Gharama za kumiliki kifo

Hapa nimeandika tu na sijataja mtu au kutoa mfano hata mmoja! Ningefanya hivyo tuu..😂 pasingetosha... Ningetapikiwa mpaka miguuni🤪
In JF na katika maisha ya kawaida jifunze kukwepa mitego ya haters na maadui kwa kufanya mambo kwa tafakuri na 'exclusivity' kwq kufanya hivyo utabaki na silaha muhimu ya 'kuwapiga bila kuwagusa'🚶🏿
EXPERIENCE MATTERS 💪🏿
 
 
Ive been to south Africa, where gun violence is eminent.
Bastola ni moja ya kitu hatari sana kumiliki hasa kama una hasira
Ukiingia kumbi za starehe kule kuna sehemu maalum ya kukabidhi silaha
 
Ukiingia kumbi za starehe kule kuna sehemu maalum ya kukabidhi silaha
Na bado humo humo kwenye ukumbi unaweza ukapigwa chuma ukizingua, usiamini kabisa ule ukaguzi wa metal detectors kwa wale securities, ule ni kwa wanyonge ni kwa mimi na wewe , wababe wanapita na silaha pale pale.
 
Hakika nakubaliana na wewe
Christmas ya 2005 nusura igeuke kilio kwenye familia ya mshkaji wetu mmoja
Jamaa alikuwa ana miliki mguu wa kuku.. Ile tar 24 kuqmkia tar 25 akawa kaikoki vema tayari kwa wezi na majambazi( kipindi kile kulikuwa na kuvamiwa vamiwa)
Kaikoki vema kaweka chini ya mto kalala? Asubuhi kuamka zikawa ni harakati za kanisani.. Mchana wake katukaribisha lunch nyumbani kwake

Tukiwa tuko sebuleni pale tunapiga story.. Watu kama sita hivi tulikuwa. Mara ghafla katokea vyumbani mwanae mdogo na bastola kaishika vizuri kwa mikono yote kainyanyua juu
Kufika sebuleni kamnyooshea baba yake direct anamwambia kiutani DAD HANDS UP!
Kilichotufanya tujue kuna tatizo ni vile jamaa alivyobadilika ghafla na kutumbua macho yote mawili kama panya aliyebanwa mlangoni
Zilikuwa sekunde kadhaa ngumu sana kwetu sote mke ndani.. Kuna ukimya mkuu wa ghafla ulitawala huku dogo akiendelea kusisitiza baba anyooshe mikono juu
Pona yake ni ujasiri wa house girl aliyetokea kwa nyuma, na kuinua juu zaidi mikono ya dogo na tukasikia paah!
Bastola haikuwa kwenye safety catch.. Rossi ilikula kioo cha dirisha na kupotelea nje!
Dogo hajui nini kimetokea analia tuu.. Baba mtu kalala chini kaficha macho.. Wageni hatujui kwa hakika ninini hasa kilikuwa kimeleta yote hayo
Mama katoka jikoni mbio
Hali ilipotulia jamaa alilia sana! Tarehe 27 yake mapema asubuhi Jamaa akairudisha silaha polisi Oysterbay
Dada wa kazi ndio alikuwa bingwa wa mchezo
 
Na bado humo humo kwenye ukumbi unaweza ukapigwa chuma ukizingua, usiamini kabisa ule ukaguzi wa metal detectors kwa wale securities, ule ni kwa wanyonge ni kwa mimi na wewe , wababe wanapita na silaha pale pale.
Nilishawahi kufanya hivyo Ukumbi mmoja mitaa ya Zithobeni.. Na bastola ndio iliniokoa (niliisimulia hapa)
 




Duh!!! Hakika hii ilikuwa kiboko na kubwa kuliko .

Tunaendelea kujifunza zaidi
 
Duh!!! Hakika hii ilikuwa kiboko na kubwa kuliko .

Tunaendelea kujifunza zaidi
Nine interact na silaha for more than 20 years.. Kama unaishi maisha ya kawaida.. Silaha ni mzigo mzito unsohitaji ulinzi sawa tu na tunguli..
Unaimiliki ili ikusaidie ulinzi na kujihami lakini yenyewe haiwezi kujilinda
Ukiibeba unailinda usije ukaporwa
Ukiimiliki unailinda isije ikaibiwa😂
Mwisho wa siku unajikuta badala ikulinde wewe...! Wewe ndio unailinda
 
Niliwahi kushuhudia jamaa akiua mke na mtoto wake then na yeye akajimaliza, ilikuwa jhb downtown.
Ilikuwa tar 23 dec, , wa south wanadesturi ya kurudi locations makwao kama wanavyofanya wachaga kipindi cha sikukuu za christmass hapa kwetu, tar hiizo zinakuwaga busy shopping days sasa mshakji wameshuka kwenye gari kali mpya, yeye na mke wake wakaingia maduka kadhaa, sasa nadshni kuliyokea sintofahamu baina yao wakiwa duka flani ndani, mwanamke akatoka nje huku akiwa anamfokea jamaa, jaa kila. akimsihi mkewe apoe nido kama anamzidisha , tukasikia mlio paa,, paa!! Jamaa kaua mkewe ya pili mwanae wa kike, watu walivyomzonga na yeye akajimaliza.
Ndani ya nusu saa, kidude kidogo kimesababisha misiba mitatu kwenye familia moja, niliichukia bastola toka siku hiyo.
 
Na shida ya South silaha zimetapakaa kila mahali na udhibiti ni mdogo! Imagine mimi nilinunua kwa Rand 200 miaka ile ya 98.. Kwenye black market lakini
 
VICHAI..........
Mmiliki wa Leicester City

Kobe ......

Noma sana
 
Kwangu Mimi hapo huyo dada wa kazi ningempandisha cheo haraka kutoka kuwa house girl mpaka msimamizi wa Mambo ya usalama nyumbani na starehe stukizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…