Gharama watakazoepuka watanzania wakichagua kutumia nishati ya gesi kupikia (M-Gas)

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Unapozungumzia nishati ya uhakika kwa ajili ya kupikia kwa watanzania, hauwezi kuacha kuutaja mkaa na kuni.

Watu wengi hutumia nishati hiyo kwa sababu ni rahisi kupatikana na wanaweza kumudu gharama yake tofauti na nishati nyingine kama gesi.

Kutumia gesi (M-Gas) wakati wa kupika chakula kuna raha yake, kwanza chakula kinaiva haraka, kinakuwa kisafi na vyombo havichafuki.

Mbali na kuokoa afya za watanzania dhidi ya madhara ya moshi, watanzania wataokoa fedha na mazingira watakapochagua kutumia gesi (M-Gas).

Kwa Masiliano zaidi: Piga +255747744895
 
Kiongozi hii m-gas ipo Zambia
Namba hii ya simu ni ya nchi gani??
 
Unapiga tu promo .gharama wala hazitifautiani sana
 
kinaiva haraka
Kinapoiva haraka hakiivi vizuri Ile uniformly,yaani both particles of atoms and molecules za liquid don't get heated equally Mana Ni sawa na unahatakisha.
Huo Moshi wa kuni mbona umetumika tokea Zama za mawe za kale mpaka saivi. Ama saivi ndio umepata akili kuliko miaka 90000000 iliyopita ama una shares zako huko kwa m-gas.
Ugali wa mkaa Ni tofauti kabisa na wa gesi sister.

Nyama iliyochomwa na Moto usipime . usitufanye watt wako Kama vipi kahonge wanasayansi uchwara waje kutoa ripoti zao uchwara na waonyeshe wagonjwa wakiwa hospital walivyougua kwa kutumia kuni.

TANZANIa bado subiria kwanza tuwe Kama ulaya. Boresha kwanza viwanda vitakavyotoa Ajira kwa watu ili maisha yawe Bora ndipo watapata hela ya kununua gesi yako ili unufaike kwa biashara yako
 
Gharama za M-gas zikoje?
Upatikanaje wake ukoje?
Nini tofauti kati ya M-gas na gesi zingine kwenye ujazo, ubora na gharama?

Bibi yangu aliyepo kule Geita vijijini ndani ndani, ambako hakuna umeme, hakuna barabara ya uhakika na maisha ni magumu, ni vipi achague kuitumia gesi badala ya mkaa au kuni?
 
Ahsante sana kwa ujumbe mzuri boss. Lakini lazima tukubali kwamba zama ZIMEBADILIKA. Hizi ni zama za gesi sio kuni na mkaa tena.
 
 
Naomba kuuliza gesi inanunuliwa kwa kiasi gani??
Mfano unit moja ya umeme ni sh kadhaa.
Je hio ges inauzwa kwa unit au ujazo..
Ujazo wa kg 15 ni bei gani?
 
Bora moshi utuue kuliko kuchangia mradi wa mafisadi. Gesi wameshatuibia sasa wakaiuze wanapopajua
 
Bora moshi utuue kuliko kuchangia mradi wa mafisadi. Gesi wameshatuibia sasa wakaiuze wanapopajua
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€Boss hakuna gesi iliyouzwa boss, gesi yetu bado ipo. Ukihitaji kuitumia nenda kaiombe TPDC boss wanatoa hiyo gesi kwa njia ya bomba kama maji ya DAWASCO.
 
So mna visima vyenu vya ges na meli zenu zinazoleta hiyo Ges Tanzania ? So Ges yenu ni cheap kuliko bei elekezi iliyopo Soko la Dunia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…