yao ya kuandamana kwa amani.

Na tumeona, wananchi wanapojitahidi kutimiza haki yao ya kuandamana, malipo yake ni kuumizwa na wengine kuuliwa. Hii ni gharama kubwa ambayo hulipwa hata bila ya mafanikio ya hicho walichokuwa wakikidai.

Matokeo ya mtindo huu yamekuwa ni kwa waTanzania sasa kuambiwa ni waoga, wapumbavu, makondoo wanaposhindwa kushiriki kwenye maandamano

Hao wanao wadhalilisha na kuwadharau waTanzania wanasahau kwamba kwenda kujitupa mbele ya mitutu ya bunduki, si ujasiri, bali ni upumbavu. Hakuna ujasiri wa kwenda kujitoa mhanga huku ukijuwa matokeo yake hayabadili chochote. Kutumia akili na ujanja, ni kumpumbaza mwenye mitutu, na kumlia hatua kwa kuchagua wakati sahihi wa kumkabili ipasavyo.

Kwa hiyo basi, fursa hii ya kipekee kabisa inayojitokeza wakati huu Oktoba hii ni wakati sahihi kabisa wa kumkabili adui. Huu ni wakati asioweza kuitumia mititu ya bunduki kuwafyeka waTanzania.

Kwa vile watawala wamekataa kuruhusu haki katika kupatikana viongozi wa kuiongoza nchi hii kwa njia za haki; na wao kufanya kila aina za hila ili wabaki madarakani kwa nguvu, itawalazimu waTanzania wafanye juhudi zote ziwezekanazo kuwaondoa madarakani hawa watawala..

Mipango yao ya hila sote tunazifahamu; lakini la muhimu zaidi ni kukataa kufanya marekebisho ya msingi ili wananchi waweze kuwachagua viongozi wao kwa uhuru na haki. Wamefanya kila njia kuhakikisha ni wao pekee ndio watakao endelea kutawala nchi hii kwa nguvu.. Wamekwisa jihakikishia kuendelea kutawala miaka mitano mingine; kinacho fanyika sasa hivi ni kiini macho tu cha kuhadaa watu na kuhalalisha uovu wao.

Ni muhimu sana kwa waTanzania kuzuia njama hizi wakati huu kwa kuzuia unaoitwa uchaguzi usifanyike hiyo tarehe 29 Oktoba, na hata kabla ya siku hiyo kwa kutumia mbinu mbalimbali zitakazo buniwa.

Siku hiyo ya 29 Oktoba, ni muhimu mambo mawili yafanyike:
1. WaTanzania wasijitokeze kwenda kwenye vituo vya kupigia kura. Kwa mTanzania yeyote anayelitakia taifa hili mema, siku hiyo asijitokeze kwenda kupiga kura. Kufanya hivyo ni kukubali kuendelea kuwa watwana wa watawala hawa. Usipo kwenda kupiga kura, hakuna polisi yeyote atakayekufuata nyumbani na mitutu ya bunduki kukuamrisha ukapige kura. Hata hao viongozi wa mitaa wakifika nyumbani kwako, wafungie nje, wasiingie nyumbani mwako.

2. Ni muhimu kushiriki katika maandamano ya nchi nzima; kupinga uhalalishaji wa jambo ambalo ni haramu.
Umuhimu wa kuungana na waTanzania wengine kwenye maandamano ni silaha ya uingi wetu kwenye maandamano hayo. Mitutu ya akina Jumanne Mulilo; ACP Awadh na wengineo haina kazi kwenye umma wa waTanzania wa aina hiyo; licha ya kwamba hakuna mitutu ya kutosha kuwakabili waTanzania hawa nchi nzima.

Kwa hiyo hii itakuwa imeepusha uhai na damu ya waTanzania kumwagwa hovyo na hawa watawala.

Kwa maana hiyo, gharama ya kazi hii itakuwa ni nafuu zaidi kuliko gharama wanayoweza kuilipa waTanzania baada ya hawa watawala kujihalalisha kuwa kwenye madaraka wakitumia njia haramu.

MTanzania, popote utakapokuwa, shiriki kuokoa taifa letu kutoka kwenye mikono ya watu waovu hawa.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Oktoba 29 Tunatiki na hamna ka kufanya, jiandae na maumivu hadi 2030
 
Polisi wamenunuliwa magari ya kudhibiti raia wema, aisee huwaambii kitu. Wanatamani hiyo siku ifike haraka ili wamfurahishe mtawala.
 
1. WaTanzania wasijitokeze kwenda kwenye vituo vya kupigia kura. Kwa mTanzania yeyote anayelitakia taifa hili mema, siku hiyo asijitokeze kwenda kupiga kura. Kufanya hivyo ni kukubali kuendelea kuwa watwana wa watawala hawa. Usipo kwenda kupiga kura, hakuna polisi yeyote atakayekufuata nyumbani na mitutu ya bunduki kukuamrisha ukapige kura. Hata hao viongozi wa mitaa wakifika nyumbani kwako, wafungie nje, wasiingie nyumbani mwako.
Sahau kuhusu hili.
 
2. Ni muhimu kushiriki katika maandamano ya nchi nzima; kupinga uhalalishaji wa jambo ambalo ni haramu.
Umuhimu wa kuungana na waTanzania wengine kwenye maandamano ni silaha ya uingi wetu kwenye maandamano hayo. Mitutu ya akina Jumanne Mulilo; ACP Awadh na wengineo haina kazi kwenye umma wa waTanzania wa aina hiyo; licha ya kwamba hakuna mitutu ya kutosha kuwakabili waTanzania hawa nchi nzima.

Kwa hiyo hii itakuwa imeepusha uhai na damu ya waTanzania kumwagwa hovyo na hawa watawala.

Kwa maana hiyo, gharama ya kazi hii itakuwa ni nafuu zaidi kuliko gharama wanayoweza kuilipa waTanzania baada ya hawa watawala kujihalalisha kuwa kwenye madaraka wakitumia njia haramu.

MTanzania, popote utakapokuwa, shiriki kuokoa taifa letu kutoka kwenye mikono ya watu waovu hawa.

Mungu Ibariki Tanzania.
Sahau pia kuhusu hili.
 
Watanzania wanaharakati wa Jf na X mnafurahisha kweli kweli.
Uzuri ni kwamba sasa tumeanza kuelewana lugha. Kwa hiyo tutakwenda vizuri sambamba hadi mwisho.

hivi ni kweli umefurahi, mkuu 'Mi mi'?

Kama ni kweli umefurahi, nami nakushukuru sana kwa furaha yako hiyo
Tanzania iliyo kombolewa ni furaha kwetu sote, au siyo, mkuu wangu!.
 
Hakuna kitu utafanya acha ujinga tafuta shughuli za kufanya.
 
Akitoka Samia atakuja mwingine kama unafikiri kuna Assad Tanzania endelea kufikiri hivyo hivyo.
Huu ni muendelezo wa furaha yako juu ya mada, au vipi?

Naona umepata mchecheto wa kipekee kabisa kutokana na unavyo onyesha mwenyewe hapa.

Naomba umfikishie Samia taarifa, ili na yeye tuone atakavyo unga nawe katika furaha yenu.
 
Hakuna kitu utafanya acha ujinga tafuta shughuli za kufanya.
Mtu mwenye furaha huwezi kuwa namna hii. Sasa unathibitisha ile tabia yenu mnayochangia na huyo Samia. Nyinyi ni watu laghai sana.
Hakuna jambo mnaloweza kuaminiwa nalo.
 
Wanasiasa na viongozi wa serikali wao wanadai polisi na jeshi watafanya usafi.
Hili mbona ndilo tangazo la kuzuia watu kwenda kwenye vituo vya kupigia kura. Maana watu wataona kabisa kwenda huko vituoni njiani watawabughudhi maaskari wafanya usafi!!!

Nadhani hapa waliotoa wazo hili hawajui kama "wanajipiga Risasi mguu"!
 
Back
Top Bottom