KERO Gharama za “Ambulance” Shinyanga ni mateso kwetu walalahoi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Zimekuwepo jitihada za Serikali na wadau wa Sekta ya Afya kusambaza Magari ya kubebea Wagonjwa (Ambulance) na sasa ukienda hospitali nyingi unakuta magari hayo, lakini kwa hapa Shinyanga licha ya uwepo wa magari hayo lakini gharama zake sio stahimilivu kwa Mwananchi wa chini.

Mfano Hospitali ya Mkoa Wananchi wanatozwa Shilingi 200,000/= hadi 300,000/= kwa ajili ya kusafirisha mgonjwa kumtoa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kumpeleka Hospitali ya Kanda ya Bugando.

Kibaya zaidi, jambo ambalo linafanya niwaze kwamba kuna mazingira ya upigaji na kutotanguliza huduma mbele, ni kwamba unakuta mara nyingi rufaa zinakuwa tatu hadi nne, yaani watu watatu hadi wanne wanasafirishwa kwa pamoja kwenye gari moja na kila Mtu anatakiwa kuchangia laki mbili na nusu.

Sio mbaya wananchi kuchangia gharama za mafuta lakini sidhani kama wanatakiwa kutozwa gharama kubwa kiasi hicho, wakati wanajumuishwa kwa pamoja na kusafiri kwenye gari moja, ambapo watu watatu wote wakitozwa laki mbili na nusu inakuwa laki 750,000/=.

Imefikia wakati wananchi au mgonjwa akisikia anatakiwa kupewa rufaa kwenda hospitali ya Kanda ya Bugando anaomba kubakia hospitalini hapo kwa kuhofia kutokumudu gharama za ambulance jambo ambalo sidhani kama ni salama.

Familia nyingine zimejikuta zikiuza baadhi ya mali ili kumudu gharama hizo ambazo kwa jamii nyingi za huku vijijini ni kubwa kulingana na hali ya maisha ilivyo kwa sasa.

Wito wangu kwa Serikali kupitia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu naomba wachunguze kwa kina suala hili, ikiwezekana Waziri afike kwenye hospitali hiyo ya Mkoa awasikilize malalamiko hayo kwa wananchi awaondoe hofu.

Pia Serikali ni vyema ikaweka na kusisitiza utaratibu wa wazi ambao utaondoa hofu kwa wananchi kujua namna ya kuchangia huduma za ambulance kulingana na eneo pamoja na mazingira ya uhitaji wa huduma hiyo, kuliko kinachoonekana kwa sasa hasa kwenye hospitali hiyo Watu kujipangia gharama na kutofautiana baina ya Mtu na Mtu hali ambayo inafikirisha zaidi.

Maana vitendo vyenye viashiria vya ubadhirifu kama hivyo vinaweza kuwa vinafanywa na watendaji wachache kwa maslahi yao binafsi na kufanya wananchi wakose imani Serikali yao au viongozi kwa kushindwa kuwajibika kusikia kilio chao.

Ufafanuzi wa Hospitali ~ Hospitali ya Mkoa Shinyanga yafafanua madai ya kutoza gharama kubwa kwa wanaohitaji Ambulance

2. Waziri Ummy : Wagonjwa wasitozwe gharama za posho ya dereva wala muuguzi ambao usindikiza mgonjwa na ambulance
 
Huna number ya mganga mfawidhi uiweke hapa Kila mwana jamvi ampigie Kwa muda wake nadhani ataelewa tu kwamba hakuna pesa ya Bure.

Kuna Uzi wetu kule unaitwa Jamii forum usiku wa manane Nako weka no yake apigiwe simu usiku wa manane tumhoji Hadi kesho kasha badiri laini kabisa na kuacha utapeli
 
Mkuu asante kwa kupaza sauti nafikiri humu ndani wahusika wapo lakini pia kuna viongozi Serious kama Mama yetu Dk Gwajima tumeshuhudia mara nyingi wakichukua hatua stahiki mara moja hivyo kwa namna ya kipekee kabisa nikuombe dada angu Dk Gwajima ujaribu japo kuwastua hawa mabwana japo sio wizara yako direct lakini mimi binafsi nna imani na wewe.
 
Zimekuwepo jitihada za Serikali na wadau wa Sekta ya Afya kusambaza Magari ya kubebea Wagonjwa (Ambulance) na sasa ukienda hospitali nyingi unakuta magari hayo, lakini kwa hapa Shinyanga licha ya uwepo wa magari hayo lakini gharama zake sio stahimilivu kwa Mwananchi wa chini.

Mfano Hospitali ya Mkoa Wananchi wanatozwa Shilingi 200,000/= hadi 300,000/= kwa ajili ya kusafirisha mgonjwa kumtoa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kumpeleka Hospitali ya Kanda ya Bugando.

Kibaya zaidi, jambo ambalo linafanya niwaze kwamba kuna mazingira ya upigaji na kutotanguliza huduma mbele, ni kwamba unakuta mara nyingi rufaa zinakuwa tatu hadi nne, yaani watu watatu hadi wanne wanasafirishwa kwa pamoja kwenye gari moja na kila Mtu anatakiwa kuchangia laki mbili na nusu.

Sio mbaya wananchi kuchangia gharama za mafuta lakini sidhani kama wanatakiwa kutozwa gharama kubwa kiasi hicho, wakati wanajumuishwa kwa pamoja na kusafiri kwenye gari moja, ambapo watu watatu wote wakitozwa laki mbili na nusu inakuwa laki 750,000/=.

Imefikia wakati wananchi au mgonjwa akisikia anatakiwa kupewa rufaa kwenda hospitali ya Kanda ya Bugando anaomba kubakia hospitalini hapo kwa kuhofia kutokumudu gharama za ambulance jambo ambalo sidhani kama ni salama.

Familia nyingine zimejikuta zikiuza baadhi ya mali ili kumudu gharama hizo ambazo kwa jamii nyingi za huku vijijini ni kubwa kulingana na hali ya maisha ilivyo kwa sasa.

Wito wangu kwa Serikali kupitia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu naomba wachunguze kwa kina suala hili, ikiwezekana Waziri afike kwenye hospitali hiyo ya Mkoa awasikilize malalamiko hayo kwa wananchi awaondoe hofu.

Pia Serikali ni vyema ikaweka na kusisitiza utaratibu wa wazi ambao utaondoa hofu kwa wananchi kujua namna ya kuchangia huduma za ambulance kulingana na eneo pamoja na mazingira ya uhitaji wa huduma hiyo, kuliko kinachoonekana kwa sasa hasa kwenye hospitali hiyo Watu kujipangia gharama na kutofautiana baina ya Mtu na tena Mtu hali ambayo inafikirisha zaidi.

Maana vitendo vyenye viashiria vya ubadhirifu kama hivyo vinaweza kuwa vinafanywa na watendaji wachache kwa maslahi yao binafsi na kufanya wananchi wakose imani Serikali yao au viongozi kwa kushindwa kuwajibika kusikia kilio chao.
Ni sawa tu tena hiyo mbona ni ndogo!! Wafanye hata laki tano kwa kila mgonjwa, hadi wananchi akili zitakapowakaa sawa, kenge hasikii hadi aone damu kwenye masikio!! Kila siku si ndio mnasema sasa mambo ni shwari kila kona?!!
 
Hii tabia pia ipo hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro. Unaandikiwa rufaa kwenda Muhimbili unaambiwa 350K na hapo unakuta mko watatu au wanne.
 
"Mfano Hospitali ya Mkoa Wananchi wanatozwa Shilingi 200,000/= hadi 300,000/= kwa ajili ya kusafirisha mgonjwa kumtoa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kumpeleka Hospitali ya Kanda ya Bugando."
 
Back
Top Bottom