Gharama za ada ya usajili wa huduma za technolojia TCRA zinakatisha tamaa wabunifu wanaoanza (start-up innovators)

mackj

Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
84
Reaction score
98
Serikali kupitia mamlakaya mawasiliano nchini TCRA inahimiza wabunifu kubuni huduma mbalimbali za kiteknolojia ili kuchochea kasi ya maendeleo na kuboresha huduma ili kurahisisha maisha

Lakini kikwazo kikubwa ni ughali wa leseni za usajili wa huduma hizo za kibunifu kwa wabunifu wanaoanza yaani start-up innovators, mfano kwa huduma ya usajili wa USSD (Unstructured Supplementary Service Data) na short code kupitia Tanzanite portal, ada ya maombi yaani Application Fee ni U$D 10, ada ya usajili yaani Registration fee ni U$D 2000, na ada malipo ya huduma kwa mwaka yaani annual maintenance fee ni U$D 2500 , ambayo kwa jumla yake ni zaidi 12Milion fedha za kitanzania.

Hapo bado hujanunua gate way, hujanunua shared USSD, kwa kampuni za hosting na kuhost huduma yenyewe, hujalipa (callback URL), kwa kweli kwa gharama hizi wabunifu wanaoanza hawawezi kumudu na mbaya zaidi ni huduma hizi kutozwa kwa dola

Mfano ni hivi karibuni nimebuni huduma ya kuriport taarifa za uwepo wa viashiria au vitendo vya moja kwa moja vya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani vinavyo sababisha ajali zinazo pelekea vifo na majeruhi, kwa njia ya USSD short code, ambapo mwananchi au abiria anakuwa snatuma ujumbe mfupi kwa njia ya SMS kupitia hiyo shortcode/ USSD menu, ili kuzuia ajali na kuokoa maisha na kuzifanya barabara zetu kuwa sehemu salama.

Huduma hii niliwasilisha kwa wadau wa usalama barabarani na ikapata mapokeo chanya lakini changamoto ikawa upatikanaji wa pesa hiyo, nikakwama.

Kufuatia hali hii naishauri serikaali iondoe ada hizi kwa wabunifu wanaonza kwakuwa wanakuwa katika majaribio ya huduma zao kwa kipindi cha miezi 3 chini ya TCRA na COSTECH, na waruhusiwe kuhost huduma zao ili wawe chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja na baada ya hapo ndio walipe gharama hizo, kwakuwa wanaweza kuwa wamepata ufadhili au kuuza huduma zao kwa wadau mbalimbali wa teknolojia ya habari na mawasiliano na kuwa na mtaji wa kusajili rasmi huduma zao.
 
"Any government is an organ of exploitation by nature."

Mikhail Bukanin
 
HUU ni ushauri mzuri Ila sidhani km wataupokea na kuufanyia kazi
 
Nyie si mnasemaga siasa haziwahusu?mnafundishwa Kwa vitendo sasa
 
Umeuliza maswali Mengi kwa wakati mmoja Ila nitakujibu 1 TU hilo la kwanza kwanini Serikali ya Tanzania haitaki vijana wa kitanzania watoboe, Ila nitakujibu kwa kituo Serikali inapita humu ikiliona swali lako itakujibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…