Gharama watakazoepuka watanzania wakichagua kutumia nishati ya gesi kupikia (M-Gas)

Nyinyi ni waongo na matapeli. Mmekata mfumo matumizi ya gas bila kujali salio la gesi alilokuwa nalo mteja kwenye mtungi. Wala kujali salio la kiasi cha pesa aliyolipa mteja kilichobaki kwenu? Tena mmekata bila kutoa maelezo wala tahadhari yoyote ile. Sasa hivi mteja akiwataarifu kuwa gesi imekata badala ya kumletea mtungi mwingine mnatuma mafundi wenu kuja kupora mtungi pamoja na salio la gesi na bila kurehesha pesa aliyolipa, huku mkidai mnaruhusiwa kuvunja mkataba muda wowote. Kama mnavunja mikataba na wateja kwanini hamjasitisha mfumo wenu wa kupokea malipo ya gesi badala yake manakata mfumo wa kumwezesha mteja kutumia gesi? Sijui kama EWURA ina taarifa na huu uhuni unaofanywa sasa hivi na hii kampuni ya mchongo. Jirani yangu alinyang'anywa mtungi wiki iliyopita baada ya kupiga simu gesi imekatq. Mama yangu amekatiwa gesi bila maelezo yoyote, salio lake linasoma zaidi ya shilingi elfu hamsini. Rudishieni wateja hela zao ndipo mvunje mikatqba, acheni wizi
 
Pole sana kwa changamoto iliyokupata ndugu. Nakushauri haya malalamiko uyapeleke ofisini M-Gas, na pia mkataba si unao tayari unaweza kukusaidia kupeleka malalamiko yako mahali popote. Pole sana kwa changamoto iliyokupata.
 
Nitumie zile connection za ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…