Gharama ya Kufanikisha Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024 – 2034) Jumla Kuu 4,554,015,000,000

Gharama ya Kufanikisha Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024 – 2034) Jumla Kuu 4,554,015,000,000

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Katika pitapita zangu nimekutana na hilo jarida la Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) nikaamua kuleta kwenu pia (doing my civic duty) document ni pdf ipo attached ila kwa ufupi naweka picha kwenye gharama zinazotazamiwa kutumika ili kufanikisha hilo jambo (baadhi ya picha za jedwari (binafsi nadhani pesa hizo tungeelekeza kwenye kuongeza usambazaji wa umeme na kupunguza bei ya umeme..., bei ikiwa rafiki mwanachi hatahitaji kuhamasishwa
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    65.4 KB · Views: 5
  • 2.jpg
    2.jpg
    63.4 KB · Views: 6
  • 3.jpg
    3.jpg
    56.7 KB · Views: 5
  • 4.jpg
    4.jpg
    54.8 KB · Views: 5
  • 5.jpg
    5.jpg
    57.4 KB · Views: 5
  • 6.jpg
    6.jpg
    59 KB · Views: 4
  • 7.jpg
    7.jpg
    72.1 KB · Views: 4
  • 8.jpg
    8.jpg
    68.5 KB · Views: 4
  • 9.jpg
    9.jpg
    63.7 KB · Views: 4
  • 10.jpg
    10.jpg
    72.3 KB · Views: 4
  • 11.jpg
    11.jpg
    66.1 KB · Views: 5
  • 12.jpg
    12.jpg
    40.4 KB · Views: 4
  • Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).pdf
    Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).pdf
    16.4 MB · Views: 6
1726420769702.png

Kuna mpaka programu ya uhamishaji wa upimaji wa VVU kwenye issue ya nishati safi ya kupikia..., hizo pesa si bora tungeongeza kwenye ruzuku ya rice cooker tukawapa wadau vijijini ?
 
1726421052664.png

Kwamba tunaendelea kuwekeza kwa kutumia pesa ili tuendelee kuagiza gesi kutoka nje ya kupikia wakati tuna nishati mbadala tayari nchini ?
 
Gesi inatoka nje kuja nchini, gesi yetu inafanya kazi gani?
 
Gesi inatoka nje kuja nchini, gesi yetu inafanya kazi gani?
Gesi yetu ni gesi asilia (methane) ambayo hata wewe unaweza kuipata kwenye Biogas Plants (kinyesi cha ngombe masalia yaliooza) tatizo gesi hii energy density yake sio kubwa yaani ukiweka kwenye ujazo uleule tuseme pipa haitapika kwa muda mrefu kama ukiweka LPG (Liquid Petroleum Gas) ambayo ndio tunaagiza.., Na itabiki compression iwe kubwa zaidi kwenye mtungi hivyo kupelekea uhitaji wa mitungi imara zaidi kwa gharama zaidi.

Kwahio kwa kutumia gesi yetu labda tutandaze mabomba kutoka source (inapochimbwa) kwa kwa mlaji au tuibadilishe iwe kiminika (LNG) na kuipeleka mpaka karibu inapotumika na kuibadilisha tena iwe gesi na kuitumia (gharama ni kubwa sana)

Kwahio ili kutumia gesi yetu ushauri wangu ni kuipeleka gesi hio mpaka vyanzo vya kuzalishia umeme na kufikisha nishati hio kama umeme kwenye kila kaya (hence watu wapikie kwa kutumia umeme)

 
Hapo nimekuelewa mkuu.

msambaza mkubwa wa LNG nchini ananufaikaje na uwepo wa gesi yetu?
 
Hapo nimekuelewa mkuu.

msambaza mkubwa wa LNG nchini ananufaikaje na uwepo wa gesi yetu?
Kwanza kabisa ili twende vizuri inabidi tuelewe kwamba gesi inatumia ujazo mkubwa sana kwahio kama unaweza kuicompress hio gesi ikawa hadi kimininika utapa gesi hio nyingi zaidi (kwahio katika usafirishaji na utunzaji hizi gesi zinatunzwa kama kimiminika) au kama una bomba kutoka gesi inapotokea mpaka kutumiwa hii ni bora zaidi sababu unapunguza matumizi ya nishati ya kuibadilisha kuwa kimininika

Sisi hatuna LNG (ingawa tuna mipango ya kuitengeneza kwa ajili ya mauzo ya nje) tuna gesi asilia ila ili uweze kupata ujazo mkubwa kwenye container ndogo inabidi kubadilisha Gasi asilia kuwa Kimiminika..., (LNG); sasa ni rahisi na gharama nafuu kubadilisha gesi ya propane (LPG) kuwa kimininika kuliko Gesi yetu asilia (Methane) kuwa kimininika LNG; Kufaidika na hii gesi Asilia ni labda kuibadilisha kuwa LNG na kuisafirisha kwenye manowari mpaka nchi za mbali zenye uhaba wa nishati na kuuza AU kuicompress hii gesi kuwa (CNG) na kuitumia kwenye magari (Compression yake sio kubwa)

Kwahio kuna mipango ya kutengeneza miundombinu ya gesi asilia kupitia kwenye mabomba kutoka inapozalishwa mpaka kutumiwa (ingawa kusambaza kila nyumba ni gharama kubwa na uzembe wetu wa kutunza miundombinu tunaweza kujikuta badala ya kuhifadhi mazingira tunayachafua kwa leakage (na pesa za kutandaza mabomba kila nyumba ni Pipe Dream) ni rahisi tusambaze nyaya za umeme kila nyumba... (Mfano gesi inayotumiwa na nchi za Ulaya ni gesi asilia ambayo inatokea Russia na kusafirishwa kwenye mabomba)
 
Back
Top Bottom