Salamu Wakuu:
Nahitaji kujielimisha kuhusu gharama za kupiga plasta ile wanasema ni ya kisasa ikiwa ni mchanganyiko wa Cement + Sand + Gypsum. Hii wanasema ndio bora na inakusugua kwingi.
Tuchukulie kuwa jengo lina vyumba vya kulala vinne alafu na sebule. Pia ukuta umefika hadi meter tatu (high ceiling) na eneo la sakafu la nyumba ni square meter 250.
Jee hiyo itakuwa kiasi gani kwa makadirio tu. Yaani kiwango cha chini alafu cha juu (Labor Cost Price Range)
Hapa naongelea Labor charge ya mafundi. Au Nguvu Kazi.
Ahsanteni
Mdoe Haji
hata mafundi wa mil 1.5 wanapatikana...ni ngumu kukadiria...maana kila fundi ana kiwango tofauti cha faida anayoitaka.....ila kwa uhakika ni kua hata milioni 1 na nusu unaweza kufanyiwa hiyo kazi.
Aisee kama ndo bei unazolipaga kwenye ujenzi utakua unatumia gharama sana..pengine unajenga nyumba mbili..yako na ya fundi....jaribu kuzunguka zunguka kidogo kuuliza mafundi wengineAndaa takribani M. 2.5, kwa mujibu wa fundi ninayemfahamu kazi kubwa iko ndani kuliko nje ya nyumba...
Si unajua tena fundi kabila moja na wife, na ushemeji humo humo. Mkuu kama vipi nipe mawasiliano ya fundi nafuu kuna kibanda kingine nataka nianze ujenzi Boko...Aisee kama ndo bei unazolipaga kwenye ujenzi utakua unatumia gharama sana..pengine unajenga nyumba mbili..yako na ya fundi....jaribu kuzunguka zunguka kidogo kuuliza mafundi wengine