Pre GE2025 Gharama ya Usajili wa Vyama vya Siasa Nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa nchini inadaiwa kuongeza gharama za usajili kwa asilimia 9,900, gazeti la JAMHURI limeelezwa.

Awali, gharama za usajili zilikuwa ni Sh 25,000 kwa usajili wa muda na Sh 50,000 tu kwa usajili wa kudumu, lakini sasa taarifa zinadai kuwa gharama wa muda zimeongezeka hadi Sh 1,000,000 huku usajili wa kudumu ukifika Sh 5,000,000, sawa na ongezeko la asilimia 9,900.

Akimzungumza na JAMHURI, mwanachama wa chama kipya cha siasa kinachotafuta usajili cha Independent People's Party (IPP) Andrew Bomani, anasema gharama za usajili zimepanda kwa kiasi cha "Ajabu ni kwamba nikumbuka kama kumewahi kutolewa tangazo lolote kwa umma kuhusu ongezeko hili."

"Lakini kitu kingine ambacho Watanzania wanapaswa kukifahamishwa ni kwamba, kwa takriban miaka 10 sasa hakuna chama kipya kilichopata usajili, iwe ni wa muda au kudumu," anasema Bomani.

Anasema IPP wamesilisha maombi ya usajili kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, lakini hadi sasa hakijapata majibu.

JAMHURI limeiona risiti ya benki ya malipo ya kiasi hicho cha fedha kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, malipo yaliyofanywa Septemba 1, 2023.

Mutungi.png

"Hatujui ni mchakato gani unaendelea na sababu za kunyimwa usajili wa muda ilhali tayari wameshakamilisha ada stahiki," anashangaa Bomani.

Soma pia:
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ifanyiwe mabadiliko makubwa

Juhudi za viongozi wa IPP kupata haki zimekuwa zikikwamishwa na danadana kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

JAMHURI limemtafuta Msajili, Jaji Francis Mutungi, kwa njia ya simu bila mafanikio. Na alipoandikiwa ujumbe kwa njia ya simu kutaka kupewa sababu za kupandisha gharama na ni kwa nini hakuna chama kipya kilichosajiliwa kwa muda mrefu huku hata waliolipa ada wakinyimwa usajili, alimwelekeza mwandishi wa habari hii kwenda maktaba ya Ofisi ya Msajili kupata majibu.

Kwa upande mwingine, viongozi wa IPP wamemwandikia barua Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kuomba msaada wa kisheria ili wapate haki ya usajili. Sehemu ya barua hiyo inasomeka: "Sisi waanzilishi wa IPP tumeshuhudia mambo ya ajabu sana katika harakati za kuomba usajili wa chama chetu."

"Tuliwasilisha maombi Mei 4, 2023. Baada ya hapo tumekuwa tukihangaika sana kufuatilia kutaka kupata majibu.
Kwa mujibu wa kipengele namba 4 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ORPP, inatakiwa kutoa majibu ndani ya siku 30."

"Wakati huo huo, ORPP inatakiwa inafanya uhakiki kuhusu uraia wetu, nk. Hilo halijafanyika mpaka leo. Hata (Ofisi ya Msajili) kujibu barua mfano barua yetu ya mwisho ya Machi 1, 2024, sasa inafika miezi mitano na haijajibiwa."

"Na hata hapo nyuma walipokuwa wanajibu barua baada ya miezi miwili au zaidi, tuliwahi kuambiwa kuhusu Public Service Charter kwa watumishi wa umma. Ni wazi wanakiuka huo muongozo."

Barua hiyo iliyoandikwa na Bomani na Gregory Urima wanaojitambulisha kama waanzilishi wa Chama cha IPP inasomeka:

"Kwa mujibu wa tovuti ya ORPP, usajili wa muda ni Sh 25,000 na wa kudumu ni Sh 50,000. Lakini sasa usajili wa muda ni Sh milioni 1 na wa kudumu Sh milioni 5.
Tuliahidiwa kuwa sheria ilibadilishwa mwaka 2019 kipindi cha Magufuli. Lakini licha ya kulipia, hakusaidia lolote."

"Niongeze kwamba kilio chetu si tu kuhusu IPP bali hata na wengine walioomba kusajili tangu kipindi cha Magufuli. Na inawezekana hamjui kwamba mara ya mwisho chama cha siasa kusajiliwa nchini ni mwaka 2014. Nacho ni ACT Wazalendo."

"Ni kana kwamba mamilioni ya Watanzania wameridhika kabisa na vyama vilivyopo kitu ambacho siyo kweli. Katika hali hiyo kuna haja gani ya kuwalipa mishahara watu ambao hawafanyi kazi yoyote?"

"Kutokana na hii hali ya sintofahamu kubwa, IPP inajilazimisha kutafuta msaada wa kisheria."

"Mara ya kwanza tuliwaendea Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) baada ya TLS chini ya Bwana Sangusia kutuonyesha ushirikiano."
LHRC angalau walisaidia kuwaandikia barua ORPP kujaribu kupata maelezo fulani kutoka ofisi hiyo. Mpaka sasa barua yao haijajibiwa."

"Ombi letu kwa TLS kama taasisi mama ya sheria nchini ni kutafuta njia yoyote zaidi ya kutusaidia sisi na ndugu zetu wa vyama vingine."

"Tumeambatanisha nakala ya umuhimu kwenye ofisi yenu. Hii hali inaweza kupeleka nchi kuingia kwenye vurugu isiyo ya lazima kutokana na utawala wa sheria kupuuzwa na serikali."

Source: Jamhuri
 
Wangeweka hatia Milioni 100 ili vyama uchwara vya kusifia visiwepo
CCM nddio inayounda hivyo vyama vya kusifia, hivyo hata wakiweka ada Ts billion itawalipia , ili kuihadaa dunia kwamba Tanzania kuna vyama vingi kumbe ni matawi ya CCM
 
Vyama vilivyopo vingi, vipo kama havipo, sijui wao watakuja na maajabu gani?
 
Ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa nchini inadaiwa kuongeza gharama za usajili kwa asilimia 9,900, gazeti la JAMHURI limeelezwa.

Awali, gharama za usajili zilikuwa ni Sh 25,000 kwa usajili wa muda na Sh 50,000 tu kwa usajili wa kudumu, lakini sasa taarifa zinadai kuwa gharama wa muda zimeongezeka hadi Sh 1,000,000 huku usajili wa kudumu ukifika Sh 5,000,000, sawa na ongezeko la asilimia 9,900.

Akimzungumza na JAMHURI, mwanachama wa chama kipya cha siasa kinachotafuta usajili cha Independent People's Party (IPP) Andrew Bomani, anasema gharama za usajili zimepanda kwa kiasi cha "Ajabu ni kwamba nikumbuka kama kumewahi kutolewa tangazo lolote kwa umma kuhusu ongezeko hili."

Anasema IPP wamesilisha maombi ya usajili kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, lakini hadi sasa hakijapata majibu.

JAMHURI limeiona risiti ya benki ya malipo ya kiasi hicho cha fedha kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, malipo yaliyofanywa Septemba 1, 2023.

"Hatujui ni mchakato gani unaendelea na sababu za kunyimwa usajili wa muda ilhali tayari wameshakamilisha ada stahiki," anashangaa Bomani.

Soma pia:
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ifanyiwe mabadiliko makubwa

Juhudi za viongozi wa IPP kupata haki zimekuwa zikikwamishwa na danadana kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

JAMHURI limemtafuta Msajili, Jaji Francis Mutungi, kwa njia ya simu bila mafanikio. Na alipoandikiwa ujumbe kwa njia ya simu kutaka kupewa sababu za kupandisha gharama na ni kwa nini hakuna chama kipya kilichosajiliwa kwa muda mrefu huku hata waliolipa ada wakinyimwa usajili, alimwelekeza mwandishi wa habari hii kwenda maktaba ya Ofisi ya Msajili kupata majibu.

Kwa upande mwingine, viongozi wa IPP wamemwandikia barua Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kuomba msaada wa kisheria ili wapate haki ya usajili. Sehemu ya barua hiyo inasomeka: "Sisi waanzilishi wa IPP tumeshuhudia mambo ya ajabu sana katika harakati za kuomba usajili wa chama chetu."

"Wakati huo huo, ORPP inatakiwa inafanya uhakiki kuhusu uraia wetu, nk. Hilo halijafanyika mpaka leo. Hata (Ofisi ya Msajili) kujibu barua mfano barua yetu ya mwisho ya Machi 1, 2024, sasa inafika miezi mitano na haijajibiwa."

"Na hata hapo nyuma walipokuwa wanajibu barua baada ya miezi miwili au zaidi, tuliwahi kuambiwa kuhusu Public Service Charter kwa watumishi wa umma. Ni wazi wanakiuka huo muongozo."

"Niongeze kwamba kilio chetu si tu kuhusu IPP bali hata na wengine walioomba kusajili tangu kipindi cha Magufuli. Na inawezekana hamjui kwamba mara ya mwisho chama cha siasa kusajiliwa nchini ni mwaka 2014. Nacho ni ACT Wazalendo."

"Ni kana kwamba mamilioni ya Watanzania wameridhika kabisa na vyama vilivyopo kitu ambacho siyo kweli. Katika hali hiyo kuna haja gani ya kuwalipa mishahara watu ambao hawafanyi kazi yoyote?"
hivi
"Kutokana na hii hali ya sintofahamu kubwa, IPP inajilazimisha kutafuta msaada wa kisheria."

"Mara ya kwanza tuliwaendea Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) baada ya TLS chini ya Bwana Sangusia kutuonyesha ushirikiano."
LHRC angalau walisaidia kuwaandikia barua ORPP kujaribu kupata maelezo fulani kutoka ofisi hiyo. Mpaka sasa barua yao haijajibiwa."

"Tumeambatanisha nakala ya umuhimu kwenye ofisi yenu. Hii hali inaweza kupeleka nchi kuingia kwenye vurugu isiyo ya lazima kutokana na utawala wa sheria kupuuzwa na serikali."

Source: Jamhuri
hivi Tundu Lisu kinachomfanya asisajili chama ni nini?
 
Back
Top Bottom