Gharama za kufunga ndoa mkoani Arusha.

Gharama za kufunga ndoa mkoani Arusha.

Mzee km huna Tembo Card Master Card ujue hutafanya chochote! Mpunga ndio kila kitu!
 
Habari za jioni wanajamvi.
Mimi ni kijana wa makamo na nimedhamiria kuchukua 'jiko' yaani mke mwakani.kwa wale wenye majiko au wazoefu wa kamati za harusi naomba msaada wenu katika hili.
Ukizingatia mimi ni mtumishi wa umma mwenye kipato cha wastani ningependa kujua ni kiasi gani cha fedha(makadirio) ninahitaji kuwa nacho mimi kama mimi kabla sijaenda kujitambulisha ukweni?
Naomba tuelezane kuhusu gharama za ukumbi,vyakula,vinywaji,mavazi ya maharusi,usafiri,mc,n.k

ningependa harusi ifanyikie mjini arusha lakini kama kuna sehemu ambayo gharama zake ni cheaper naweze kuangalia uwezekano wa kufanyia huko.
N.B ndoa itakua ya kikristu.

Naamini michango yenu itasaidia wadau wengi walioko kwenye mchakato wa kufunga ndoa.
Hili si suala la kuuliza,wewe mwenyewe unajua unataka harusi yako iwe vp kulingana na hela ulizonazo
 
Mie sikuchangiwa na mtu nilijigharamia mwenyewe. Watu waliohudhuria karibu wote walituzawadia bahasha kwa mapenzi yao wenyewe na ndani kulikuwa na chochote. Kwa hiyo nikajikuta nimerudisha gharama yote ya harusi na kubakiwa na kitu chochote.

Sema inategemea sana na unayemuoa, kama ndio wale wanaotaka harusi za show off kama ya Prince William na Kate Middleton wakati uwezo wenu ni wa raia wa kawaida basi jua pesa itawatoka sana na pengine gharama isirudi.

I did it simple na kila aliyehudhuria alifurahi sana. Presha ya kufatilia michango sikuwa nayo.

NB: Huwa sichangii harusi yoyote, ila nikipewa kadi ya mwaliko wa sherehe naenda na natoa zawadi kwa maharusi jinso moyo wangu utakavyonituma.
 
Kwanza hongera sana kwa kuamua kuingia uwanjani KUIJAZA DUNIA kama amri kuu tuliyopewa.
la msingi mwenza wako ndio atakusaidia mfanye harusi ya aina gani,kumbuka kumtanguliza mbele kwenye maamuzi yako vinginevyo utachemka mapema.
Harusi ndio kila kitu kwa mwanamke...kama amehudhuria sherehe 20 za harusi basi kila moja alikuwa anafanya sampling ya jambo gani zuri kalipenda na atalifanya pia kwenye harusi yake mathalani sare,mapambo,staili ya keki nk.
so,msikilize na baadae muamue kwa kutegemea nguvu ya uchumi wenu ili msije ingia na madeni kwenye ndoa.
inabidi uwe umejiimarisha kidogo kwani umesema hata kwao hujaenda kwani kuna hatari wazazi wakaweka ngumu kama kuna dalili za binti yao kula ugali na picha ya samaki.
Mungu akubariki sana na akufanyie wepesi ufanikiwe.
lastly,Pray Hard brother.
God listens.
 
mkuu mchango wako unatia nguvu na utulivu wa moyo.
 
Sie wengine bado 2po 2po kwanza, we can tell you nothing, alafu kuoa cku hizi ni kipaji eeh! Au kama vp nitafute twende zetu ktk viti virefu vya counter then kukaidhabu hiyo hela ulinayo mpk sasa, alafu ujue kama huna gx 100, kama wee c wakili, na kama huna mjengo, bac imekula pande yako chalii yangu.
 
Unaweza fanya harusi ya 3m na ukaita watu mia tu, ukumbi wa kawaida huko sinza zipo, kama utoji au lulu ni laki 250-300. vinywaji boxi tatu za wine 75,000. gari la harusi chukua corora tu 50000. soda crate 20*12500, chakula weka ndizi na nyama za kukaanga,bagia na kachumbali kwa sh 2000.mc chukua wa uswahilini laki mbili zinamtosha, duuu inabana sana ila unaweza ukajibana nayo.hahahahahahaha
kwenye kikao ingalau utoe laki tano
 
promising!
 
Back
Top Bottom