Gharama ya ujenzi darasa moja

Gharama ya ujenzi darasa moja

KABALEGA

Senior Member
Joined
Jul 18, 2017
Posts
164
Reaction score
104
Kichwa cha habari chajieleza,

Wandugu, wataalam na wazoefu wa ujenzi naomba mnisaidie,

Je ni tofali ngapi za block zinatakiwa kujenga chumba kimoja cha darasa? Kuna fundi aliniambiai inatakiwa tofali 1800 na mwingine akanambia tofali za block 1650, sasa nimebaki njia panda nikaona ni vyema nije humu kuwauliza mafundi ili nipata exposure na kuepuka kuibiwa, pia ili naweza pata fundi humu humu ambae pengine si mpigaji na kama tutaridhiana na kukubaliana.

Ni hayo tuu ndugu zanguni, ahsanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona tofauti si kubwa kiasi cha kukutisha hivyo! Tofauti ya matofali 150 haifiki laki 2. Mara nyingi hayo ni makisio. Siyo lazima upate idadi kamili. Mi nashauri fanya budget ya matofali 1800 ambayo ndo kiwango cha juu. Ninalojua mfuko mmoja wa sementi unajenga matofali 70. Na eneo la mraba la ukuta kinachukua matofali 8. Sasa kokotoa eneao la mraba la darasa ambalo kulingana na standard za wizara ya elimu darasa ni mita 7 kwa mita 9. Usisahau kuondoa eneo pa madirisha la milango. Halafu kwasababu darasa lina gable kuna matofali mengine yatakatwa. Ndiyo maana unachopewa ni estimates.

Darasa linaukubwa gani? Unaposema darasa tu hata humu hatuwezi kukusaidia,weka dimensions

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona tofauti si kubwa kiasi cha kukutisha hivyo! Tofauti ya matofali 150 haifiki laki 2. Mara nyingi hayo ni makisio. Siyo lazima upate idadi kamili. Mi nashauri fanya budget ya matofali 1800 ambayo ndo kiwango cha juu. Ninalojua mfuko mmoja wa sementi unajenga matofali 70. Na eneo la mraba la ukuta kinachukua matofali 8. Sasa kokotoa eneao la mraba la darasa ambalo kulingana na standard za wizara ya elimu darasa ni mita 7 kwa mita 9. Usisahau kuondoa eneo pa madirisha la milango. Halafu kwasababu darasa lina gable kuna matofali mengine yatakatwa. Ndiyo maana unachopewa ni estimates.

Sent using Jamii Forums mobile app
Poa kaka ,shukrani

Mkuu hapa kwa Square meter naomba nieleweshe kidogo.
Kwa darasa la sq. meter mfano upana 7 na urefu 9 ina maana ni Sq. meter 63. Kwa asumption ya tofali 8 kwa sq. meter 1 hapo unapata tofali 504 tu???
 
anamaanisha pima mita 7 kuta 2 na mita 9 kuta2
kisha zidisha kozi ngapi then ondoa eneo la dirisha
kwa ujenzi wa kawaida kila tofali 70 utatumia mfuko 1 wa cement
hapo utapata idadi ya cement na matofali
na mafundi kila tofali wanajenga kati ya 250 hadi 500 inategemea na mkoa uliopo na stage ya ujenzi kadri kozi zinavyokuwa juu na bei inapanda
 
Tofali 70 mfuko 1!!!?
Mkuu hiyo itakuwa ni bonding au unataka jengo liporomoke!?
 
Consider hizi assumptions

Brick size 430*230
Opening 13.5m²
Wall height 3.5m
Wall size 98.5m²

Total brick 1030
 
Back
Top Bottom